Inter Press Service News Agency
Wednesday, April 25, 2018   07:57 GMT    
   Homepage
   World Service
   East Africa
   Southern Africa
   West Africa
   Central Africa
 
   Environment
   Health-HIV/AIDS
   Education
   Rights
   Politics
   Economics
   and Finance
   Development
   Energy
   Population
   Culture
 
   Radio Service
 
   Français
 
   About IPS
 
   ENGLISH
   ESPAÑOL
   FRANÇAIS
   ARABIC
   DEUTSCH
   ITALIANO
   NEDERLANDS
   PORTUGUÊS
   SUOMI
   SVENSKA
   SWAHILI
   TÜRKÇE
PrintSend to a friend
Readers Opinions


Umoja wa Mataifa Waanzisha Kampeni ya Kimataifa ya Kukomesha Ndoa za Utotoni
Na Thalif Deen

UMOJA WA MATAIFA, Novemba 12 (IPS) - Umoja wa Mataifa umezindua kampeni ya kimataifa ya kukomesha ndoa za utotoni, jambo ambalo bado linaendelea katika baadhi ya jamii duniani. "Mikataba ya kimataifa inasema kuwa ndoa za utotoni ni ukiukwaji wa haki za binadamu kwasababu zinanyima watoto wa kike haki za kuamua ni lini wanataka kuolewa na wataolewa na nani," inasema ripoti mpya iliyotolewa Alhamisi na Shirika la Idadi ya Watu la Umoja wa Mataifa (UNFPA).

Uzinduzi huo pia ulikuwa sehemu ya siku ya kwanza ya Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa kike – Okt. 11 – kama ilivyoamuliwa na wajumbe 193 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwaka jana ili "kutambua haki za wanawake na kuonyesha changamoto za kipekee zinazokabili watoto wa kike duniani".

Zaidi ya wanawake milioni 67, wenye umri kati ya miaka 20 hadi 24 mwaka 2010, waliolewa wakiwa watoto wa kike. Nusu yao walikuwa barani Asia, moja ya tano barani Afrika, ulisema utafiti huo. Na katika muongo ujao, watoto wa kike milioni 14.2 chini ya miaka 18 wataolewa kila mwaka.

Kama hali ya sasa ikiendelea, idadi itaongezeka hadi kufikia wastani wa watoto wa kike milioni 15.1 kwa mwaka, kuanzia mwaka 2021 hadi mwaka 2030, kwa mujibu wa utafiti uliopewa jina la "Kuolewa Utotoni: Kukomesha Ndoa za Utotoni".

Mkurugenzi Mkuu wa UNFPA Dkt. Babatunde Osotimehin, ambaye anakosoa kwa kiasi kikubwa ndoa za utotoni, anasema ana nia ya kusaidia kukomesha ndoa za utotoni duniani kote.

"Hakuna sababu ya msingi ya kijamii, kitamaduni wala kidini ya kuwafanya watoto wa kike kuolewa wakiwa na umri mdogo na uharibifu ambao unajitokeza kwa watoto hawa wa kike," alisema. "Mtoto wa kike anapaswa kuwa na haki ya kuchagua anataka kuolewa na nani na wakati gani. Kutokana na wazazi wengi na wanajamii wanataka mafanikio makubwa kwa mabinti zao, ni lazima kufanya kazi pamoja kukomesha ndoa hizi".

"Ni njia pekee ambayo tunaweza kukomesha jambo ambalo linaweza kuwa janga la kibinadamu la ndoa ya utotoni," alisema.

Dkt. Osotimehin pia alisema kuwa ndoa za utotoni ni ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na zinawanyima watoto wa kike fursa za elimu, afya na matarajio yao ya baadaye.

"Ndoa za utotoni zinaweza kusababisha matatizo makubwa ya mimba na kuzaa mtoto – sababu kuu zinazosababisha vifo vya watoto wa kike kati ya miaka 15-19 katika nchi zinazoendelea," aliongeza.

Dkt. Osotimehin pia alielezea waziwazi wake juu ya mtoto wa kike anayesoma wa Pakistan mwenye umri wa miaka 14 ambaye alipigwa risasi kutokana na kufanya kampeni dhidi ya kutetea haki ya kupata elimu nchini mwake.

Kampeni ya kukomesha ndoa za utotoni inaungwa mkono kutoka mashirika kadhaa ya Umoja wa Mataifa, ikiwa ni pamoja na UN Women, shirika la kuhudumia watoto la UNICEF, na mashirika ya haki za binadamu ya kimataifa kama vile Girls Not Brides na Human Rights Watch.

Michelle Bachelet, mkurugenzi mkuu wa UN Women, aliiambia IPS kuwa UN Women inakaribisha ripoti ya UNFPA juu ya ndoa za watoto.

"Ripoti inapaswa kutoa wito kwa sote sisi kuwa tunahitaji hatua kuchukua hatua kali kukomesha ndoa za utotoni," alisema.

Alisema hakuna mtoto wa kike anayetakiwa kunyimwa haki yake ya kufaidi utoto wake, kupata elimu na afya, na kufikia matarajio yake.

"Hata hivyo leo hii zaidi ya watoto wa kike milioni 14 wananyimwa haki zao kila mwaka wanapoolewa wakiwa watoto. UN Women inatoa wito kwa serikali zote na watu wote kukomesha ndoa za utotoni na kulinda haki za watoto wa kike," alisema Bachelet.

Anju Malhotra, wa Kitengo cha Jinsia katika UNICEF, alisema Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike inaonyesha haja ya kuweka mahitaji ya haki za mtoto wa kike katikati mwa ajenda ya maendeleo.

"Umoja wa Mataifa na washirika wake wanakusanyika pamoja kuonyesha mafanikio makubwa yaliyopatikana kuonyesha changamoto zilizopo," alisema.

Katika taarifa zilizotolewa hivi karibuni, UNICEF ilisema kuwa India, moja ya nchi zenye ndoa nyingi za utotoni miongoni mwa watoto wa kike kabla hawajafikisha miaka 18, ndoa za utotoni zimepungua kitaifa na karibu katika majimbo yote kutoka asilimia 54 mwaka 1992-1993 hadi asilimia 43 mwaka 2007-2008, lakini kasi ya kupungua ni ndogo.

Ikilinganishwa na nchi kama Bangladesh, Burkina Faso, Djibouti, Ethiopia, India, Niger, Senegal na Somalia inaonyesha jinsi gani hatua za kisheria pamoja na kuungwa mkono na wanajamii, kunatoa njia zinazowezekana – hasa kwenda shule – na kuwezesha jamii kujadili na kufikia hitimisho, uamuzi wa pamoja na kukomesha ndoa za utotoni kunaleta matokeo mazuri, ilisema UNICEF.

Katika ripoti yake, Human Rights Watch ilisema imeweka kumbukumbu ya ukiukwaji dhidi ya haki za wasichana na wavulana walioingia katika ndoa kwenye nchi za Afghanistan, Bangladesh, India, Iraq, Kenya, Kyrgyzstan, Nepal, Papua New Guinea, Sudan Kusini, na Yemen.

Ushuhuda wa watoto waliohojiwa unaonyesha madhara makubwa ya ndoa za utotoni katika maumbile yao na kiakili, kielimu, na uwezo wa watoto wa kuishi bila ya haki zao kukiukwa.

Madhara ya ndoa za utotoni hayaishii tu wakati mtoto anapoolewa na kufikia utu uzima, lakini mara nyingi huwafuata katika maisha yao yote wakati wakikabiliwa na hali zao za kiafya kutokana na kupata mimba wakiwa watoto mno na mara nyingi kukosa kwao elimu na kukosa uhuru wa kiuchumi, unyanyasaji wa majumbani, na ubakaji wa kwenye ndoa.

Alipoulizwa ni haki au siyo haki kusema kuwa ndoa nyingi za utotoni zinajitokeza miongoni mwa nchi za Kiislam, Liesl Gerntholtz, mkurugenzi wa kitengo cha haki za wanawake kwenye shirika la Human Rights Watch, aliiambia IPS, "Siyo haki kusema hili, kwani ndoa za utotoni zinajitokeza katika jamii tofautitofauti, ikiwa ni pamoja na jamii za Kikristo."

Akitoa mifano michache, alisema, nchini Burkino Faso, asilimia 48 ya watoto wa kike kwa sasa kati ya umri wa miaka 20 na 24 waliolewa kabla ya kufikisha umri wa miaka 18; nchini Cameroon, takwimu zinaonyesha asilimia 36; katika Jamhuri ya Afrika ya Kati ni asilimia 61; na katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo asilimia ni 39.

"Hizi ni takwimu za UNICEF, hivyo zinaaminika sana," alisema.

Wakati huo huo, UNFPA ilitangaza kuwa itawekeza dola za nyongeza kiasi cha milioni 20 katika kipindi cha miaka mitano ijayo kufikia "watoto wa kike wanaonyanyaswa zaidi katika nchi 12 zenye kiwango cha juu zaidi cha ndoa za utotoni". Nchi hizo ni pamoja na Guatemala, India, Niger and Zambia.

"Uwekezaji huu utaruhusu UNFPA kutekeleza mipango ya kimpangilio zaidi na iliyounganishwa pamoja kuongeza msaada kwa watoto wa kike walioolewa na wasioolewa wenye umri kati ya miaka 10-18 ambao wako hatarini kuacha shule, kuolewa wakiwa watoto na kupata mimba za utotoni," alisema Dk. Osotimehin, mkurugenzi mkuu wa UNFPA.

Shirika la Ford Foundation lenye makao yake mjini New York lilitoa ahadi ya dola milioni 25 kama msaada wake wa kusaidia kukomesha ndoa za utotoni duniani kote. (END/2012)

 

 
 Latest News from Africa
News in RSS
XML error: The element 'html' is used but not declared in the DTD/Schema.
  Dernières Nouvelles
News in RSS
DEVELOPPEMENT: Nous devons penser autrement à la "sécurité"
AUSTRALIE: Le port de Newcastle bloqué par les Guerriers du changement climatique
IRAN: L’examen d’un document clé à l’AIEA suggère un coup d’Israël
PAKISTAN: Les Ahmadis confrontés à la mort ou à l’exil
ETATS-UNIS: Le budget de la défense peut accroître alors que le public est fatigué de la guerre
A lire également>>