Inter Press Service News Agency
Monday, June 18, 2018   10:43 GMT    
   Homepage
   World Service
   East Africa
   Southern Africa
   West Africa
   Central Africa
 
   Environment
   Health-HIV/AIDS
   Education
   Rights
   Politics
   Economics
   and Finance
   Development
   Energy
   Population
   Culture
 
   Radio Service
 
   Français
 
   About IPS
 
   ENGLISH
   ESPAÑOL
   FRANÇAIS
   ARABIC
   DEUTSCH
   ITALIANO
   NEDERLANDS
   PORTUGUÊS
   SUOMI
   SVENSKA
   SWAHILI
   TÜRKÇE
PrintSend to a friend
Readers Opinions


Mfalme Nchini Swaziland Anakabiliwa Na Nguvu ya Umma Mwaka 2012
Na Mantoe Phakathi

MBABANE, Novemba 12 (IPS) - Mfalme wa Swaziland Mswati III anakabiliwa na shinikizo kubwa kufuatia mgogoro wa kikatiba ambao umesababisha baraza lake la mawaziri kukataa kujiuzulu baada ya Bunge kupitisha kura ya kutokuwa na imani na baraza hilo.

Wachambuzi wa kisiasa wanahisi hili limeonyesha kukosekana kwa demokrasia katika mfumo mzima wa serikali ya Swaziland na kuwa imemweka Mswati katika hali ya hatari ambapo inabidi kuchagua kati ya matakwa ya watu na ya wale ambao aliwaweka madarakani.

"Hatua ya waziri mkuu kuweka wazi kuwa serikali ina madaraka na kuwa nguvu ya kikatiba ya maneno au ya kimaandishi haina thamani," mchambuzi wa kisiasa Dkt. Sikelela Dlamini aliiambia IPS, akimaanisha Waziri Mkuu Barnabas Sibusiso Dlamini (hawana uhusiano) kukataa kuondoka madarakani.

Bunge la nchini humo, liliondosha madarakani baraza la mawaziri, ambalo ndicho chombo cha juu cha serikali, ambalo linahusu pia waziri mkuu na mawaziri wengine, siku ya Oktoba 3 kufuatia uamuzi wa Mahakama ya Usuluhishi ya Kimataifa (ICA) kulazimu Shirika la Posta na Simu la Swaziland (SPTC) linalomilikiwa na serikali kufunga huduma zake zote za simu za mokononi baada ya shirika la simu za mikononi la MTN nchini Swaziland kulalamikia kukosekana kwa uwanja sawa wa kibiashara. Tangu kufungiwa huko, SPTC imebaki na huduma yake ya simu za mezani tu.

Mswati anamiliki asilimia 10 ya hisa katika shirika la MTN wakati Waziri Mkuu Dlamini ana hisa katika shirika la Swaziland Empowerment Limited, ambalo linamiliki asilimia 19 ya hisa katika MTN.

Hata hivyo, baadhi ya wataalam wa sheria wamesema kuwa uamuzi wa ICA haukuwa unafunga kisheria kwasababu siyo amri iliyotolewa na mahakama za nchini, pamoja na kuwa serikali ilisisitiza kuwa inafungwa na uamuzi huo.

Waziri Mkuu Dlamini alisema masaa machache tu baada ya kura ya kukosa imani na baraza la mawaziri kuwa asingeweza kujiuluzu.

"Serikali ya Kifalme inaamini kuwa hoja iliyopitishwa na Bunge siyo sahihi kwani inataka kushinikiza baraza la mawaziri kukiuka amri za mahakama," Dlamini alisema, akiwa na maana uamuzi wa ICA.

Wakati mahakama inasema wazi kuwa baraza la mawaziri linapaswa kujiuzulu siku tatu baada ya kura ya kukosa imani nalo, msemaji wa serikali Percy Simelane aliiambia IPS kuwa tawi la utekelezaji wa shughuli za serikali bado linasubiri uamuzi wa Mfalme. Oktoba 9, aliwaambia waandishi wa habari kuwa waziri mkuu asingejiuzulu.

Swaziland ni nchi ya kifalme na Mswati anateua baraza la mawaziri na maseneta 20 kati ya 30 katika bunge la kifalme, huku maseneta wengine wakiteuliwa na Bara la Bunge.

Na wakati vyama vya siasa haviruhusiwi kufanya kampeni tangu mwaka 1973, wananchi wanaweza kuchaguliwa kuwa wabunge wa Baraza Kuu la Bunge chini ya Tinkhundla ambao ni mfumo wa majimbo. Kura ya kukosa imani na baraza la mawaziri imeonekana kama kura ya watu.

Mkurugenzi wa Uratibu wa Baraza la Mashirika Yasiyokuwa ya Kiserikali Emmanuel Ndlangamandla alisema kuwa uamuzi wa Baraza Kuu la Bunge unaonyesha matakwa ya watu na Mswati anatarajiwa kupitisha azimio hilo kama anazingatia utawala wa sheria na demorkasia.

"Hatuwezi kuwa na hali ambapo tuna mamlaka kwa upande mmoja na watu kwa upande mwingine. Katika hali kama hii, ni wazi kuwa watu hawaitaki serikali," alisema Ndlangamandla.

Chanzo cha habari cha kuaminika kiliiambia IPS kuwa mfalme mwenye umri wa miaka 44 anakataa kuonana na Spika wa Bunge kuzungumzia suala hilo na hayupo tayari kuchukua hatua yoyote juu ya kura ya kukosa imani na baraza la mawaziri kwasababu alikasirishwa mno na azimio la Bunge.

Katiba inampatia Mswati mamlaka ya kuvunja baraza la mawaziri baada ya kupigiwa kura ya kukosa imani. Spika wa Bunge, Prince Guduza, ambaye ni kaka wa kambo wa Mswati, alisema bado anatafuta jinsi ya kuzungumza na Mfalme juu ya suala hilo.

"Hadi sasa Mfalme hajasema jambo lolote," alisema Simelane. "Hivyo mambo yanaendelea kama kawaida."

Hata hivyo, Chama cha Wanasheria Swaziland kilisema katika taarifa yake ya Oktoba 12 kuwa kura ya kukosa imani itakuwa halali hadi mahakama zitakaposema vinginevyo. "Ni maoni yetu kuwa suala hili lilipaswa kupelekwa mahakamani kama suala la haraka," ilisema taarifa.

Wakati huo huo, Bunge limeamua kugomea baraza la mawaziri, jambo lenye maana kuwa mijadala na upitishaji wa miswada bungeni imesitizwa.

Lakini sheria ipo upande mwingine wa watu, alisema mwanasheria wa katiba Thulani Maseko, ambaye alisema kuwa hata Mswati hayupo juu ya katiba. Aliongeza kuwa hakushangazwa na tukio hilo hasa kutokana na kuwa mamlaka haifuati utawala wa sheria na haki za binadamu.

"Sheria imekuwa ikipuuzwa, ikikiukwa mara nyingi," Maseko aliiambia IPS.

Rais wa Shirikisho la Jumuiya ya Wafanyabiashara Swaziland Henry Tum du Pont aliiambia IPS kuwa gharama za huduma za mawasiliano nchini Swaziland zilikuwa za juu zaidi katika nchi za kidemokrasia Kusini mwa Afrika kutokana na kuwa na mfumo hodhi wa simu za mkononi na kumkosoa zaidi waziri mkuu kutokana na kulichukulia jambo hilo kwa maslahi binafsi.

"Kashfa ya SPTC ni moja ya maamuzi mengi ya kulinda maslahi binafsi yanayotolewa na baraza la mawaziri, ambalo kwa kiasi kikubwa linadhoofisha heshima ya biashara nchini humo," alisema Du Pont.

Msuguano kati ya baraza la mawaziri na Bunge unaimarisha sauti ya maendeleo katika wito wao wa kutaka demokrasia. Tangu mwaka 2008, vyama vya wafanyakazi vimetoa wito wa kuwepo kwa demokrasia ya vyama vingi kupitia maandamano ya wafanyakazi ambayo yamekabiliwa na ukandamizaji mkubwa wa vyombo vya usalama.

Maseko alisema kuwa msuguano huo kati ya pande mbili za serikali unaonyesha kuwa "hatimaye kuku amefikishwa nyumbani kwa ajili ya kuchomwa moto." (END/2012)

 

 
 Latest News from Africa
News in RSS
XML error: The element 'html' is used but not declared in the DTD/Schema.
  Dernières Nouvelles
News in RSS
DEVELOPPEMENT: Nous devons penser autrement à la "sécurité"
AUSTRALIE: Le port de Newcastle bloqué par les Guerriers du changement climatique
IRAN: L’examen d’un document clé à l’AIEA suggère un coup d’Israël
PAKISTAN: Les Ahmadis confrontés à la mort ou à l’exil
ETATS-UNIS: Le budget de la défense peut accroître alors que le public est fatigué de la guerre
A lire également>>