Inter Press Service News Agency
Tuesday, June 19, 2018   21:25 GMT    
   Homepage
   World Service
   East Africa
   Southern Africa
   West Africa
   Central Africa
 
   Environment
   Health-HIV/AIDS
   Education
   Rights
   Politics
   Economics
   and Finance
   Development
   Energy
   Population
   Culture
 
   Radio Service
 
   Français
 
   About IPS
 
   ENGLISH
   ESPAÑOL
   FRANÇAIS
   ARABIC
   DEUTSCH
   ITALIANO
   NEDERLANDS
   PORTUGUÊS
   SUOMI
   SVENSKA
   SWAHILI
   TÜRKÇE
PrintSend to a friend
Readers Opinions


Magonjwa ya Mimea Yatishia Usalama wa Chakula huko Kivu, DRC Kongo
Na Baudry Aluma

BUKAVU, DR Kongo, Oktoba 9 (IPS) - Magonjwa ya mimea yanayoathiri ndizi na mihogo yanazidi kuenea katika majimbo mawili mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, kwa mujibu wa waziri wa kilimo wa jimbo la Kivu ya Kusini, Gisèle Batembo.

Kiwango cha uharibifu kinaonekana katika jimbo zima: ugonjwa wa kunyauka majani unatokana na bakteria wanaoshambulia ndizi wakati mashamba mengi ya muhogo yamejawa na kudumaa kwa mime na hivyo kuwa na mihogo iliyojikunja ikiwa ni pamoja na majani yaliyokunjamana, dalili ya ugonjwa unaosababishwa na virusi.

Kupungua kwa uzalishaji kumesababisha kuongezeka kwa uingizaji wa mazao haya toka nchi jirani ya Rwanda, ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa bei mwaka jana, huku bei ya mkungu wa ndizi (wenye kati ya kilo 30-50) ikiruka kutoka dola mbili hadi dola saba katika kipindi cha chini ya mwaka mmoja.

Familia laki tatu zinapanda ndizi katika Kivu ya Kusini, na zaidi ya kaya 900,000 zinapanda mihogo kwa ajili ya matumizi na kuzalisha kipato.

Akisisitiza umuhimu wa mazao hayo kwa usalama wa chakula, mtaalam wa uchumi wa kilimo Daniel Rutegeza, ambaye anaongoza Kitengo cha Uzalishaji wa Mimea katika kurugenzi ya kilimo ya jimbo, alisema jumla ya uzalishaji wa ndizi katika Kivu ya Kusini mwaka 2009 ilifikia tani 450,000, kutoka kwenye mashamba ya karibu hekta 100,000. Mazao ya mihogo katika hekta 325,000 zinazolimwa yanakadiriwa kuwa tani milioni nne.

Ili kukabiliana na tishio linaloongezeka la magonjwa, wakulima wadgo wadogo wanajifunza mbinu mpya za kupunguza madhara, Batembo aliwaambia washiriki katika warsha ya Agosti 6 mjini Katana, kaskazini mwa mji mkuu wa jimbo la Kivu ya Kusini wa Bukavu. Warsha hiyo iliandaliwa kwa malengo mawili ya kuongeza ufahamu na kutafuta ufumbuzi wa kuenea kwa kasi kwa magonjwa yanayoathiri mazao makuu ya chakula katika jimbo.

Katika mkutano wa waandishi wa habari mwezi Juni, gavana wa jimbo la Kivu ya Kusini, Marcellin Cishambo, alithibitisha kuongezeka kwa madhara ya magonjwa kwa wakulima. "Ugonjwa wa kunyauka kwa migomba umeingia Kalehe, kaskazini mwa Bukavu, na unaenea kwa kasi kubwa. Ugonjwa huu unatishia mashamba ya ndizi katika maeneo manne kati ya nane ya kiutawala katika jimbo," alisema.

"Eneo la Kalehe limeathirika zaidi, huku karibu nusu ya mashamba yakiharibiwa. Katika Kabare – katika eneo la kaskazini – kiwango cha asilimia 25, wakati eneo la Idjwi lina kiwango cha kati ya asilimia 10 na 25, na Walungu lina wastani wa kati ya asilimia 10 na 20," Cishambo alisema.

Batembo alitoa tahadhari mapema mwezi mmoja kabla, katika ripoti yake ya mwezi Mei katika nusu ya kwanza ya mwaka 2012. Magonjwa ya kunyauka kwa migomba na virusi vya mihogo yanaaminika kuingia katika majimbo ya Kivu kutoka nchi jirani ya Uganda, ambako wakulima wamekuwa wakijitahidi kukabiliana na magonjwa hayo kwa miaka kadhaa.

Dalili za magonjwa ya bakteria ni pamoja na migomba ya ndizi kunyauka majani yake na ndizi zenyewe kugeuka kuwa njano kabla ya kukomaa, kwa mujibu wa Profesa Jean Walangululu, mkuu wa Kitengo cha Sayansi ya Kilimo katika Chuo Kikuu cha Katoliki cha Bukavu.

Mazao ya mihogo katika jimbo, profesa aliiambia IPS, yanashambuliwa na Virusi Vinavyoshambulia Mihogo vya Afrika Mashariki vinavyojulikana kama Mosaic Virus, ambavyo huenezwa na inzi weupe aina ya Bemisia, ambao ni wagumu mno kuwadhibiti. Mazao yaliyoathirika yanadumaa na majani kujikunja, na kudumaa kukua na kuwa na mavuno duni.

Ugonjwa huo pia unaweza kuenezwa kwa kupanda mihogo iliyoathirika na ugonjwa. Rutegeza alisema ubadilishanaji wa mbegu kati ya wakulima wadogo ni moja ya sababu kuu za kuenea kwa ugonjwa wa mihogo na ndizi.

Ugonjwa haujaacha kuathiri eneo lolote lile la jimbo, Cishambo alisema. Alisema ugonjwa ulionekana kwa mara ya kwanza katika jimbo mwaka 2000, na jitihada kali zimechukuliwa kupambana na ugonjwa huo, hasa kwa kusisitiza umuhimu wa kutumia mbegu za mihogo mpya na ambazo zinatokana na mimea isiyoathirika na ugonjwa.

Lakini, kwa mujibu wa Cishambo, hii haijazuia uharibifu kuongezeka kwa kasi kubwa, hadi katika hali ambapo inatishia usalama wa chakula katika jimbo zima.

Gavana wa Kivu ya Kusini ametoa kanuni kumi za kukabiliana na kuenea kwa magonjwa hayo, jambo muhimu zaidi likiwa ni kupiga marufuku kusambazwa au kuingizwa kwa mbegu za mihogo au ndizi katika Kivu ya Kusini kutoka nchi jirani za Rwanda au Uganda, au Kivu ya Kaskazini, ambayo pia inakabiliwa na matatizo kama hayo.

Biashara na usafirishaji wa mbegu hizo unaruhusiwa tu kama utaambatana na cheti cha Mkaguzi wa Kilimo kinachoonyesha kuwa mbegu hizo ni salama na ambacho hutolewa na Taasisi ya Kuthibitisha Ubora wa Mbegu (SENASEM).

Wataalam katika taasisi ya SENASEM walipendekeza matumizi ya moto au dawa kuondoa maambukizi katika mihogo inapotolewa kutoka ardhini. Pia wanashauri jitihada kubwa za kuzuia wanyama wasizurule katika mashamba ya ndizi, na kuhakikisha kuwa uuzaji wowote ule au ubadilishanaji wa mbegu za mihogo na ndizi unafanywa na wataalam waliothibitishwa na SENASEM na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo.

FAO inajaribu kufanyia majaribio mbinu mpya za kukabiliana na ugonjwa wa kunyauka kwa ndizi ambazo tayari zimeshatumika nchini Uganda. Kwa mujibu wa Rutegeza, tiba hii inahusu wakulima kungo’a miche ya migomba ya kiume katika mashina ya ndizi kila baada ya siku mbili. Mwezi Aprili, baadhi ya wakulima 150 wa ndizi katika Bweremana, katika eneo la Masisi Kaskazini mwa Kivu, walipatiwa mafunzo juu ya suala hili, alisema.

Mike Robson, mtaalam wa magonjwa ya mimea katika shirika la FAO ambaye aliwezesha ubadilishanaji wa kiufundi kati ya Uganda na DRC, alisema kuwa matokeo ya kwanza kutoka katika majaribio haya yanatarajiwa mwezi Oktoba 2012, kabla ya kuingizwa kwake katika Kivu ya Kusini.

Nzanzu Kasuvita, waziri wa klilimo wa jimbo la Kivu ya Kaskazini, alitambua kuwa bado kuna kazi kubwa kufanyika, hasa katika kuelimisha wahusika wote na washirika katika jitihada za kuleta usalama wa chakula.

Hata hivyo, vita kati ya jeshi la DRC na askari wa kikundi cha waasi cha Mouvement du 23 Mars (M23), ambayo imeathiri baadhi ya maeneo ya Kaskazini mwa Kivu kati ya Aprili, inahatarisha kuzuia utatuzi wa tatizo la magonjwa ya mimea ambayo yanaweza kutishia usalama wa chakula, alisema. (END/2012)

 

 
 Latest News from Africa
News in RSS
XML error: The element 'html' is used but not declared in the DTD/Schema.
  Dernières Nouvelles
News in RSS
DEVELOPPEMENT: Nous devons penser autrement à la "sécurité"
AUSTRALIE: Le port de Newcastle bloqué par les Guerriers du changement climatique
IRAN: L’examen d’un document clé à l’AIEA suggère un coup d’Israël
PAKISTAN: Les Ahmadis confrontés à la mort ou à l’exil
ETATS-UNIS: Le budget de la défense peut accroître alors que le public est fatigué de la guerre
A lire également>>