Inter Press Service News Agency
Saturday, June 23, 2018   07:12 GMT    
   Homepage
   World Service
   East Africa
   Southern Africa
   West Africa
   Central Africa
 
   Environment
   Health-HIV/AIDS
   Education
   Rights
   Politics
   Economics
   and Finance
   Development
   Energy
   Population
   Culture
 
   Radio Service
 
   Français
 
   About IPS
 
   ENGLISH
   ESPAÑOL
   FRANÇAIS
   ARABIC
   DEUTSCH
   ITALIANO
   NEDERLANDS
   PORTUGUÊS
   SUOMI
   SVENSKA
   SWAHILI
   TÜRKÇE
PrintSend to a friend
Readers Opinions


Nafasi ya Pili kwa Mapinduzi ya Kijani Afrika
Sabina-Zaccaro

ROME, Oktoba 23 (IPS) - Wakati dunia ikisaka njia za kuzalisha chakula kufikia angalau asilimia 70 ifikapo mwaka 2050 kulisha idadi kubwa ya watu wanaozidi kukumbwa na njaa, wengi wanaangalia barani Afrika kama eneo muhimu kufikia malengo haya, zaidi kutokana na kuwa na eneo kubwa la ardhi.

Mjini Arusha, Tazania, hivi karibuni kumekuwa eneo la kuumiza vichwa juu ya mada hii, wakati ambapo wahusika wengi wa Jukwaa la mapinduzi ya Kijani Afrika (AGRF) walikutana kuanzia Sept. 26 hadi 28, kwa nia ya kuleta usalama wa chakula unaoongozwa na Afrika.

Katika mkutano wa kilele wa mataifa yenye viwanda vingi duniani ya G8, viongozi wa dunia ikiwa ni pamoja na wale wanaotoka mataifa 21 ya Afrika na makampuni binafsi 27 walitoa dola bilioni tatu kusaidia umoja mpya wa kuleta usalama wa chakula na lishe.

Lengo lao ni kuondoa watu milioni 50 kutoka katika umaskini katika kipindi cha miaka 10 ijayo. AGRF imejengeka kuhamasisha dhamira ya viongozi wa Afrika kwa kukuza uwekezaji wa dharula na sera za kusaidia kuongeza uzalishaji wa kilimo na kipato kwa wakulima wa Afrika – hasa kupitia mbinu za kilimo endelevu na mifumo ya kiubunifu ya ufadhili wa kilimo.

Rais wa IFAD, Dk. Kanayo F. Nwanze, alizungumzia masuala haya katika Jukwaa la Arusha katika jopo la mjadala lililolenga juu ya jinsi gani ya kufanya masoko ya kitaifa na kikanda Afrika kufanya kazi.

Ukuaji wa kilimo wa hivi karibuni nchini Tanzania ni mfano wa nini kinawezekana, wanasema waandalizi wa jukwaa hilo. Katika wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro, mazao ya mahindi yanayolimwa na wakulima wadogo yameongezeka hivi karibuni kutoka tani 1.5 hadi 4.5 kwa hekta; mavuno ya mpunga yameongezeka kutoka tani 2.5 hadi 6.5 kwa hekta.

Wakulima hao wadogo ni muhimu kwa ukuaji wa kilinmo barani Afrika na kunatambuliwa kwa kiasi kikubwa, na wanaharakati wanatarajia jukwaa "litajadili njia mpya za kutoa rasilimali, kukabiliana na changamoto na kuboresha mavuno kwa mamilioni ya wakulima ambao wanafanya kazi katika chini ya hekta moja ya ardhi katika bara hilo".

Kwa mujibu wa Carlos Seré, mwanamkakati mkuu wa maendeleo katika shirika la Maendeleo ya Kilimo la Kimataifa (IFAD), kuongeza uwekezaji katika kilimo ni suala muhimu sana. "Tunataka kuwekeza katika kilimo kwani mapinduzi ya kijani ni jambo ambalo soko litayaendesha lenyewe."

"Kwa sasa tunakubali kuwa tuna hifadhi ndogo. Hifadhi kubwa, kwa mfano nafaka, zinazohifadhiwa na mashirika ya serikali kwa sasa zimepungua kwa kiasi kikubwa. Hivyo wakati ukame nchini Marekani au Australia, au matatizo nchini Russia yalipokumba masoko haya, bei zinapanda kwa kasi kutokana na hakuna kiwango kikubwa cha hifadhi kama ilivyokuwa hapo zamani."

Uwekezaji katika kilimo una faida kubwa za moja kwa moja katika maisha ya wakulima wadogo, ambao wanaendesha maeneo makubwa ya ardhi katika dunia inayoendelea.

"Wanahitaji bidhaa zaidi za umma kwa njia ya utafiti, ugani na mazingira mazuri ya sera," Seré aliiambia IPS.

"IFAD inashiriki kikamilifu katika kusaidia serikali kufanya hivyo. Kazi yetu ni kuhusu kuongeza usambazaji wa chakula, na kusaidia kujenga nguvu ya wakulima wadogo na mashirika yao kuwa na ufanisi zaidi, kutumia ardhi kwa ufanisi zaidi, kugawana maarifa, kujipanga vizuri, na kuongeza uzalishaji wao katika hali ambayo ni ya gharama nafuu, kufikisha chakula mijini na masokoni bila gharama kubwa."

Watu wengi maskini wanatumia zaidi ya nusu ya kipato chao kwa ajili ya chakula, na hivyo kuwafanya kuwa rahisi kuathirika na bei za chakula.

Ripoti ya bei ya chakula ya FAO, ambayo inapima bei za kila mwezi na jinsi zinavyobadilika ambazo zinahusu nafaka, mbegu za mafuta, bidhaa za maziwa, nyama na sukari, ilikuwa wastani wa 213 mwezi Agosti, na kutokubadilika mwezi Julai. Pamoja na bei kuwa bado ziko juu, ripoti ya FAO kwa sasa inasimamia katika 25 chini ya kiwango cha juu zaidi cha 238 mwezi Februari 2011 na 18 chini ya kiwango chake cha Agosti mwaka 2011.

Kwa mujibu wa FAO, ripoti hiyo inapima kwa pamoja na kuwa uangalizi unahitajika, bei za sasa "hazihalalishi mazungumzo ya mgogoro wa chakula duniani".

"Hii ni hali tofauti mno ikilinganishwa na kile tulichokuwa nacho miaka iliyopita," Seré aliiambia IPS. "Tunakubali kuwa hali hii inafaa kufuatiliwa kwa karibu, lakini hatuoni kuwa na uzito mkubwa kama ilivyokuwa hapo kabla."

Wataalam wa usalama wa chakula wana imani kuwa jumuiya ya kimataifa kwa sasa inajiandaa vizuri kushughulikia bei za vyakula kuliko ilivyokuwa hapo kabla mwaka 2007 na 2008. "Tuna mifumo mizuri vya uratibu, uchambuzi, na kupeana taarifa," kwa mujibu wa Seré.

Changamoto nyingi bado zipo. "Kuna haja ya ukuaji wa uzalishaji, hasa mifumo ya wakulima wadogo, kilimo kinachokabiliana vyema na mabadiliko ya hali ya hewa, masoko yanayofanya kazi vizuri na yaliyounganishwa, na vipato vya juu na vilivyotulia kwa wanawake na wanaume wanaoishi katika umaskini," Seré alisema.

Masuala yote haya yanapaswa kuwa sehemu ya ajenda zinazoendelea, ambazo zinakwenda mbali ya mifano maalum ya kupanda kwa bei za vyakula.

Jambo linalowasumbua wataalam ni kukosekana kwa ufahamu wa kuunganisha matokeo ya usalama wa chakula. Lakini wakati bei za nafaka zilianza kupanda duniani hadi kwenye ngazi ya juu mwezi Juni mwaka huu, kufuatia ukame mbaya zaidi kuipiga Marekani – mzalishaji mkuu wa mahindi na maharage – ilitoa ujumbe mzito kuhusu mfumo wa chakula duniani uliounganika.

"Nadhani ni muhimu kufanya uhusiano kati ya mgogoro wa chakula nyumbani na nini kinatokea katika maeneo mengine ya dunia," Seré alisema. "Mara nyingi watu hawaelewi vizuri jinsi gani masuala haya yanaunganika. Kwa mfano, maharage kwa ajili ya kulisha nguruwe nchini Ujerumani yanakuja kutoka Brazili, (ambayo) imeathirika kutokana na kukatwa kwa misitu ya mvua halafu linakuja suala la ajira inayotokana na uzalishaji huu wa bidhaa hizi katika maeneo tofauti."

Ni uchambuzi tu wa jumla wa mfumo wa chakula unaweza kuleta ufumbuzi kamili wa mgogoro wa chakula duniani. (END/2012)

 

 
 Latest News from Africa
News in RSS
XML error: The element 'html' is used but not declared in the DTD/Schema.
  Dernières Nouvelles
News in RSS
DEVELOPPEMENT: Nous devons penser autrement à la "sécurité"
AUSTRALIE: Le port de Newcastle bloqué par les Guerriers du changement climatique
IRAN: L’examen d’un document clé à l’AIEA suggère un coup d’Israël
PAKISTAN: Les Ahmadis confrontés à la mort ou à l’exil
ETATS-UNIS: Le budget de la défense peut accroître alors que le public est fatigué de la guerre
A lire également>>