Inter Press Service News Agency
Saturday, June 23, 2018   07:12 GMT    
   Homepage
   World Service
   East Africa
   Southern Africa
   West Africa
   Central Africa
 
   Environment
   Health-HIV/AIDS
   Education
   Rights
   Politics
   Economics
   and Finance
   Development
   Energy
   Population
   Culture
 
   Radio Service
 
   Français
 
   About IPS
 
   ENGLISH
   ESPAÑOL
   FRANÇAIS
   ARABIC
   DEUTSCH
   ITALIANO
   NEDERLANDS
   PORTUGUÊS
   SUOMI
   SVENSKA
   SWAHILI
   TÜRKÇE
PrintSend to a friend
Readers Opinions


Kuwafanya Watoto wa Kike Kuendelea na Masomo
Na Andrew Green

KAMULI, Uganda, Oktoba 23 (IPS) - Miaka mitatu iliyopita, baada ya Irene Kamyuka kumaliza miaka yake sita ya shule ya msingi nchini Uganda, baba yake alifilisika. Huku akiwa na ndugu zake wa tumbo moja wanne wakiwa wanasoma, baba yake Kamyuka alimwambia binti yake huyo kuachana na shule hadi hali yake ya kifedha itakapokuwa nzuri. "Baba aliniambia kuwa hana pesa," alisema. "Baba alisema: Subiri hadi wengine watakampomaliza kusoma.’"

Kamyuka, ambaye alikuwa na shauku la kusoma kutokana na kutaka kupata ajira siku za mbeleni," aliachana na ndoto yake hiyo. Hatimaye fedha za kutosha zilipatikana hivyo kuwa na uwezo wa kumaliza shule ya msingi katika darasa la saba, Mei mwaka huu. Halafu baba akawa hana pesa tena kabla ya kumpeleka shule ya sekondari.

Pamoja na kuwa taifa hili la Afrika mashariki linaendesha shule za serikali ambazo kinadharia ni bure, katika uhalisia wazazi ambao hawawezi kumudu sare za shule, vitabu na matumizi mengine hawawezi kupeleka watoto wao shule.

Waganda wanaoishi katika maeneo ya kijijini kama Kamyuka, kutoka Kamuli – mji kandokando mwa Ziwa Kyoga katikati mwa Uganda – na ambao wanaishi kwa kutegemea kilimo kidogo kidogo, wanakabiliwa na magumu ya mara kwa mara kulipa ada za shule za watoto wao.

Kwa suala la Kamyuka, matokeo ya ndoto mara nyingi yanaingiliwa au yanafutwa. Wakiwa wameacha shule, watoto wa kike wanasema wananyanyapawa kwasababu watu wanadhani wameacha shule kutokana na kufanya mapenzi. Katika hali halisi, uchaguzi wa kuendelea kusoma siyo wao kwasababu mara nyingi wazazi wanaona kipaumbele kidogo kwa mabinti zao kumaliza masomo.

"Wanaona watoto wa kike kama mzigo, kwasababu familia zinawaandaa kwa ajili ya kuolewa," alisema Johnson Ntende, mkurugenzi wa Shule ya Kamuli, sekondari katikati mwa mji huo. "Jukumu la mke katika familia ni kupika kwa ajili ya watoto na kumtunza mume. Jukumu hilo halihitaji mafanikio shuleni."

Kwa mujibu wa takwimu za awali za Wizara ya Elimu ya Uganda mwaka 2012 wa shule, idadi ya watoto wa kike ambao walihitimu kwenda shule ya sekondari ilikuwa 343,000, ikilinganishwa na wanaume 408,000.

Kwa mujibu wa Benki ya Dunia, kiwango cha kujua kusoma na kuandika miongoni mwa vijana wa kike wa umri kati ya miaka 15 hadi 24 katika taifa hili la Afrika mashariki lisilokuwa na bandari lenye wakazi milioni 35 ni asilimia 84 mwaka 2010, ikilinganishwa na asilimia 90 ya wanaume katika kundi kama hilo. Hii ni hali inayojionyesha katika dunia nzima, huku watoto wa kike wakiwa na fursa ndogo ya kujiunga shule na kupata huduma za kitabibu na kuwa na uwezekano mkubwa wa kunyimwa chakula.

Matokeo yake, kwa mujibu wa utafiti wa Benki ya Dunia, ni kundi lenye uzalishaji duni na ambalo linaandamwa zaidi na umaskini katika jamii.

Kwa suala la Kamyuka, wazazi wake walitaka kumpeleka shule, lakini hawakuwa na uwezo. Kijana huyo mwenye umri wa miaka 15 kwa sasa anasoma mwaka wake wa kwanza katika shule ya Kamuli Progressive College, kutokana na msaada wa shirika la Plan International. Alianza kusoma Agosti mwaka huu.

Shirika hilo la misaada ya kimaendeleo ya kimataifa linalipia ada, ambazo ni sawa na dola 20 kwa kila kipindi cha miezi mitatu. Wakati shule ipo katika mpangilio wa ushirikiano wa sekta ya umma na binafsi na inapokea baadhi ya ufadhili kutoka serikalini chini ya mpango wa elimu ya msingi, kuna baadhi ya michango ya ziada kwa ajili ya sare na vitabu.

Gloria Titi, mratibu wa mipango wa Plan International, alisema kuwa kwa kuongeza katika kulipia watoto wa kike 54 katika eneo la shule, shirika linatafuta njia za kuboresha uwezeshaji ndani na nje ya shule kuondokana na suala la kushindwa kumaliza masomo kiwango ambacho bado ni kikubwa – na mara nyingi halitokani na kukosa fedha.

Hadi watoto wa kike asilimia 54 mjini Kamuli wataacha shule kabla ya kuhitimu, kwa mujibu wa Titi. Katika shule ya Kamuli Progressive College, kuna chati katika ukuta wa ofisi ya mkurugenzi ikiorodhesha takwimu za watoto waliojiunga shule. Kuna watoto wa kike 133 waliojiunga na shule katika mwaka wao wa nne; idadi ilishuka kwa 21 katika darasa la tano.

Sababu ni nyingi: kubughudhiwa na wanaume wakiwa wanatembea umbali mrefu kwenda shule, kukosekana kwa vyoo vyenye usiri, na kukosekana kwa pesa za kununulia taulo la usafi wakati wakiwa mwezini. Kamyuka alisema kuwa baadhi ya watoto wa kiume shuleni kwake wanawalenga watoto wa kike kwa ajili ya kufanya mapenzi ya kuridhia au ya nguvu, jambo ambalo linaweza kuathiri hadhi ya mtoto wa kike. Na kama anapata mimba, analazimishwa kuacha shule, wakati baba wa mtoto anaendelea kusoma.

"(Wanafunzi wa kike) wanaanza kuwapenda watoto wa kiume, jambo linalowapeleka kuacha shule," Kamyuka alisema. "Watoto wa kiume wanaharibu tu maisha yetu."

Kamyuka na wanafunzi wenzake wanasema bila elimu, kuolewa mapema ni chaguo pekee kwao. Wazo hilo linajulikana sana katika jamii za Uganda. Lilimfanya Claire Namakula kuwa katika uhusiano wa unyanyasaji wa miaka miwili.

Akiwa na umri wa miaka 15 alifanya mapenzi na kijana – ambaye "alikuwa akinipiga, alikuwa akitumia madawa ya kulevya, akilewa pombe , akivuta sigara" – halafu nikapata mimba. Baada ya miaka miwili, na pamoja na kukosa pesa, alichukua hatua isiyokuwa ya kawaida katika mji wake mkuu wa Uganda, Kampala.

Namakula, ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 28 na alinyimwa fursa ya kwenda shule, alisomea masuala ya vyakula kwa ajili ya wanawake wenye elimu ndogo. Alipomaliza masomo, yeye na wanawake wengine walianzisha kampuni ya chakula, ambayo waliita "Allied Female Youth Initiative". Alisema mafunzo yalimuonyesha kuwa ana machaguo mengine mbali ya kutegemea rafiki wa kiume au mume.

Kabla ya mafunzo, "Sikuweza hata kuwa na akaunti ya benki," Namakula alisema. "Watu wasingeniheshimu. Sasa watu wanaweza kunipigia magoti na kusema ‘mambo’ kwasababu ni mtu mwenye majukumu." (END/2012)

 

 
 Latest News from Africa
News in RSS
XML error: The element 'html' is used but not declared in the DTD/Schema.
  Dernières Nouvelles
News in RSS
DEVELOPPEMENT: Nous devons penser autrement à la "sécurité"
AUSTRALIE: Le port de Newcastle bloqué par les Guerriers du changement climatique
IRAN: L’examen d’un document clé à l’AIEA suggère un coup d’Israël
PAKISTAN: Les Ahmadis confrontés à la mort ou à l’exil
ETATS-UNIS: Le budget de la défense peut accroître alors que le public est fatigué de la guerre
A lire également>>