Inter Press Service News Agency
Saturday, June 23, 2018   07:12 GMT    
   Homepage
   World Service
   East Africa
   Southern Africa
   West Africa
   Central Africa
 
   Environment
   Health-HIV/AIDS
   Education
   Rights
   Politics
   Economics
   and Finance
   Development
   Energy
   Population
   Culture
 
   Radio Service
 
   Français
 
   About IPS
 
   ENGLISH
   ESPAÑOL
   FRANÇAIS
   ARABIC
   DEUTSCH
   ITALIANO
   NEDERLANDS
   PORTUGUÊS
   SUOMI
   SVENSKA
   SWAHILI
   TÜRKÇE
PrintSend to a friend
Readers Opinions


Kampuni ya Marekani Yadaiwa Kusaidia ‘Uporaji wa Ardhi’ Cameroon - U.S.
Carey L. Biron

WASHINGTON, Oktoba 23 (IPS) - Mashirika ya mazingira yanatuhumu kampuni ya kilimo yenye makao yake jijini New York, Herakles Farms, kutokana na kuendelea na mipango yake ya kuchukua shamba la mafuta ya mawese lenye ukubwa wa hekta 73,000 na mtambo wa kusafishia mafuta hayo kusini magharibi mwa Cameroon pamoja na kutokupata ridhaa ya serikali, pingamizi mbili za mahakama, na kuendelea kwa upinzani kutoka kwa jamii.

Siku ya Jumatano, Taasisi ya Oakland na Greenpeace, mashirika mawili ya kupigania utunzaji wa mazingira yenye makao yake hapa Marekani, yalitoa ripoti inayoonyesha kuwa mradi huo uliopo katika eneo ambalo lipo katika sehemu yenye utajiri mkubwa wa bioanuwai kati ya maeneo mawili ya hifadhi kubwa, kungeathiri vibaya watu 45,000.

Mashirika hayo yanaonya kuwa mradi, ambao unahusishwa na Blackstone Group, kampuni kubwa ya uwekezaji, inawakilisha harakati mpya "za kugombea ardhi" barani Afrika kunakofanywa na makampuni ya Magharibi.

"Herakles inadai kushiriki katika kuboresha usalama wa chakula nchini Cameroon na hali ya kibinadamu, lakini tumegundua huu kuwa ni udanganyifu. Kwa uhakika, wanakaribia kuangamiza vyanzo vya kipato vya maelfu," Frederic Mousseau, mwandishi wa ripoti hiyo, alisema katika vyombo vya habari Jumatano.

"Vile vile, Herakles inadai kupata kuungwa mkono na wenyeji wa maeneo husika, lakini tumegundua kuwa huu ni uongo wa wazi. Mwisho, madai kuwa ardhi hii ni msitu wa kupandwa na kuwa umeharibiwa yanapotosha ukweli wa mambo. Ukweli ni kwamba, eneo kubwa halijakatwa miti." (Hadi kuandika taarifa hii, maofisa wa Herakles hawajajibu maombi ya kuwataka kutoa maoni yao.)

Mradi huo, unaosimamiwa na kampuni ndogo ya Herakles ijulikanayo kama SG Sustainable Oils Cameroon (SGSOC), bado upo katika hatua za awali, ambapo kwa sasa una vitalu vitatu vya miche ya miti. "Kwa sasa tunasubiri uamuzi wa serikali ya Cameroon kwenda mbele zaidi ya vitalu vya miti," Mousseau anasema. "Hivyo huu ni wakati muhimu sana – mradi unaweza kusimamishwa."

Upinzani dhidi ya SGSOC ulipata nguvu mpya katika wiki iliyopita, kufuatia taarifa ya Agosti 24 kuwa Herakles ilikuwa ikiondoa mradi kutoka katika taratibu maalum za kuzingatia miongozo ya kiikolojia inayojulikana kama Roundtable on Sustainable Palm Oil (RSPO).

Katika kuelezea hatua hiyo, Herakles, ambayo inajipambanua yenyewe kama "yenye dhamira ya kushughulikia masuala mazito ya usalama wa chakula kupitia mipango ya kilimo endelevu", ilitoa mfano wa muda mrefu ambao maombi yake ya RSPO yamechukua, wakati ikibainisha kuwa ilikuwa "ikishughulikia mahitaji makubwa ya kibinadamu" nchini Cameroon.

Hakuna uidhinishwaji wa haraka

Uhalali wa vitalu vya miche ya miti tayari umeanza kuhojiwa. Pamoja na kuwa SGSOC ilisaini mkataba na serikali wa kumiliki ardhi kwa miaka 99 mwaka 2009, sheria za Cameroon zinataka matumizi ya ardhi kubwa kama hiyo kupewa kibali na rais.

Kutokana na kibali hicho bado hakijatolewa, wanaharakati wanapendekeza kuwa SGSOC haina msingi wa kisheria wa kuanza kulima ardhi na mashamba ya kakao na mbogamboga ambapo wanajamii walitegemea.

Jaji wa nchini humo aliandaa mashitaka mawili dhidi ya hatua za serikali hizo, lakini kwa mujibu wa waangalizi wa ndani kampuni imekataa kuridhia.

"Siyo tu kwamba wanataka kuzingatia sheria zilizopo, lakini kampuni imegeuza mgongo wake juu ya mbinu endelevu," anasema Samuel Nguiffo, mwanasheria na mkurugenzi wa Kituo cha Mazingira na Maendeleo, katika mji mkuu wa Cameroon, Yaounde. "Muundo wa serikali nchini mwetu ni dhaifu sana, hivyo tunataka serikali ya Marekani kuisimamisha kampuni hiyo."

Maofisa wa Herakles wanasema kuwa wameungwa mkono na jumuiya kuendesha mradi huo, lakini mashuhuda wanasema hii haina uhakika.

"Wakati kampuni ilipofika hapa, walisema kuwa mradi huu tayari umeshaidhinishwa na rais wa Cameroon … Tuliamua kuwa kimya tu," Edward Ndomo, mwenyekiti wa baraza la jadi, aliwaambia watafiti wa Taasisi ya Oakland wanaoandaa kipindi kipya cha televisheni. "Hatujawahi kuwa na mikutano kamili na kampuni."

Marie Meboka Boya, mbunge anayewakilisha eneo hilo ambako vitalu vya miti vimejengwa, aliwaambia watafiti kuwa anadhani kampuni imechukua mfumo wa "manunuzi", kutoa fedha kidogo au chakula kwa ajili ya kuungwa mkono na wakazi wenyeji.

"Kutokana na maelezo ya jamii na mtizamo usiokuwa na ukweli wa kampuni hiyo," anasema, "Najua kuwa hakuna mkataba kamili."

Kugombania ardhi Afrika

Mradi wa Herakles ni moja ya idadi kubwa ya mipango ya uwekezaji wa wageni katika ardhi barani Afrika. Na pamoja na ukubwa wake, mradi huo siyo mkubwa kuliko yote – kwani nchini Kongo, kwa mfano, mpango wa mamilioni ya hekta umejadiliwa.

"Kuna watu wengi wa Ulaya na Marekani ambao wanatafuta ardhi mpya barani Afrika kwa sasa, tuna wasiwasi kuwa utafutaji wa ardhi unaweza kuchukua sura mpya na kuwa mkubwa mno," Rolf Skar wa Greenpeace anasema.

Pamoja na Cameroon kuwa mzalishaji mpya mkubwa wa mafuta ya mawese, wengi wanapendekeza sasa kuwa kinachotokea kwa kampuni ya Herakles kinaweza kuwa mfano kwa bara zima.

"Kama tunathibitisha kuwa mpango huu ni mbaya, kampuni zote zinazokuja zitakuwa na mipango mibaya kama ilivyo kwa Herakles," anasema Nguiffo.

"Cameroon na chi jirani kwa sasa zinakabiliwa na mahitaji makubwa ya ardhi, na ushindani wa ardhi mkubwa kama huu ni mpya sana kwetu sisi – unashangaza. Ni wazi kuwa mfumo wa serikali nchini mwetu ni dhaifu mno, hivyo tunataka Marekani kusimamisha kampuni hii."

Nguiffo anasema kuwa wakati Cameroon kwa sasa ina hekta zipatazo 500,000 zinazotumika kama shamba makubwa ya kilimo cha biashara, zaidi katika mashamba ya zamani, katika kipindi cha miaka mitatu mahitaji ya ardhi yameongezeka mno hadi kufikia hekta milioni tatu, kutokana na ongezeko la wawekezaji wa kigeni wanaoungwa mkono na serikali zao na mashirika ya kimataifa yanayotoa mikopo.

"Wahisani na taasisi za fedha za kimataifa wamezidi kuzitaka nchi za Afrika kufungua uchumi wao, pamoja na ukweli kwamba katika nchi hizi nyingi kuna utawala wa sheria kidogo sana," anasema Anuradha Mittal, mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya Oakland, ambapo katika miaka ya karibuni imefanya utafiti kuhusu mipango mipya 70 ya ardhi barani Afrika.

Karibu mipango yote hii, anasema, inagubikwa na kukosekana kwa uwazi na kushirikisha wazawa, ikiwa ni pamoja na kukosekana kwa faida nyingi zilizoahidiwa kwa ajili ya uchumi wa ndani na wa kitaifa – ajira, ukuaji wa pato la ndani, ujenzi mpya wa kliniki au vyanzo vya maji kwa wanajamii.

"Pia kumekuwepo na imani potofu nyingi kuhusu wawekezaji ni akina nani," anasema. "Siyo Wachina tu au Wahindi au mataifa ya Ghuba. Idadi ya wawekezaji kutoka Ulaya na Marekani ni kubwa, ikiwa ni pamoja na makampuni binafsi ambayo yanapatiwa fedha kubwa, wote wakitaka kupata fursa ya kuzalisha bidhaa za bei nafuu."

Maendeleo kwa ajili ya nani?

Hata hivyo, hali imebadilika katika miaka ya karibuni, kwani walaji wamezidi kutambua masuala ya ajira na mazingira duniani.

"Inabidi kampuni kuuza bidhaa zake mahali fulani, na mbinu hizi zinapingana moja kwa moja na wazalishaji na wanunuzi – makampuni ya Kraft, Nestle, Unilever –yanataka viwango vya juu zaidi vya mafuta ya mawese kwa ajili ya kuuza," Skar wa Greenpeace anasema. "Herakles inashindwa katika suala hili na inabidi kujibu wabia wake ni kwa nini kufanya hivyo."

Kwa wanaharakati wengi, suala linakuja juu ya aina ya maendeleo ambayo jumuiya ya kimataifa inajaribu kushinikiza.

"Leo hii shinikizo kubwa ni kuondokana na mamilioni ya wakulima wadogo nchini Cameroon, kuwabadili kuwa vibarua wa ujira mdogo katika mashamba makubwa," Mousseau wa Greenpeace anasema.

"Katika mijadala ya maendeleo ya sasa tunaambiwa suala hili ni muhimu, na tunatoa misamaha ya kisheria na kifedha kwa wawekezaji. Lakini hatuoni matokeo yoyote yale ya kimaendeleo kutoka kwa wawekezaji hawa – tunachokiona ni unyonyaji wa binadamu na rasilimali za nchi. (END/2012)

 

 
 Latest News from Africa
News in RSS
XML error: The element 'html' is used but not declared in the DTD/Schema.
  Dernières Nouvelles
News in RSS
DEVELOPPEMENT: Nous devons penser autrement à la "sécurité"
AUSTRALIE: Le port de Newcastle bloqué par les Guerriers du changement climatique
IRAN: L’examen d’un document clé à l’AIEA suggère un coup d’Israël
PAKISTAN: Les Ahmadis confrontés à la mort ou à l’exil
ETATS-UNIS: Le budget de la défense peut accroître alors que le public est fatigué de la guerre
A lire également>>