Inter Press Service News Agency
Tuesday, June 19, 2018   21:24 GMT    
   Homepage
   World Service
   East Africa
   Southern Africa
   West Africa
   Central Africa
 
   Environment
   Health-HIV/AIDS
   Education
   Rights
   Politics
   Economics
   and Finance
   Development
   Energy
   Population
   Culture
 
   Radio Service
 
   Français
 
   About IPS
 
   ENGLISH
   ESPAÑOL
   FRANÇAIS
   ARABIC
   DEUTSCH
   ITALIANO
   NEDERLANDS
   PORTUGUÊS
   SUOMI
   SVENSKA
   SWAHILI
   TÜRKÇE
PrintSend to a friend
Readers Opinions


Wanawake wa Mauritania Wageukia Ufugaji wa Kuku Kupambana na Umaskini
Na Mohamed Abderrahmane

NOUAKCHOTT, Oktoba 10 (IPS) - Kwa sasa jengo limesimama likiwa tupu, lakini Fatimetou Mint M’Barkenni anaangalia ni lini litajaa tena vifaranga wa kuku. Mapema mwaka huu, alifuga kundi la kwanza la kuku wa nyama kama mradi wa majaribio, kuwezesha kuongeza kipato chake na usalama wa chakula katika eneo la Bourate, kijijini mwa Mauritania.

"Vifaranga wa kwanza niliofuga niliwauza mwezi Juni, na nasubiri kampuni ya PROLPRAF kuleta vifaranga wengine wa kundi la pili – kuna mahitaji makubwa mno," alisema M’Barkenni mwenye umri wa miaka 53.

PROLPRAF, mradi wa kuongeza thamani ya mazao na kupunguza umaskini, ni mradi wa pamoja wa serikali ya Mauritania na Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD), wenye lengo la kukuza na kuimarisha usalama wa chakula wakati huo huo ukikuza uzalishaji wa ndani wa mazao saba ya chakula –mboga mboga, dengu, maziwa, ngozi na kwato, nyama nyekundu na mazao ya msituni na kuku.

"Kitengo cha Uzalishaji wa Kuku wa Nyama ni Baraka kwetu sisi, hasa wakati wa kipindi hiki cha ukame mkubwa wakati kuna matatizo makubwa ya utapiamlo," M’Barkenni aliiambia IPS.

"Mpango huu ni muhimu kwa wanawake, kutokana na kuwa wanaume wamekwenda kutafuta kazi katika miji mikubwa, kama vile Nouakchott na Nouadhibou," aliongeza.

Mariem Mint Sidi ni meneja wa mtambo wa kuzalishia vifaranga vya kuku wa pili wa Foum Gleita, kusini mashariki mwa nchi. Anajivunia kile ambacho tayari amejifunza juu ya kulisha na kutunza vifaranga. Pia anapendezwa na bei nafuu ya kuku. "Mmoja anaweza kununua kilo 2.4 za kuku wa nyama wenye afya, nyama wenye lishe kwa dola sita."

Mwezi Juni, vitengo viwii vya kuku katika Bourate na Foum Gleita kila kimoja kimepokea vifaranga 1,600 wa kuku walioagizwa kutoka nchi jirani ya Morocco, alielezea Ahmed Ould Sidina, msaidizi wa PROLPRAF anayehusika na uzalishaji wa mifugo. Aina ya kuku wa nyama wanaokua kwa haraka wanaofaa kwa biashara wanapendwa kwa ajili ya mradi huo; aina ya kuku wanaojulikana kama Cobb500 ambao walitoka nchini Marekani wana uwezo wa kustawi hata kwa kupewa chakula cha ubora mdogo.

"Vifaranga hao wana uwezo wa kukua vizuri katika maeneo ya joto kali (nyuzi 40 katika kivuli) na ni vifaranga 34 tu waliweza kufa kati ya 1,600," alisema Ahmed Ould Brahim Khlil, mtaalam wa mifugo kutoka PROLPRAF.

Aliiambia IPS kuwa vifaranga walikuwa wamepatiwa chanjo dhidi ya ugonjwa wa Gumboro na Newcastle, magonjwa mawili yanayoshambulia zaidi kuku nchini Mauritania, na mameneja walikuwa wamepewa mafunzo ya jinsi ya kusafisha vifaranga na kuwapatia dozi ya vitamini.

Kila kitengo kinagharimu dola zipatazo 10,000 kukijenga, ikiwa ni pamoja na ujenzi wa jengo la mabati, ununuzi wa vifaranga na chakula, na ufungaji wa mabeseni ya maji na chakula, vifaa vya uingizaji wa joto, taa za sola na majokofu.

Mint Sidi na M’Barkenni ni wafanyakazi wa kujitolea ambao hawalipwi na mradi, ambao bado uko katika awamu ya majaribio.

Kipato kutokana na mradi wa majaribio kimeuwezesha mradi kujenga mtaji wa uendeshaji wa dola 3,500 ambao utatumika kununulia vifaranga wapya na chakula. Oda nyingine ya vifaranga 2,000 inatarajiwa kutolewa katikati mwa Agosti, alisema Brahim Khlil.

"Ufugaji wa kuku katika maeneo yenye umaskini mkubwa una malengo ya kuhakikisha uzalishaji endelevu na kuongeza shughuli za uingizaji wa kipato na kujenga ajira," alielezea Mohamed Ould Abdallahi, mratibu wa PROLPRAF.

Abdallahi anasema kuwa kutokana na msaada wa dola milioni 4.17 kutoka kwa IFAD, PROLPRAF ina lengo la kupunguza upoteaji wa fedha kwa kuhakikisha uagizaji wa mazao kutoka nje nafasi yake inachukuliwa na bidhaa za ndani. Mpango huo una lengo kuu la kuimarisha hali ya maisha na vipato kwa wanawake na vijana kwa ujumla.

Kwa mujibu wa wizara ya maendeleo ya vijijini, wananchi wa Mauritania wanakula wastani wa tani 11,000 za kuku kwa mwaka, wastani wa kilo tatu hadi nne kwa kila mtu.

Mahitaji ya kuku nchini Mauritania kwa sehemu yanatokana na uzalishaji wa ndani, lakini kuku wengi wanaingizwa kutoka nje, wakiwa katika hali barafu. Kuku wanaofikia tani 5,000 na vifaranga wapatao 40,000 wenye umri wa siku moja wanaingia nchini kila mwaka. Vile vile, ni theluthi moja tu ya mayai yanayoliwa kwa mwaka nchini Mauritania yapatayo milioni tano yanazalishwa nchini.

Gharama za uagizaji wa mayai, kuku wa barafu, vifaranga na chakula, vifaa na masuala mengine kunakadiriwa kufikia dola milioni 18 kwa mwaka, kwa mujibu wa Moktar Fall, mshauri wa mifugo katika wizara ya maendeleo ya vijijini.

Abdallahi Ould Nabgha, rais wa chama cha taifa cha wafugaji wa kuku Mauritania, alisema kuna mashamba 60 ya kuku yanayozunguka mji wa Nouakchott kusini magharibi, Nouadhibou huko magharibi, na Rosso na Sélibaby upande wa kusini.

"Sekta ya kuku inaajiri watu 10,000, bila hata kuhesabu faida inayopatikana kutokana na sekta hiyo, kama vile mbolea inayotumika au manyoya ambayo yanatumika kutengenezea vifutio vya kompyuta," alisema Nabgha.

Alikosoa nchi kutokana na kukosa miundombinu, ambako kunasababisha kuingiza vifaranga, chakula na vifaa kwa ajili ya ufugaji wa kuku.

Ili kukabiliana na uhaba huu, serikali ilisaini mkataba na wafanyabiashara wa ndani Julai 22 kwa ajili ya ujenzi wa jengo la kuku mjini Nouakchott, mji mkuu wa nchi kwa gharama ya dola milioni 34.

Litakapokamilika katika miezi 18 ijayo, jengo hili litatumika kama kitengo cha uzalishaji wa vifaranga wa siku moja na kuku wa nyama kwa uwezo wa tani 20,000 kwa mwaka, ikiwa ni pamoja na kuzalisha mayai milioni 15 na tani 120,000 za chakula cha kuku kwa mwaka, Yahya Ould Abdeldayem, mkurugenzi wa uwekezaji katika wizara ya afya, aliiambia IPS. (END/2012)

 

 
 Latest News from Africa
News in RSS
XML error: The element 'html' is used but not declared in the DTD/Schema.
  Dernières Nouvelles
News in RSS
DEVELOPPEMENT: Nous devons penser autrement à la "sécurité"
AUSTRALIE: Le port de Newcastle bloqué par les Guerriers du changement climatique
IRAN: L’examen d’un document clé à l’AIEA suggère un coup d’Israël
PAKISTAN: Les Ahmadis confrontés à la mort ou à l’exil
ETATS-UNIS: Le budget de la défense peut accroître alors que le public est fatigué de la guerre
A lire également>>