Inter Press Service News Agency
Monday, June 18, 2018   10:54 GMT    
   Homepage
   World Service
   East Africa
   Southern Africa
   West Africa
   Central Africa
 
   Environment
   Health-HIV/AIDS
   Education
   Rights
   Politics
   Economics
   and Finance
   Development
   Energy
   Population
   Culture
 
   Radio Service
 
   Français
 
   About IPS
 
   ENGLISH
   ESPAÑOL
   FRANÇAIS
   ARABIC
   DEUTSCH
   ITALIANO
   NEDERLANDS
   PORTUGUÊS
   SUOMI
   SVENSKA
   SWAHILI
   TÜRKÇE
PrintSend to a friend
Readers Opinions

Mwasali na Majibu
Lazima Wanawake na Wasichana Kuwa Mbele na Katikati
Na Malgorzata Stawecka

UMOJA WA MATAIFA, Oktoba 29 (IPS) - Malgorzata Stawecka anamhoji BABATUNDE OSOTIMEHIN, mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Idadi ya Watu la Umoja wa Mataifa Wakati idadi ya watu duniani wakiwa katika hali ya kufikia bilioni tisa ifikapo mwaka 2050, kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa, mpango wa kuchukua hatua unahitajika kukabiliana na changamoto za kukomesha umaskini, kuhakikisha mfumo wa afya unaofanya kazi vizuri na upatikanaji wa elimu, ikiwa ni kuhakikisha ushirikishwaji wa kijamii wa kila mmoja.

"Idadi ya watu duniani ina maana nyingi, haihusiki tu na ongezeko, lakini kuna masuala mengine ambayo yanafaa kutafutiwa ufumbuzi," alisema Babatunde Osotimehin, mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA), shirika ambalo linashiriki katika kutetea haki za binadamu na usawa wa kijinsia, kwa kulenga zaidi katika vijana na wanawake.

"Na naweza kuzipata kwa kuangalia kile ninachoweza kukiita aina tofauti ya maisha," aliongeza wakati wa mahojiano na IPS.

Osotimehin alisema kuwa, ukiachana an suala la migogro ya sasa ya kiuchumi na kimazingira duniani, msisitizo zaidi lazima uwekwe katika masuala kama ya wazee, upatikanaji wa afya ya uzazi na elimu ikiwa ni pamoja na kuwapatia uwezo wanawake na vijana.

Akizungumza na mwandishi wa habari wa IPS Malgorzata Stawecka wakati wa uzinduzi mpango wa katiba mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon wa ‘Elimu Kwanza ‘ siku ya Ijumaa, Osotimehin alielezea jinsi gani nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa pamoja na UNFPA wanajiandaa kukabiliana na changamoto za dunia ya watu bilioni tisa.

Sehemu ya mazungumzo inafuata. Swali: Nini kitakuwa shabaha kuu ya UNFPA mwaka ujao? Uzee? Uzazi wa Mpango? Ongezeko la Idadi ya watu katika dunia inayoendelea? Jibu: Kuna mambo makuu mawili ambayo tunayashughulikia. Kwanza vijana wote ambao wana umri wa kuzaa au watakaokuja kuwa na uwezo wa kuzaa katika maisha yao. Kutokana na ukweli kwamba wengi wa vijana hawa wanaishi katika dunia inayoendelea, ambako ongezeko la idadi ya watu bado ni la kasi kubwa, shirika linafanya kazi na serikali kutafutia ufumbuzi masuala ya elimu ya kina ya kujamiiana, kwa ujumla kwa watoto wa kike, kuhakikisha kuwa tunawapatia uwezo wa kutumia fursa zao kikamilifu, kwasababu tunajua kuwa wakati watoto wa kike wanapoelimika wanatafuta machaguo tofauti katika maisha yao.

Huduma za afya ya uzazi zinaingizwa katika mpango na tunafanya kazi na serikali kuweka pamoja sera na kuhakikisha kuwa kuna fursa kwa watu kufanya uchaguzi bila kutumia nguvu. Kama utafikia ngazi hiyo, utapunguza ongezeko la idadi ya watu. Na tutaendelea kufanya hivyo. Tumefanya hivyo katika nchi nyingi na imefanikiwa.

Ili kwenda pamoja na mfumo unaojikita katika haki, kutoa huduma za elimu, itakuwa ni jambo sahihi la kufanya. Kwa sasa hiyo ni sehemu ya jambo hilo.

Kuna sehemu ya jambo hilo ambapo unaliangalia na kuona kuwa idadi ya watu wanazidi kuwa wazee na kwamba nchi zinazidi kunyong’onyea kutokana na kuwa na idadi kubwa ya watu.

Hapo ni lazima uwezo wa kuzalisha uathirike kwasababu tutakuja kuwa na vijana wachache kuliko wazee. Leo hii mtu mmoja katika kila tisa duniani ana umri wa zaidi ya miaka 60. Lakini ifikapo mwaka 2050, mtu mmoja katika kila watano atakuwa na umri wa zaidi ya miaka 60. Hivyo, tunaona kuongezeka kwa wazee. Ni lazima kujua jambo hilo.

Katika kujaribu kuweka mifumo na sera za kijamii tunaangalia kuongezeka kwa wazee kuna maana gani katika uzalishaji, kuendesha huduma, ajira, sera za kijamii, huduma za jamii, afya, nyumba na elimu. Haya ni masuala ambayo tunayashughulikia na hii ndiyo njia ya jinsi ya kuyashughulikia kwa kushirikiana na serikali.

Swali: Unadhani mgogoro wa sasa wa kiuchumi barani Ulaya, utakuwa na madhara katika kufadhili programu za idadi ya watu duniani kote? Jibu: Mgogoro wa sasa wa kiuchumi unaweza kuathiri programu za idadi ya watu kwasababu hatujui ni kwa muda gani hili litaendelea. Baadhi ya wafadhili wanaathirika wakati huu, lakini tuna imani ufumbuzi utapatikana kuhusu mgogoro wa nchi zinazotumia sarafu ya euro na kuanza kuona tofauti katika utoaji wa misaada ya maendeleo ya nje.

Lakini pengine pia ni wakati ambapo tunapaswa kuanza kuangalia mifumo ya maendeleo kwa macho tofauti. Kwa mfano, tunachofanya katika ‘makubaliano ya Busan’ ambayo yanahusu hasa ushirikiano wa nchi za Kusini, ushirikiano badala ya utoaji wa misaada una mantiki, misaada ya kiufundi, njia za kuathiri mchakato wa maendeleo, ambayo inaweza isitegemee kabisa katika fedha.

Mwisho ni kukosoa nchi zenye uchumi unaoibukia kuanza kushiriki katika ajenda ya maendeleo kupitia ushirikiano wa kusini na kuhakikisha kuwa ubadilishanaji huu wa uzoefu unatumika katika kanda zote za dunia. Nadhani hilo ndilo litakuja kujitokeza.

Swali: Mpango wa utekelezaji uliopitishwa mwaka 1994 na Mkutano wa Kimataifa wa Idadi ya Watu na Maendeleo (ICPD) mjini Cairo utaadhimisha miaka 20 mwaka 2014.Unafikiria kutakuwepo na mkutano mwingine? Jibu: Hakutakuja kuwa na mkutano wa kimataifa, lakini mkutano wa wakubwa katika Umoja wa Mataifa. Nadhani kuwa katika mahali ambapo tupo sasa, kuangalia jinsi gani tumekwenda mbali katika mchakato wa Cairo na ifikapo mwaka 2014 tutakuja kuwa na ripoti ya katibu mkuu juu ya nini tayari tumekifanya kwa kutumia mifumo sahihi ya afya ya uzazi, lakini kimsingi kubainisha mapengo, ni mambo gani tunahitaji kuyaendeleza, katika programu.

Tutaweza kutumia hilo kuingiza katika ajenda zetu, lakini suala muhimu zaidi ni kuingiza katika ajenda ya maendeleo ya mwaka 2015 kwasababu afya ya uzazi na haki za wanawake na wasichana zinapaswa kuwa mstari wa mbele na katikati kwa ajili yetu kuweza kufanya maendeleo.

Swali: Nini hasa ni mafanikio na mapungufu ya ICPD? Je fedha zinazolenga ICPD zimefikiwa? Kama siyo, mapungufu yana ukubwa gani?

Jibu: Malengo ya kutafuta fedha hayajafikiwa hadi sasa. Nisingeweza kukuambia ni kiasi gani, lakini tumepata mafanikio. Kama unavyoweza kuona, kuna ongezeko kubwa la wanawake wanaojiunga na shule duniani. Pia tumeweza kutoa elimu ya kina ya uzazi wa mpango katika nchi nyingi kuboresha mazingira ya kisera na afya ya uzazi.

Pia tumeshuhudia matumizi makubwa ya serikali katika eneo hili. Hata kama kuna changamoto nyingi, kama vile upinzani dhidi ya masuala ya wanawake kuhakikisha afya na haki ya uzazi, lakini nadhani kwa ujumla wake, tutapata mafanikio makubwa.

Swali: Kwa kuzindua mpango wa ‘Elimu Kwanza’, mpango wa elimu wa kimataifa wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon, jukumu la UNFPA litakuwa ni lipi?

Jibu: Jukumu la UNFPA katika mpango huu ni kuonyesha mtimzamo wa kipekee katika elimu. A) Juu ya suala la sasa la elimu kwa mtoto wa kike ambalo ni la msingi kwa maendeleo ya kitaifa; B) kusisitiza kuwa elimu ni ya kina na kuhusisha elimu ya kina ya kujamiiana; C) pia kwenda mbali kuzungumzia kuhusu uwezeshwaji wa vijana na kuwapatia ujuzi kuweza kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya taifa. Hilo ndilo tunalileta.

Miaka mitatu iliyopita, nilisema vijana ni taifa la kesho na niliambiwa na vijana, "Hapana, tupo hapa. Sisi siyo wa taifa la kesho, ni taifa la leo." Na hii ni kweli. Kutokana na mabadiliko ambayo yamejitokeza Afrika Kaskazini yaliyofanywa na vijana na haya ndiyo yanayojitokeza duniani kote sasa.

Kuna changamoto kwa sisi sote, lakini ni muhimu kuona jinsi gani tutahakikisha kuwa vijana ni sehemu ya mjadala na kuwa wanajiona kuwa sehemu ya ufumbuzi na wala siyo sehemu ya tatizo. (END/2012)

 

 
 Latest News from Africa
News in RSS
XML error: The element 'html' is used but not declared in the DTD/Schema.
  Dernières Nouvelles
News in RSS
DEVELOPPEMENT: Nous devons penser autrement à la "sécurité"
AUSTRALIE: Le port de Newcastle bloqué par les Guerriers du changement climatique
IRAN: L’examen d’un document clé à l’AIEA suggère un coup d’Israël
PAKISTAN: Les Ahmadis confrontés à la mort ou à l’exil
ETATS-UNIS: Le budget de la défense peut accroître alors que le public est fatigué de la guerre
A lire également>>