Inter Press Service News Agency
Monday, June 18, 2018   10:54 GMT    
   Homepage
   World Service
   East Africa
   Southern Africa
   West Africa
   Central Africa
 
   Environment
   Health-HIV/AIDS
   Education
   Rights
   Politics
   Economics
   and Finance
   Development
   Energy
   Population
   Culture
 
   Radio Service
 
   Français
 
   About IPS
 
   ENGLISH
   ESPAÑOL
   FRANÇAIS
   ARABIC
   DEUTSCH
   ITALIANO
   NEDERLANDS
   PORTUGUÊS
   SUOMI
   SVENSKA
   SWAHILI
   TÜRKÇE
PrintSend to a friend
Readers Opinions


Sheria Yashindwa Kulinda Watoto wa Malawi
Na Charity Chimungu Phiri

BLANTYRE, Oktoba 29 (IPS) - Patrick Martin, 14, na kaka yake Mayeso, 15, kwa sasa wako salama wakiwa nyumbani na ndugu zao katika kijiji cha Kasonya, Wilaya ya Phalombe kusini mwa Malawi, baada ya wao na watoto wengine 12 kuokolewa na kutokana na kutaka kusafirishwa na baba yao katika biashara ya usafirishaji haramu wa binadamu kwenda nchi jirani ya Msumbiji mwezi uliopita.

Kila msimu wa kilimo, watu kutoka Wilaya ya Phalombe wanapelekwa katika taifa hilo la kusini mwa Afrika la Msumbiji ili kuingizia familia zao pesa za kutosha kununulia baiskeli – ambayo inaonekana kuwa chombo cha anasa katika nchi ambayo asilimia 65 ya wakazi wake milioni 16 wanaishi chini ya mstari wa umaskini.

Habari ya watoto hawa ni moja ya matukio mengi ya kawaida nchini Malawi wakati huu, wakati takwimu za serikali zikionyesha kuwa kwa uchache watoto milioni 1.4 wanashiriki katika ajira mbaya za watoto na asilimia 20 kati yao wanasafirishwa ndani ya nchi na kimataifa kwa ajili ya sekta ya ngono na kazi nyingine haramu.

Lakini usalama wa baadaye wa wavulana hawa unabakia kutokueleweka, na wanaweza kulazimika kutumbukia tena katika ajira ya watoto, kwani sheria zilizopitwa na wakati nchini humo zina maana kuwa baba yao hatapata adhabu yoyote ile. Nchi hiyo haina sheria ya usafirishaji haramu wa watoto, na pamoja na kuwepo kwa kifungu kinachopinga usafirishaji wa watoto Kifungu cha 79 cha Sheria ya Kulinda Haki za Watoto, hakitekelezwi kiusahihi.

Baba yao, James Martin, 31, ataachiwa huru kutoka gereza la Mulanje baada ya kutumikia kifungo cha miezi 18. Yeye, pamoja na James Banda, 23; Daniel Thumpwa, 21; na Dickson Kambewa, 37, wamekutwa na hatia ya kutumikisha watoto wenye chini ya umri wa miaka 18 katika ajira.

Wameshitakiwa chini ya Sheria ya Ajira, na wala siyo katika suala zima la usafirishaji haramu wa watoto kwa mujibu wa Kifungu cha 79 cha Sheria ya Kulinda Haki za Watoto.

Sheria hii, ambayo ilianza kutumika Disemba 2011, inasema kuwa msafirishaji haramu wa watoto anapaswa kuhukumiwa kifungo cha juu jela cha maisha yake yote anapokutwa na hatia ya kusaririsha watoto wenye umri wa chini ya miaka 16.

Maxwell Matewere, mkurugenzi mkuu wa shirika lisilokuwa la kiserikali la "Eye of the Child", ambalo linajishughulisha zaidi kupanmbana na usafirishaji haramu wa watoto, aliiambia IPS kuwa sheria za nchi zinafanya kuwa vigumu kwa mashirika yasiyokuwa ya ksierikali na polisi kufanya kazi kikamilifu katika kupambana na vitendo hivyo.

"Tatizo sasa ni kwamba mahakimu hawatumii Sheria ya Kulinda Haki za Watoto kutoa hukumu hasa kutokana na kwamba siyo lazima na pia inategemeana na sababu kadhaa kama vile ngazi gani ya kusafirishwa ambayo mtoto aliokolewa na pia umri wake.

"Pia nchini Malawi hatuna sheria ya usafirishaji haramu wa binadamu hivyo wakati wahalifu wanapokamatwa na polisi na kufunguliwa mashitaka kwa sheria ya usafirishaji haramu wa binadamu mashitaka yanabadilishwa na mahakama kutokana na kuwa hakuna sheria," alisema.

"Mwanaume wa Zambia ambaye alikamatwa kwa kusafirisha watoto kwa njia haramu kutoka Dedza (katika Mkoa wa Kati mwa Malawi) kufanya kazi katika mashamba ya mahindi nchini Zambia, aliachiliwa huru baada ya kulipa faini," alisema.

Matewere aliongeza kuwa sheria ya sasa ya Kulinda Haki za Watoto ina mapungufu kadhaa.

"Sheria inatoa tu fasili ya usarishaji haramu wa mtoto kama kosa linaloweza kuadhibiwa kwa hukumu ya kifungo cha maisha jela; hata hivyo, haitoi maelekezo yoyote yale ni jinsi gani waathirika watabainishwa na kupatiwa matunzo. Pia iko kimya katika masuala muhimu kama fasili ya ajira, na nini kinaweza kutokea kwa NGO (kwa mfano ya kulea watoto yatima ambayo inatafutia watoto walezi wa kudumu kinyume cha sheria) au kampuni ya basi ambayo inashiriki katika kusafirisha watoto," alisema.

Matewere alisema ni wakati tu serikali itakapokuwa na dhamira ya kisiasa kushughulikia suala hilo ndipo sababu za msingi za tatizo, ambalo analielezea kama umaskini, ukosefu wa ajira, ukosefu wa elimu na ukosefu wa utambulisho wa kitaifa, watoto wengi zaidi wataendelea kusafirishwa kwa njia haramu.

Naibu msemaji wa polisi wa taifa Kelvin Maigwa aliiambia IPS kuwa kati ya Januari na Agosti mwaka huu, kesi 43 za usafirishaji haramu wa watoto ziliripotiwa, ambapo kati ya hizo idadi ilikuwa sawa kati ya watoto wa kike na wa kiume.

"Sababu ni kwa nini watoto hawa wanasafirishwa kutoka majumbani mwao ni kutokana na mabwana zao kutaka wafanyakazi wa ujira mdogo ili watoto wakafanye kazi katika mashamba ya chai na tumbaku na kuwalipa ujira mdogo kutokana na kwamba hawawezi kulalamika. Watoto wa kike kwa kiasi kikubwa wanaingizwa katika ajira za ukahaba katika mabaa na nyumba za kulala wageni ambapo wanavutia wateja wao na mara nyingine kuuza bia, wanaajiriwa pia katika kazi za majumbani katika miji midogo na mikubwa," alisema.

Herbert Bimphi, mwenyekiti wa kamati ya bunge ya masuala ya jamii na mbunge wa chama cha Democratic Progressive Party katika jimbo la Ntchisi Kaskazini, aliiambia IPS kuwa kutokana na kukosekana kwa sheria ya usafirishaji haramu wa watoto mahakama zitaendelea kutoa hukumu ambazo haziendani na kile ambacho kinajitokeza.

"Lakini taarifa nilizonazo ni kuwa Tume ya Sheria imeandaa rasimu ya Muswada wa Usafirishaji wa Binadamu na kwamba kwa sasa upo kwa Waziri wa Sheria na Mambo ya Ndani. Waziri mwenye dhamana ataufikisha Bungeni ili uweze kuangaliwa halafu utakwenda kwa wataalam wengine kuupitia tena kujua kama umeandikwa vizuri, halafu tutaujadili na kuupitisha," alisema.

Waziri wa Jinsia na Masuala ya Watoto Anita Kalinde aliiambia IPS kuwa Muswada wa Usafiridshaji Haramu wa Binadamu unahitimishwa kuandaliwa, lakini kwamba kuna sheria nyingine zinazolinda haki za watoto, ambazo zina vifungu vya kutosha.

"Kinachotakiwa kufanyika ni kuzitangaza sheria hizo kupitia elimu ya umma; na kutafsiri Sheria katika lugha za kienyeji ili watu waweze kudai haki zao," alisema.

Kalinde, hata hivyo, anakubali kuwa hukumu zinazotolewa kwa wahalifu hazitoshi "hasa ikizingatiwa ukweli kwamba usafirishaji haramu wa mtoto unaangamiza maisha yake ya baadaye. Ningependelea kutolewa kwa adhabu kali zaidi."

Alisema zaidi kuwa serikali imeweka mbinu kadhaa za kusaidia kupunguza umaskini miongoni mwa familia ambazo ziko hatarini kutumbukia katika usafirishaji haramu na ajira kwa watoto.

Kalinde alielezea suala la ruzuku za kilimo, ambapo familia maskini zaidi zinanunua pembejeo za kilimo kwa bei ya chini, na hivyo kuwezeshwa kuzalisha kiasi cha kutosha kwa ajili ya familia zao.

Hata hivyo, Maigwa aliiambia IPS sheria za nchi zinaweza kuchochea wahalifu kufanya vitendo vya kihalifu tena.

"Kwa ujumla wake, baadhi ya sheria zimepitwa na wakati na ni dhaifu …haziendani na hali halisi ya sasa. Wakati zikiandaliwa zilikuwa na nguvu lakini kwa sasa kwa mfano kama unamtaka mhalifu kutoa faini ya kwacha 200 (sawa na dola moja) kutokana na kumnyanyasa mtu kwa mfano, hakuna anayeweza kushindwa kufanya hivyo na hivyo kuacha wakosaji kuachiwa huru."

Msemaji wa polisi wa Wilaya ya Phalombe Augustus Nkhwazi aliiambia IPS kuwa wasafirishaji haramu wa watoto wanavuka mpaka wa Msumbiji kwa urahisi kinyume cha sehria kwasababu hakuna maofisa polisi wa nchini Malawi katika kituo cha mpaka huo.

"Wakati watu hawa wakiingia katika nchi hiyo wanaonekana kama wazazi wa watoto au walezi kwasababu watu kutoka nchi hizo mbili wameimarisha uhusiano wa kibiashara ikiwa ni pamoja na kuaona. Kutokana na hali hii kuna wasafiri wanaovuka mipaka kila siku,"alisema Nkhwazi.

Nkhwazi alisema zaidi kuwa vitendo hivyo vinaonekana zaidi katika wilaya yake kutokana na umaskini na kukosekana kwa ardhi ya kilimo ya kutosha na pia wazazi kupenda kushiriki katika vitendo hivyo.

Hata hivyo, Maigwa ana matumaini kuwa muda unabadilika kutokana na kuajiriwa kwa Jeshi la Polisi la Kulinda Watoto katika kila wilaya katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.

"Kila kituo cha polisi kina Kitengo cha Polisi Jamii ambapo tuna Ofisa wa Ulinzi wa Watoto ambaye kimsingi anafanya kazi ya kutoa elimu ya uraia kwa jamii, kuwafundisha juu ya mbinu ambazo wasafirishaji haramu wanazitumia wakifika majumbani mwao, kama vile kutoa ahadi za kupata ajira zenye malipo makubwa au kupata mabadiliko ya haraka ya kiuchumi kwa watoto …hivyo tuna imani kuwa watu wanapata maarifa zaidi juu ya uhalifu huu kuliko ilivyokuwa hapo kabla," alisema. (END/2012)

 

 
 Latest News from Africa
News in RSS
XML error: The element 'html' is used but not declared in the DTD/Schema.
  Dernières Nouvelles
News in RSS
DEVELOPPEMENT: Nous devons penser autrement à la "sécurité"
AUSTRALIE: Le port de Newcastle bloqué par les Guerriers du changement climatique
IRAN: L’examen d’un document clé à l’AIEA suggère un coup d’Israël
PAKISTAN: Les Ahmadis confrontés à la mort ou à l’exil
ETATS-UNIS: Le budget de la défense peut accroître alors que le public est fatigué de la guerre
A lire également>>