Inter Press Service News Agency
Thursday, June 21, 2018   09:54 GMT    
   Homepage
   World Service
   East Africa
   Southern Africa
   West Africa
   Central Africa
 
   Environment
   Health-HIV/AIDS
   Education
   Rights
   Politics
   Economics
   and Finance
   Development
   Energy
   Population
   Culture
 
   Radio Service
 
   Français
 
   About IPS
 
   ENGLISH
   ESPAÑOL
   FRANÇAIS
   ARABIC
   DEUTSCH
   ITALIANO
   NEDERLANDS
   PORTUGUÊS
   SUOMI
   SVENSKA
   SWAHILI
   TÜRKÇE
PrintSend to a friend
Readers Opinions


Mradi wa Kijiji Wasaidia Wakulima wa Vijijini Senegeal
Na Koffigan E. Adigbli

POTOU, Senegal, Oktoba 30 (IPS) - Ongezeko la mavuno kaskazini mwa Senegal katika jamii ya Léona kunatoa ushahidi wa faida za msaada katika kilimo. Lakini wakati mavuno yao yakiongezeka, wakulima wanatoa wito wa kuwepo kwa sera za kulinda masoko ya mazao yao. Tangu mwaka 2008, kijiji cha Potou kimekuwa eneo la jitihada za kisekta za kupambana na umaskini, moja ya vijiji 12 vya "Milenia" kilichopo katika eneo linalokumbwa na njaa ya mara kwa mara katika nchi kumi barani Afrika.

Kila eneo limechaguliwa kuwakilisha ukanda tofauti wa kilimo na kiikolojia katika Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, kuonyesha ni jinsi gani mchanganyiko wa maarifa ya jadi na mifumo ya kisayansi inaweza kuboresha kufikia Lengo la Maendeleo ya Milenia la kupunguza umaskini uliokithiri na njaa kwa nusu – hata katika mazingira magumu kabisa. (Malengo ya MDGs ni malengo kadhaa ya kupambana na umaskini yaliyokubaliwa na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa mwaka 2000.)

Mradi ulianzishwa na mwanauchumi Jeffrey Sachs, mkurugenzi wa Earth Institute, na umepata kuungwa mkono kutoka vyanzo mbalimbali ikiwa ni pamoja na Mashirika ya Umoja wa Mataifa, makampuni ya kimataifa ya kemikali na kilimo, watu mmoja mmoja na serikali za ndani na za wafadhili wa kigeni.

Mradi wa Kijiji cha Milenia una malengo ya kupunguza umaskini uliokithiri kwa nusu, kuwapatia wakulima mbegu zenye mavuno makubwa, mbolea na vifaa vya umwagiliaji. Lakini mradi haujaangalia tu katika kilimo.

"Watu katika jamii yetu sasa wanapata maji safi na nishati ya jua ambayo siyo tu kwamba inatoa mwanga katika nyumba zetu lakini pia inasadia katika umwagiliaji wa kati ya hekta 800 kati ya 1,000 zinazotumika kwa kilimo cha vitunguu katika kanda," alisema Serigne Abdou Boye, makamu wa rais wa Chama cha Wakulima wa Bustani cha Senegal.

Mradi pia umeongeza vituo vinne vipya vya afya katika Léona, ambapo kati ya hivyo wakazi 31,000 katika jamii wanaweza kupata huduma za afya za bure. Madarasa mapya sitini yanaandaliwa kuejngwa pia, ili kuondokana na majengo ya muda mfupi ambayo wanafunzi wengi wa wilaya hiyo huyatumia kwa ajili ya masomo.

Wakulima wa Léona wanapanda kila aina ya mazao, ikiwa ni pamoja na nyanya, pilipili na karoti, lakini El Hadj Mamadou Bâ, rais wa jamii hii ya kijijini, alisema kuwa wakulima wa vitunguu wamekuwa wanafaidika zaidi na mradi wa Kijiji cha Milenia.

"Mwaka jana, nilivuna chini ya tani 20 za vitunguu kutoka katika hekta moja. Mwaka huu, nimepata hekta mbili za umwagiliaji ambazo nimezipanda vitunguu, na hii inatokana na msaada wa mradi wa mbegu za vitunguu, nadhani nitaweza kupata tani 80," aliiambia IPS.

Mkulima mwingine wa vitunguu, Idrissa Diallo, aliiambia IPS kuwa kwa kutumia mbegu bora, umwagiliaji na mbolea za asili kutokana na kinyesi cha ng’ombe, zaidi ya tani 60,000 za vitunguu zilivunwa wakati wa msimu wa kupanda wa 2012-2011, kiwango cha juu zaidi kuliko tani 45,000 zilizozalishwa mwaka 2009-2010.

"Kabla ya mradi, tulihitaji wafanyakazi wengi kumwagilia mashamba, lakini mazao yetu hayakuongezeka. Tulivuna chini ya tani 20 kwa hekta moja, lakini kutokana na mradi, mara nyingine tumeweza kupata hadi tani 70 kwa hekta," alisema Idrissa Diallo, mkulima wa vitunguu wa Potou.

Wakati wa ziara katikati mwa mwezi Julai, Bouri Sanhouidi, mwakilishi mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa mjini Dakar, alisema mfumo mpya wa umwagiliaji unapatia jamii rasilimali kupanda mbegu. Alitoa wito kwa mashirika ya Umoja wa Mataifa kusaidia mradi huo.

Wakati wa msimu wa kupanda wa kuanzia Aprili hadi Novemba kila mwaka, wakazi wa Potou – kijiji chenye jumla ya wakazi 3,000 kati ya wakazi 31,000 wa Léona, kwa mujibu wa sensa ya mwisho kufanyika – kuna ongezeko la wafanyakazi wa mashambani wanaohama kutoka nchi za jirani.

Ahmadou Konté, kutoka Guinea, aliiambia IPS amekuja kufanya kazi hapa tangu mwaka 2008. Alisema anarejea nyumbani kila mwisho mwa mwaka akiwa ameingiza dola zipatazo 360.

Bâ aliongeza kuwa vyama vya ushirika vinavyofanya kazi katika Léona vimejenga ajira kwa vijana 102 ambao walirejeshwa kutoka Hispania kama wahamiaji haramu mwaka 2005.

Mafanikio ya wanajamii hao yamevutia watu wengine kutoka mahali pangine kuhamia katika eneo hilo, lakini bado kuna changamoto za kushughulikiwa.

Wakulima wanalalamika kuwa wametengwa na barabara duni za ukanda huo. Pia wanasema kuwa mbolea na mbegu zilitolewa kwa kuchelewa mno na kwamba gharama za pembejeo hizo ni kubwa mno.

"Ndiyo, tumekuwa tukipewa mbegu na mbolea kutoka katika mradi, lakini bei ya pembejeo hizi ni ya juu mno. Tungependa kupata msaada wa nyongeza kutoka serikalini. Gramu mia tano za mbegu zinagharimu faranga za CFA 21,000 (sawa na dola 42), na mfuko mmoja wa mbolea wa kilo 50 unagharimu faranga 12,000 (dola 24). Bei hiyo ni ya juu mno," Yoro Ba aliiambia IPS.

Pia kuna kutokuridhika na bei za vitunguu, Fatoumata Dia Sy, mkurugenzi wa kanda wa Huduma ya Taifa ya Ushauri Vijijini huko Louga, kaskazini mwa nchi, aliiambia IPS.

"Bei ya vitunguu imewekwa katika makubaliano kati ya serikali na wakulima," alisema. Wakulima wanapata sawa na senti 24 za dola za Kimarekani kwa kila kilo kutoka kwa wafanyabiashara ambao wanapewa mamlaka ya kuuza vitunguu kwa senti 33 kwa kilo kwa wachuuzi ambao wataweza kuviuza kwa walaji kwa senti 50 kwa kila kilo.

Mkulima Moussa Sow pia alipendekeza kuondolewa kwa ushuru wa kuingiza vitunguu nchini ambako serikali ilianzisha mwezi Februari hadi mwishoni mwa Agosti. "Kuruhusu tena kuingizwa kwa vitunguu ni changamoto. Kunahatarisha kuua uzalishaji wetu katika eneo hili," alisema, akihofia kushuka kwa mauzo ya vitunguu vya ndani kama soko litajaa vitunguu kutoka nje.

"Tumechukua mikopo yetu ya benki, na sasa hatuwezi tena kuuza mazao yetu kutokana na kukosa soko," Sow alisema.

Rais wa Léona Mamadou Bâ alitoa wito wa kupigwa marufuku uingizwaji wa vitunguu kwa kipindi cha miaka mitatu.

Waziri mkuu wa Senegal, Abdoul Mbaye, litembelea mradi huo Julai, na kuupongeza kama "mfano mzuri wa maendeleo." Alisisitiza haja ya serikali kufanya kazi ili kuufanya mradi huo kuwa endelevu na kuutekeleza katika maeneo mengine ya vijijini. Kuangaliwa kwa madai ya wakulima juu ya suala la soko ingekuwa eneo zuri kuanzia. (END/2012)

 

 
 Latest News from Africa
News in RSS
XML error: The element 'html' is used but not declared in the DTD/Schema.
  Dernières Nouvelles
News in RSS
DEVELOPPEMENT: Nous devons penser autrement à la "sécurité"
AUSTRALIE: Le port de Newcastle bloqué par les Guerriers du changement climatique
IRAN: L’examen d’un document clé à l’AIEA suggère un coup d’Israël
PAKISTAN: Les Ahmadis confrontés à la mort ou à l’exil
ETATS-UNIS: Le budget de la défense peut accroître alors que le public est fatigué de la guerre
A lire également>>