Inter Press Service News Agency
Monday, June 18, 2018   10:44 GMT    
   Homepage
   World Service
   East Africa
   Southern Africa
   West Africa
   Central Africa
 
   Environment
   Health-HIV/AIDS
   Education
   Rights
   Politics
   Economics
   and Finance
   Development
   Energy
   Population
   Culture
 
   Radio Service
 
   Français
 
   About IPS
 
   ENGLISH
   ESPAÑOL
   FRANÇAIS
   ARABIC
   DEUTSCH
   ITALIANO
   NEDERLANDS
   PORTUGUÊS
   SUOMI
   SVENSKA
   SWAHILI
   TÜRKÇE
PrintSend to a friend
Readers Opinions


Linapokuja Suala la Njaa, Sifuri ni Namba Pekee Inayokubalika
Na Sabina Zaccaro

ROME, Oktoba 29 (IPS) - Takwimu mpya kutoka Umoja wa Mataifa zinaonyesha kuwa kumekuwepo na mafanikio ya kupunguza njaa kwa wakazi wa dunia. Lakini makadirio kuwa karibu watu milioni 870, mtu mmoja katika kila watu nane, walikabiliwa na ukosefu sugu wa lishe katika kipindi cha miaka miwili iliyopita "haziwezi kukubalika", wanasema wataalam.

Idadi ya watu wanaokabiliwa na njaa sugu imepungua kwa watu milioni 130 tangu mwaka 1990, kupungua kutoka watu bilioni moja hadi milioni 868. Idadi kubwa ya watu hawa, milioni 852, wanaishi katika nchi zinazoendelea, jambo ambalo lina maana kuwa asilimia 15 ya watu katika nchi zinazoendelea wanateseka na njaa, wakati ni watu milioni 16 tu wanakabiliwa na lishe duni katika nchi zilizoendelea.

Wakati huo huo, sehemu ya idadi ya watu ambao wanawekwa kwenye tabaka la watu "wanaopata lishe duni ilipungua kutoka asilimia 18.6 mwaka 1990 hadi kiwango cha sasa cha asilimia 12.5, na kutoka asilimia 23.2 hadi asilimia 14.9 katika nchi zinazoendelea.

Ripoti ya Hali ya Kukosekana Kwa Usalama wa Chakula Duniani Mwaka 2012 (SOFI), ambayo imetolewa kwa pamoja na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) na Shirika la Mpango wa Chakula (WFP), "inawakilisha makadirio mazuri ya lishe duni inayojikita katika kuboresha mbinu na takwimu katika kipindi cha miongo miwili iliyopita."

Ripoti inasema kuwa kama "hatua stahiki" hazijachukuliwa kulisha watu wenye njaa na kupunguza kasi ya kupungua kwa uzalishaji kwa mwaka 2007-2008, lengo la kupunguza nusu ya watu wenye njaa katika ulimwengu unaoendelea ifikapo mwaka 2015 halitafikiwa.

"Kama wastani wa kupungua kwa njaa kila mwaka katika kipindi cha miaka 20 iliyopita utaendelea hadi mwaka 2015, asilimia ya watu wenye lishe duni katika nchi zinazoendelea itafikia asilimia 12.5 – juu ya MDG (Lengo la Maendeleo ya Milenia) la asilimia 11.6, lakini kubwa zaidi kuliko ilivyokadiriwa hapo kabla," inasema ripoti hiyo.

"Habari njema ni kuwa tuna baadhi ya mafanikio lakini bado ina maana kuwa mtu mmoja katika kila watu nane anakumbwa na njaa, na kuwa hili halikubaliki," Mkurugenzi Mkuu wa FAO José Graziano da Silva aliwaambia waandishi wa habari katika makao makuu ya FAO siku ya Jumanne. "Katika FAO namba inayokubalika ya watu wenye njaa ni sifuri tu."

"Hata kama tunapunguza nusu ya watu wenye njaa ifikapo mwaka 2015, ni muhimu kuangalia mbele na kufikia kutokomeza kabisa njaa, na hivyo kujibu wito wa mkutano wa kilele wa Rio+20 wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon wa ‘Changamoto ya Namba Sifuri ya Njaa’," alisema Graziano da Silva.

Hali sasa ni mbaya barani Afrika, ambapo idadi ya watu wenye njaa imeongezeka katika kipindi cha miaka ishirini iliyopita kutoka watu milioni 175 hadi milioni 239. Katika Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, kiasi cha chini kilichofikiwa katika miaka ya karibuni kilibadilika mwaka 2007, huku njaa ikiongezeka kwa asilimia mbili kwa mwaka tangu wakati huo.

Pamoja na ongezeko la idadi ya watu, kiwango cha watu wenye lishe duni katika bara la Asia na Pacific kilipungua kutoka asilimia 23.7 hadi 13.9, hasa kutokana na mafanikio ya kiuchumi na kijamii katika nchi nyingi za ukanda huo.

Amerika Kusini na Caribbean pia ilipata mafanikio, kutoka watu milioni 65 waliokumbwa na njaa hadi watu milioni 49 kati ya mwaka 1990 na 2012, pamoja na kuwa kiwango cha mafanikio kilipungua hivi karibuni.

Nchi katika kanda zenye maendeleo makubwa pia ziliona njaa ikiongezeka kutoka watu milioni 13 hadi milioni 16 kati ya mwaka 2004 na 2012.

Takwimu mpya zilikusanywa kwa kutumia taarifa mpya juu ya idadi ya watu, usambazaji wa chakula, upotevu wa chakula, mahitaji ya mlo wenye lishe kamili na ukokotoaji sahihi zaidi wa kusambaza chakula katika nchi. Njia hii haihusu madhara ya muda mfupi ya kupanda kwa bei za vyakula na mitikisiko mingine ya kiuchumi lakini inalenga zaidi katika idadi ya watu wenye njaa zaidi duniani kote.

Ukuaji wa kiuchumi ni muhimu kwa maendeleo endelevu na maendeleo ya kudumu katika kupunguza njaa na utapiamlo, kwa mujibu wa ripoti. Hata hivyo pia imeonekana kuwa ukuaji peke yake hautoshi kama serikali "haitumii mazingira ya ziada kutoka ukuaji wa uchumi kujenga hatua za kusaidia watu wenye njaa".

Ili kufikia ukuaji halisi, "mifumo ya ulinzi wa kijamii inahitajika kuhakikisha kuwa wenye uwezekano wa kuathirika zaidi pia wanaweza kufaidika na ukuaji na ushiriki huu".

FAO inakadiria kuwa utapiamlo wa watoto unasababisha vifo kutoka kwa zaidi ya watoto milioni 2.5 kila mwaka.Kupungua kwa ulaji wa chakula kunaweza kupunguza kiwango cha lishe muhimu wakati wa siku elfu moja za mwanzo katika maisha yao, kuanzia wanapozaliwa.

"Tunajua kuwa lishe bora katika kipindi hiki inawapatia watoto mwanzo mzuri wa maisha yao," Valerie Guarnieri, mkuu wa mipango wa WFP, aliiambia IPS. "Lishe duni wakati wa awamu hiyo inaweza kusababisha madhara mabaya kwa ukuaji wa mtoto na maendeleo yake. Kama tunaweza kuhakikisha kuwa mama wajawazito na mtoto hadi umri wa miaka miwili wanapata lishe kamili maendeleo ya ubongo wa mtoto, ukuaji wa mtoto unaboreshwa halafu watakuwa na fursa bora zaidi ya kushiriki na kujifunza shuleni.

"Na jambo hilo linachangia kipato kikubwa na maendeleo yao wenyewe na familia zao wanapokua maishani," aliongeza.

Ripoti pia inasisitiza kuwa uhusiano kati ya ukuaji wa kilimo kwa wakulima wadogo na kupungua kwa utapiamlo katika maeneo ya vijijini. "Kuna fursa kubwa ya kukabiliana na umaskini kupitia ukuaji mzuri wa kilimo," Carlos Seré, mwanamkakati mkubwa wa maendeleo wa IFAD, aliiambia IPS. "Mwanzo wa kila jambo inabidi kuwa na mfumo wa ukuaji mzuri, na mfumo wenye ufanisi na endelevu unahitajika."

Ukuaji wa kilimo unahusu wakulima wadogo, hasa wanawake, unaripotiwa kuwa hatua muhimu sana katika kupunguza umaskini uliokithiri na njaa inapozalisha uhaba wa ajira kwa maskini.

Wakati ikionyesha mafanikio, takwimu za Umoja wa Mataifa zilikusanya majibu yanayoonyesha wasiwasi kutoka kwa mashirika ya kiraia.

Kwa mujibu wa Marco de Ponte, katibu mkuu wa ActionAid, Italia, ripoti ya kupungua kwa idadi ya watu wenye njaa inatokana zaidi na ukweli kuwa mgogoro wa chakula duniani una madhara madogo zaidi kwa nchi kama China, India na Indonesia kuliko ilivyokokotolewa katika siku za zamani.

"Hii ina maana kuwa takwimu mpya hazitokani na dhamira kubwa ya kisiasa kutoka kwa serikali kuhusu (kupunguza njaa)," aliiambia IPS. (END/2012)

 

 
 Latest News from Africa
News in RSS
XML error: The element 'html' is used but not declared in the DTD/Schema.
  Dernières Nouvelles
News in RSS
DEVELOPPEMENT: Nous devons penser autrement à la "sécurité"
AUSTRALIE: Le port de Newcastle bloqué par les Guerriers du changement climatique
IRAN: L’examen d’un document clé à l’AIEA suggère un coup d’Israël
PAKISTAN: Les Ahmadis confrontés à la mort ou à l’exil
ETATS-UNIS: Le budget de la défense peut accroître alors que le public est fatigué de la guerre
A lire également>>