Inter Press Service News Agency
Tuesday, June 19, 2018   19:14 GMT    
   Homepage
   World Service
   East Africa
   Southern Africa
   West Africa
   Central Africa
 
   Environment
   Health-HIV/AIDS
   Education
   Rights
   Politics
   Economics
   and Finance
   Development
   Energy
   Population
   Culture
 
   Radio Service
 
   Français
 
   About IPS
 
   ENGLISH
   ESPAÑOL
   FRANÇAIS
   ARABIC
   DEUTSCH
   ITALIANO
   NEDERLANDS
   PORTUGUÊS
   SUOMI
   SVENSKA
   SWAHILI
   TÜRKÇE
PrintSend to a friend
Readers Opinions


Kuwapatia Wanawake Ardhi ni Kuwapatia Maisha ya Baadaye
Na Ngala Killian Chimtom

YAOUNDE, Oktoba 30 (IPS) - Kwa taabu Clarisse Kimbi anaweza kuendesha maisha kwa kutegemea kipande kidogo cha ardhi katika kijiji cha Kom katika Mkoa wa Kaskazini Magharibi mwa Cameroon. Leo hii, akiwa mama wa watoto sita anapata shida kulisha watoto wake na yeye mwenyewe. Lakini miaka mitano iliyopita, mume wake na watoto wake walikuwa wakionekana watu wenye uwezo.

Mwaka 2007, akiwa analima ardhi yenye ukubwa wa hekta tano, Kimbi aliweza kulisha familia yake bila shida, na bado angepata chakula cha ziada kwa ajili ya kukiuza. Katika nchi ambapo asilimia 40 ya wakazi wanaishi chini ya mstari wa umaskini, familia yake ilionekana kuwa miongoni mwa familia tajiri.

Lakini mambo yalibadilika wakati mume wake alipofariki dunia miaka mitano iliyopita. Karibu kila kitu kilichukuliwa kutoka kwake na watoto wake.

"Siku moja tu baada ya mazishi ya mume wangu, shemeji zangu walipora hekta tano za ardhi ya mume wangu ambazo nimekuwa nikilima kwa miaka 27," aliiambia IPS. Mila za eneo hilo zinawapatia wanaume haki ya kurithi ardhi.

"Mambo sasa yamekuwa mabaya mno kiasi kwamba ilibidi kuwaachisha baadhi ya watoto shule," alisema.

Wawili kati ya watoto wake hao hawaendi shule ya sekondari, na wengine watatu wanakwenda kwa shida mno shule ya msingi. Pamoja na tangazo la Rais Paul Biya la kutoa elimu ya msingi bure nchini Cameroon mwaka 2004, lakini wazazi bado wanatakiwa kulipia ada kusaidia shule zenye miundombinu duni kufanya kazi.

Tatizo la Kimbi siyo la pekee. Takwimu kutoka Taasisi ya Takwimu ya Taifa ya mwaka 2010 inaonyesha kuwa wanawake ni asilimia 52 ya wakazi wote wa Cameroon milioni 20.

Na pamoja na kuwa wanawake wanazalisha asilimia 80 ya mahitaji ya chakula nchini Cameroon kwa mujibu wa Wizara ya Kilimo na Maendeleo Vijijini, wanamiliki asilimia mbili tu ya ardhi, kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2011 za Mtandao wa Usawa wa Jinsia Cameroon.

"Kama tunaongelea kuhusu jamii ya usawa na ya haki, tunapaswa wanawake kudhibiti kwa uchache asilimia 35 ya ardhi," Judith Awondo, mratibu wa mtandao huo, asasi isiyokuwa ya kiserikali ambayo inafanya kazi kuwapatia uwezo wanawake, aliiambia IPS.

Pamoja na kwamba Sheria ya Umilikaji wa Ardhi ya Mwaka 1974 nchini Cameroon inahakikishia usawa wa kumiliki ardhi raia wote, sheria za kimila na desturi zinabagua wanawake dhidi ya haki zilizopo katika sheria. Hii imesababisha matatizo katika uchumi wa wanawake.

"Kukosekana kwa uwezo kwa wanawake kumiliki ardhi na kudhibiti njia za kumiliki rasilimali kunawaweka katika nafasi duni katika suala zima la uzalishaji wa kilimo na ukuaji wa kiuchumi, usalama wa chakula, kipato cha familia na ushiriki sawa katika utawala," Fon Nsoh, mratibu wa NGO ya nchini humo ya Vuguvugu la Haki ya Chakula Cameroon, aliiambia IPS.

Kwa mujibu wa utafiti wa kaya wa mwaka 2007, asilimia 52 ya watu wanaoishi katika kaya maskini nchini Cameroon ni wanawake.

Matatizo ya umiliki wa ardhi kwa wanawake na wanajamii yamezidishwa zaidi na upokonyaji wa ardhi unaoongozwa na makampuni ya kimataifa na jamii tajiri, kwa mujibu wa Nsoh. Alitoa mfano wa "Herakles Farms" katika Mkoa wa Kusini Magharibi mwa Cameroon kama suala "gumu zaidi na linalopingwa zaidi."

Novemba 7, 2011,Kitengo cha Mahakama Kuu cha Kupe-Muanenguba katika Mkoa wa Kusini Magharibi kilitoa amri kuwa mradi huo usimamishwe. Lakini Nsoh alielezea wasiwasi wake kuwa kampuni hiyo ilikuwa inaendelea kuandaa shamba la miwese la hekta 73,000 na kuwa na kibali cha umiliki cha miaka 99 kinachotokana na mazingira ya kashfa.

Mashirika yenye makao yake nchini Marekani ya Taasisi ya Oakland na Greenpeace, shirika la mazingira la kimataifa, yalitoa ripoti inayopendekeza kuwa mradi huo uliopo katika eneo ambalo linatajwa kuwa na utajiri wa baoanuwai kati ya maeneo makuu ya hifadhi, unaweza kuathiri vibaya watu wapatao 45,000.

Mashirika ya mazingira yanatuhumu kampuni ya kilimo ya Herakles Farms yenye makao yake mjini New York kutokana na kuendelea na mipango yake pamoja na pingamizi mbili za mahakama na kukosekana kwa kibali cha serikali, na huku kukiwa na upinzani mkubwa kutoka kwa jamii.

"Kuna mamia ya watu huko ambao wanaweza kupoteza mashamba yao, hasa wanawake ambao hawakuwa sehenu ya mazungumzo," Nsoh aliiambia IPS.

Kwa sasa anafanya kazi pamoja na NGOs nyingine na mashirika ya kiraia kuwezesha mageuzi ya Sheria ya Umilikaji wa Ardhi ya mwaka 1974 ambayo inaongoza masuala ya ardhi nchini Cameroon.

"Sheria ya Ardhi ya Mwaka 1974 imepitwa na wakati. Imepitishwa kama miaka 38 iliyopita na haiendani tena na siku za sasa hivi na uhalisia wa siku hizi," Nsoh alisema.

Kifungu cha 12 cha Sheria ya Ardhi ya mwaka 1974 kinasema "serikali itakuwa inadhibiti ardhi yote. Katika uwezo huu itaingilia kati kuhakikisha matumizi sahihi ya ardhi au katika maslahi muhimu, ulinzi au sera za uchumi wa taifa."

Nsoh anasema kuwa kifungu hicho kinawaondoa wanajamii katika mijadala inayohusu ardhi, huku akitoa mfano wa kesi kadhaa ambapo serikali imechukua ardhi kwa ajili ya uwekezaji, bila hata kushauriana na wanajamii wanaoishi katika ardhi hiyo.

Pamoja na NGOs nyingine na mashirika ya kiraia, vuguvugu la Nsoh linashinikiza kuwepo kwa sheria shirikishi zaidi, akisema kuwa sheria inapaswa kutokusema tu kuwa wanajamii washirikishwe katika mazungurumzo ya ardhi, lakini pia sehemu kubwa iwahusu wanawake na makundi yaliyopo pembezoni linapokuja suala zima la ardhi, ili angalau waweze kuwa na udhibiti nayo.

Tangu mwaka jana makundi haya yamekuwa yakifanya kazi ya kuja na muswada wa haki ya ardhi ili iweze kuwasaidia kuondokana na vikwazo vya upatikanaji wa ardhi. Sheria inayopendekezwa inataka kuhakikisha kuwa kuna sheria juu ya mila za kibaguzi ambazo zinazuia wanawake wasipate ardhi.

"Hatimiliki lazima zitambue umiliki wa mwanaume na mwanamke na majina mawili ya mume na mke yaandikwe kwenye hati hiyo ili kuondokana na mfumo dume wa urtihi wa ardhi ambao umeenea sana nchini Cameroon," Nsoh alisema. Aliongeza kuwa mahitaji kama hayo yangewezesha kuwa vigumu kwa wanawake kama Kimbi kunyimwa ardhi yao na wanafamilia wengine kama mmoja wa wanandoa wao akifariki.

Mbali na wito wa kutaka wanawake kuingizwa katika kamati zote zinazohusika na masuala ya ardhi, mashirika ya kiraia katika taifa hili la Afrika ya Kati yanashinikiza pia kurahisishwa kwa taratibu ndefu na zinazochosha za kupata hatimiliki, na gharama za kupata hati hizo kupunguzwa kufikia kiwango ambacho wanawake wanaweza kumudu, hasa wanawake maskini ambao wamekuwa maskini kutokana na sera zilizopo.

"Tunahitaji kupitia upya sheria hii na kuipatia mwelekeo wa kijinsia," Nsoh alisema.

Alisema pamoja na kwamba serikali bado haijajibu madai ya mashirika ya kiraia, ana matumaini kuwa hatimaye itakuja kujibu. Wakati wa maonesho ya wakulima na wafugaji ya mwaka 2011 yaliyoandaliwa huko Ebolowa Mkoa wa Kusini mwa Cameroon, Rais Biya alielezea haja ya kupitia upya sheria hiyo.

Inaweza kuchukua muda mrefu, lakini kutokana na kuwa natoka katika mamlaka ya juu kabisa ya kisiasa nchini, hakuna wasiwasi kuwa itafanyika," Nsoh alisema. Hata hivyo, bado amechanganyikiwa juu ya kasi ndogo ambayo matukio hayo yanafanyiwa kazi, kwasababu hii ina maana kuwa wanawake wengi wa Cameroon wanaendelea kuteseka na kunyimwa haki. (END/2012)

 

 
 Latest News from Africa
News in RSS
XML error: The element 'html' is used but not declared in the DTD/Schema.
  Dernières Nouvelles
News in RSS
DEVELOPPEMENT: Nous devons penser autrement à la "sécurité"
AUSTRALIE: Le port de Newcastle bloqué par les Guerriers du changement climatique
IRAN: L’examen d’un document clé à l’AIEA suggère un coup d’Israël
PAKISTAN: Les Ahmadis confrontés à la mort ou à l’exil
ETATS-UNIS: Le budget de la défense peut accroître alors que le public est fatigué de la guerre
A lire également>>