Inter Press Service News Agency
Tuesday, June 19, 2018   21:24 GMT    
   Homepage
   World Service
   East Africa
   Southern Africa
   West Africa
   Central Africa
 
   Environment
   Health-HIV/AIDS
   Education
   Rights
   Politics
   Economics
   and Finance
   Development
   Energy
   Population
   Culture
 
   Radio Service
 
   Français
 
   About IPS
 
   ENGLISH
   ESPAÑOL
   FRANÇAIS
   ARABIC
   DEUTSCH
   ITALIANO
   NEDERLANDS
   PORTUGUÊS
   SUOMI
   SVENSKA
   SWAHILI
   TÜRKÇE
PrintSend to a friend
Readers Opinions


Kuishi kwa Mlo Mmoja kwa Siku Katika Ukanda wa Savana Nchini Ghana
Albert Oppong-Ansah

TAMALE, Ghana, Oktoba 9 (IPS) - Ili kuhakikisha kuwa yeye na familia yake wanaishi katika hali ya kukosa mavuno mwaka huu, Adams Seidu, kama ilivyo kwa wakulima wengine katika maeneo ya kijijini katika Mkoa wa Kaskazini mwa Ghana, ameamua kutekeleza mkakati wa kuishi. Anatumia kitu ambacho Seidu anakiita "mkakati wa moja-sifuri-moja" kwa watoto, na "mkakati wa sifuri-sifuri" kwa watu wazima.

Mikakati hiyo inawakilisha milo mitatu kwa siku. Moja inawakilisha mlo, wakati sifuri inawakilisha kukosekana kwa mlo. Hivyo watoto wanne wa Seidu wanaweza kuwa na kifungua kinywa wakati wa asubuhi, wasile chochote katikati mwa siku,halafu kuwa na mlo mmoja wakati wa usiku, wakati yeye na mke wake wanakula mlo mmoja tu kwa siku, wakati wa jioni – kama ilivyo kwa familia nyingi katika taifa hili la Afrika magharibi.

Uhaba wa chakula unazidi kuwa suala gumu katika mkoa. Utafiti uliofanywa juu ya lishe mwezi Machi na Taasisi ya Utafiti wa Afya Ghana ulionyesha kuwa asilimia 32.2 ya watoto 208,742 wenye umri wa chini ya miaka mitano katika Mkoa wa Kaskazini walikuwa na upungufu wa lishe bora na hivyo kudumaa kukua.

Familia ya Seidu inaendelea kusihi, lakini kwa shida sana.

Hii ni kutokana na Seidu, ambaye anaishi huko Fuo, kitongoji katika mji mkuu wa Mkoa wa Kaskazini wa Tamale, amekuwa hapati mavuno mazuri kwa miaka kadhaa ya karibuni.

Majimbo ya Kaskazini, Upper West na Upper East nchini Ghana yaliwahi kuwa chanzo kikuu cha mazao ya chakula aina ya nafaka na mizizi. Lakini mabadiliko ya hali ya hewa katika mikoa hii, ambayo yanapatikana katika ukanda wa Savana wa Gahana, yamesababisha kuwepo kwa mvua haba, mavuno machache na hatimaye kukosekana kwa usalama wa chakula.

"Msimu wa kilimo uliopita ulikuwa mbaya zaidi na ulishuhudia wakulima wengi wakipoteza mazao yao kutokana na mvua haba, ambazo zilisababisha mazao kunyauka kabla hayajakomaa," Seidu, ambaye ana shamba dogo la mahindi, mpunga na viazi vikuu aliiambia IPS.

Wakati wa msimu wa mvua wa mwaka 2000, wilaya ya kaskazini ya Nanumba katika Mkoa wa kaskazini ilirikodi wastani wa milimita 1,495 za mvua. Lakini mwaka 2010 katika kipindi kama hicho eneo hilo lilirikodi milimita 433 tu.

Kupungua kwa mvua kuliathiri kwa kiasi kikubwa mkoa huu. Kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya Taifa ya mwaka 2010, Mkoa wa Kaskazini ni wa tatu kwa kuwa na wakazi wengi nchini Ghana, ambapo asilimia ipatayo 80 ya watu hao wanajishughulisha na kilimo. Kwa sasa, nusu ya wakulima wa mkoa huo wanapata shida kuendesha maisha yao kwani mazao yao yanazidi kushindwa, kwa mujibu wa Taasisi ya Takwimu ya Ghana.

Kati ya ekari mbili za ardhi ambazo Seidu amelima mwaka huu, alivuna magunia matatu tu yenye ujazo wa kilo 84. "Miaka miwili iliyopita nilivuna magunia saba katika ardhi hiyo hiyo. Baadhi ya mimea haikutoa maua, achana na kushindwa kwake kutoa matunda mwaka huu," alisema mkulima, ambaye ni kilema mwenye mkono mmoja tu.

Takwimu za Ofisi ya Mkoa wa Kaskazini za Wizara ya Chakula na Kilimo zinaonyesha kuwa uzalishaji wa mahindi katika mkoa ulishuka kutoka tani 164,200 mwaka 1991 hadi chini ya nusu, tani 78,800 mwaka 2000. Hakuna takwimu za karibuni zinazoonyesha hali ya sasa.

Ofisa mwandamizi wa hali ya hewa wa mkoa katika Taasisi ya Hali ya Hewa ya Ghana, Kafui Quashiga, aliiambia IPS kuwa mvua imepungua kwa kiasi kikubwa kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa yaliyojitokeza katika kipindi cha miaka 10 iliyopita. Takwimu zilizoandaliwa na shirika zinaonyesha kuwa kumekuwepo na kupungua kwa muda mrefu kwa wastani wa mvua wa milimita 6,550, ambayo ilikuwa mvua ya wastani mwanzoni mwa miaka ya 2000.

"Unapolinganisha takwimu za mvua kuanzia mwaka 1991 hadi 2010 kwa eneo la Wa katika mkoa wa Upper West, eneo la Tamale huko kaskazini, eneo la Navorongo katika mkoa wa Upper East na eneo la Krachie katika mkoa wa Volta, kuna kupungua kwa kasi kwa kiwango cha mvua na kuna uwezekano wa kuzidi kushuka," alisema.

Umaskini, kutokujua kusoma na kuandika, magonjwa na utapiamlo kwa sasa yamekuwa matatizo ya kawaida katika mikoa hiyo.

Seidu alikubali kuwa kutokana na mavuno haya duni hakuweza hata kulipia ada ya shule kwa watoto wake wawili. "Kutokana na mavuno duni ambayo tumepata katika miaka ya karibuni, sasa naweza kupeleka shule watoto wawili tu kati ya wanne."

Mkulima mwingine, Nindoo Salisu mweye umri wa miaka 60, aliiambia IPS kuwa watoto watatu tu kati ya 10 ana uwezo wa kuwapeleka shule. "Tuliweza kupata mazao ya kutosha hadi hali ya hewa ilipoamua kutuangusha na kutufanya kuwa maskini."

"Hali hii ni mbaya sana, na jitihada za mapema zitasaidia kwani hali hii ina madhara hasi mno kwetu sisi kama binadamu," Quashiga alisema.

Na wakati kuna baadhi ya miradi ya kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa katika mkoa huo, bado haijaonyesha kuwa na mafanikio.

Abubakar Sadique Haruna, mkulima katika Mkoa wa Kasakzini nchini Ghana, anakodisha trekta lake kwa ajili ya kulimia kwa wakulima wadogo wadogo wa eneo lake.

Kwa msaada wa Mpango wa Maendeleo ya Kilimo na Kuongeza Thamani ya Mazao (ADVANCE), Haruna anatoa huduma kwa wakulima wapatao 400.

ADVANCE, mpango unaofadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Kimataifa, ulianza kufanya kazi mwaka jana. Kupitia mpango huo wakulima wapatao 1,000 wamepatiwa msaada wa huduma za kulimia, na walipatiwa elimu ya jinsi ya kutumia mbegu zilizoboreshwa, teknolojia mpya na mbinu bora za kilimo.

Haruna alielezea kuwa katika kila ekari moja inayolimwa kwa trekta, wakulima aidha walimpatia dola nne – sawa na lita 4.5 za mafuta – au kumpatia mfuko wa kilo 84 za mahindi mwishoni mwa msimu wa kilimo.

Mbali na huduma hizi za kulimia, Haruna anawapatia wakulima mbegu bora zilizoboreshwa kemikali za kilimo na mbolea za viwandani. Pia anawapatia wakulima elimu ya mbinu bora za kilimo ili kuongeza mazao yao.

"Jambo la bahati mbaya ni kwamba baadhi ya wakulima, baada ya kulipa kutokana na kulimiwa, wanashindwa kumudu kemikali hizi za kilimo (kutokana na kupata mavuno haba),"aliiambia IPS.

Haruna alisema kuwa mwaka 2011 haukuwa mwaka wa mafanikio kwa wakulima, kwani wateja wake wapatao 200 walishindwa kumudu gharama za kulima tena mashamba yao.

Ofisa wa ufuatiliaji wa Wizara ya Chakula na Kilimo, Festus Aaron Langkuu, aliiambia IPS kuwa njia mpya za uvunaji maji zinafanyiwa majaribio katika baadhi ya maeneo.

Alisema kuwa mabwawa ya Golinga na Bontanga katika Mkoa wa Kaskaizni mwa nchi, ambayo yalikuwa yakikarabatiwa chini ya Mradi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Milenia wa mwaka 2010, yalikuwa yakiwapatia baadhi ya wakulima maji kwa ajili ya mazao yao.

"Pamoja na kuwa serikali inasaidia baadhi ya wakulima kuwapatia mbolea, suala la msingi ni kwamba kama hakuna mvua, wakulima hawa hawataweza kupanda mazao yao, na hili litarejesha nyuma lengo la kupunguza umaskini," Langkuu alisema. (END/2012)

 

 
 Latest News from Africa
News in RSS
XML error: The element 'html' is used but not declared in the DTD/Schema.
  Dernières Nouvelles
News in RSS
DEVELOPPEMENT: Nous devons penser autrement à la "sécurité"
AUSTRALIE: Le port de Newcastle bloqué par les Guerriers du changement climatique
IRAN: L’examen d’un document clé à l’AIEA suggère un coup d’Israël
PAKISTAN: Les Ahmadis confrontés à la mort ou à l’exil
ETATS-UNIS: Le budget de la défense peut accroître alors que le public est fatigué de la guerre
A lire également>>