Inter Press Service News Agency
Saturday, June 23, 2018   07:16 GMT    
   Homepage
   World Service
   East Africa
   Southern Africa
   West Africa
   Central Africa
 
   Environment
   Health-HIV/AIDS
   Education
   Rights
   Politics
   Economics
   and Finance
   Development
   Energy
   Population
   Culture
 
   Radio Service
 
   Français
 
   About IPS
 
   ENGLISH
   ESPAÑOL
   FRANÇAIS
   ARABIC
   DEUTSCH
   ITALIANO
   NEDERLANDS
   PORTUGUÊS
   SUOMI
   SVENSKA
   SWAHILI
   TÜRKÇE
PrintSend to a friend
Readers Opinions

Maswali na Majibu
Kukabiliana na Majanga Kunaanzia na Wanawake katika Ngazi ya Chini ya Jamii
Na Julia Kallas

UMOJA WA MATAIFA, Oktoba 30 (IPS) - Julia Kallas anamhoji JOSEPHINE CASTILLO, HAYDEE RODRÍGUEZ na VIOLET SHIVUTSE Wanawake na wasichana wanaweza kuwa wakala wa mabadiliko wenye nguvu, lakini wanaathiriwa zaidi na majanga kutokana na majukumu yao katika jamii, kubaguliwa na umaskini.

Siku ya Kimataifa ya Kupunguza Majanga mwaka huu ilikuwa na kaulimbiu ‘’Wanawake na Wasichana – Nguvu ya Kukabiliana na Majanga Isiyoonekana’’.

Mwandishi wa IPS Julia Kallas alikaa chini na wanawake watatu – Josephine Castillo, kiongozi wa jamii katika ngazi ya chini na mwandalizi wa DAMPA mjini Manila, Ufilipino; Haydee Rodríguez, rais wa Umoja wa Vyama vya Ushirika vya Wanawake, Las Brumas, huko Jinotega, Nicaragua; na Violet Shivutse, kiongozi na mwanzilishi wa Jamii ya Wafanyakazi wa Afya ya Shibuye nchini Kenya – kuzungumzia kuhusu umuhimu wa watoto wa kike na wanawake kama watekelezaji na viongozi wa kukabiliana na majanga.

Swali: Nyote mnatokea katika mazingira tofauti. Mnaweza kuniambia kuhusu changamoto kubwa zinazowakabili katika kujenga njia za kukabiliana na majanga katika jamii mnamoishi?

JOSEPHINE CASTILLO: Mimi ni mmoja wa wakurugenzi wa bodi wa chama cha jumuiya. Ni chama cha wamiliki wa majengo, tuna wanachama 421 na kila mmoja anamiliki ardhi tangu mwaka 1995. Hii inatokana na mpango wenye mafanikio ambao chama chetu kimeufanya kwa kushirikiana na serikali, ambayo ilipatia wanawake mikopo ya nyumba kununua majengo.

Tuna programu ambazo zinaleta wanajumuiya yetu pamoja kama kukitokea majanga. Tunafundisha timu ya kukabiliana na majanga punde yanapotokea kwa kushirikiana na serikali yetu ya mitaa na mipango yetu ya kukabiliana na majanga inashirikiana pia na Tume ya Huairou na shirika la GROOTS International.

Watu walioathirika na mafuriko mwezi Agosti mjini Manila waliletwa katika maeneo yetu ya kuwahifadhi, ambayo yaliokoa wanafamilia walioathirika na mafuriko na tetemeko la ardhi. Majanga ya asili yanajitokeza mara kwa mara kutokana na mabadiliko ya tabia nchi na hivyo kuhitaji njia za kukabiliana na mabadiliko haya, kuwa na mbinu za kuzuia majanga na mbinu za kuhimili majanga.

HAYDEE RODRIGUEZ: Mimi ni rais wa Umoja wa Vyama vya Ushirika vya Wanawake, "Las Brumas" huko Jinotega, Nicaragua, na tunajenga vyama vya ushirika vya wanawake katika ngazi ya chini 20 vyenye jumla ya wanawake 1,200 na wengine 960 ambao siyo wanachama wa moja kwa moja.

Tunakabiliwa na matatizo mengi katika jamii yetu ikiwa ni pamoja na mabadiliko ya tabia nchi na umiliki wa ardhi. Hivyo kupitia kazi yetu ya kukabiliana na majanga tumejenga mpango wa kulima chakula na mazao ya dawa katika nyumba zetu katika jamii ikiwa ni pamoja na mpango wa kujenga mjadala bora kati ya jamii na serikali.

Pia tumefanikiwa katika kuingiza wanawake wa ngazi ya chini kushiriki katika vyama. Uchaguzi ujao, ambao utafanyika Novemba 4, utashirikisha wanawake 14 kutoka ndani ya vyama.

VIOLET SHIVUTSE: Nilipokuwa nafanya kazi katika ofisi ambayo ilisajili wakulima, nilikutana na wanawake wengi mno wenye mimba ambao walipata shida ya kujifungua. Wengi wao walifariki wakati wa kujifungua, wengine walikuwa na matatizo ya kujifungua wakati watoto wao walipofariki au wanawake walikuwa wagonjwa kwa muda mrefu baada ya kujifungua.

Tatizo kubwa ni kuwasaidia na kuhakikisha kuwa wanawake hawa waliweza kufika hospitalini, kwasababu ya umbali na gharama kubwa za huduma. Halafu nikaanza kufikiri kuhusu jinsi gani ya kusaidia wanawake hawa ambao ni muhimu mno katika jamii. Hivyo ndivyo nilipoanza kushiriki katika kazi za jamii na masuala ya afya za wanawake.

Fedha za kupambana na VVU/UKIMWI, usalama wa chakula, vipindi vya ukame na mafuriko ni matatizo makubwa katika jamii yangu. Maji, vyoo na usafi pia ni matatizo kwa watoto wa shule. Wakati nilikubaliana kuwa matatizo haya yalikuwa yakiongezeka, nilichukua wanawake katika ngazi ya chini ya jamii kufanya kazi nao kuanzisha jamii yetu. Tulianza shirika linalojikita katika jamii lijulikanalo kama Wafanyakazi wa Afya wa Jumuiya ya Shibuye, ambalo kwa sasa lina wanawake kutoka ngazi ya chini ya jamii 2,036 nchini Kenya ambao wanafanyia kazi masuala haya.

Swali:Ni kwa nini ni muhimu kuelekeza nguvu kwa wanawake na watoto wa kike katika muktadha mzima wa kupunguza majanga? JC: Kwasababu wanawake na watoto wa kike ndiyo waathirika wakuu wa majanga yanapotokea. Wanahitaji kujiandaa na kupatiwa mafunzo. Hatutaki kusema kuwa sisi ni dhaifu, lakini ni kweli kuwa ni dhaifu. Tunapozungumzia kukabiliana na majanga hatuzungunzii tu kuhusu majanga ya asili. Kukosekana kwa elimu pia kuna maana janga. Wanawake na watoto wa kike hawawezi kupata ajira bila ya kuwa na elimu. Hii ndiyo sababu wanawake wanashiriki katika mikutano ya kimataifa, kuonyesha haja ya kupambana na haki zetu.

HR: Wanawake kufanya kazi ya kupambana na majanga ni muhimu kwasababu tunataka kufanyia kazi maisha yetu na maisha ya jamii zetu. Wanawake wanahitaji kufanya kazi ya kukabiliana na majanga kwasababu kama hatutatunza maji, kwa mfano, hakutakuwa na kilimo na kama hakuna uzalishaji, kutakuwa na njaa.

VS: Tuna imani kuwa kazi ya kukabiliana na majanga inaanza na mwanamke. Wao ndiyo wanaotunza jamii za vijijini kwasababu wanaume wanahamia mijini kutafuta ajira. Hivyo madhara ya majanga kwa wanawake na watoto wa kike ni kubwa. Tunahamasisha wanawake kufanya kazi katika makundi ili waweze kuelewa jinsi gani ya kujenga uwezo wa kukabiliana na majanga. Kukabiliana na majanga kuna maana kuwa na chakula katika majumba yao, kujenga hifadhi za vyakula, kubainisha rasilimali za asili na kuzilinda. Pia tuna imani kuwa ni muhimu kuwafundisha watoto wetu wa kila kazi za kukabiliana na majanga ili wakijakuwa watu wazima na mama watoto waweze kusaidia jamii zao.

Swali: Njia ya kujenga miradi yenye ufanisi ya kukabiliana na majanga inayoendeshwa na wanawake ikoje? JC: Ni muhimu kuwa na ushirikiano na serikali za mitaa, taasisi na mashirika duniani kote. Pia kuangalia mijadala ni muhimu sana. Mashirika yanatakiwa kuelekeza nguvu katika zaidi ya masuala zaidi ya moja, kwasababu ya kuelekeza nguvu katika suala moja na suala hilo likishatatuliwa huna suala jingine la kufanyia kazi. Programu zetu zilitokana na watu, siyo kutoka kwa wafadhili.

HR:Nina imani tunahitaji kuhamasisha wanawake kushiriki katika kutoa maamuzi na kushika nafasi za uongozi. Mashirika yanatakiwa kusaidia na kuhamasisha wanawake kuwa wabunifu kwa kuwapatia rasilimali .Pia wanawake katika ngazi za chini wanapaswa kufanya kazi zao na miradi na wanajamii ili kusaidia kufanya kazi za kukabiliana na majanga.

VS: Kwanza tunahitaji kuelimisha wanawake na watoto wa kile … kwasababu kama hawana elimu hawawezi kushiriki katika kazi za jamii. Pili ni kuwafanya wanawake kuwa na nguvu kiuchumi na kisiasa. Kuwapatia thamani zaidi na ubora katika kazi za mazingira (END/2012)

 

 
 Latest News from Africa
News in RSS
XML error: The element 'html' is used but not declared in the DTD/Schema.
  Dernières Nouvelles
News in RSS
DEVELOPPEMENT: Nous devons penser autrement à la "sécurité"
AUSTRALIE: Le port de Newcastle bloqué par les Guerriers du changement climatique
IRAN: L’examen d’un document clé à l’AIEA suggère un coup d’Israël
PAKISTAN: Les Ahmadis confrontés à la mort ou à l’exil
ETATS-UNIS: Le budget de la défense peut accroître alors que le public est fatigué de la guerre
A lire également>>