Inter Press Service News Agency
Thursday, February 22, 2018   05:12 GMT    
   Homepage
   World Service
   East Africa
   Southern Africa
   West Africa
   Central Africa
 
   Environment
   Health-HIV/AIDS
   Education
   Rights
   Politics
   Economics
   and Finance
   Development
   Energy
   Population
   Culture
 
   Radio Service
 
   Français
 
   About IPS
 
   ENGLISH
   ESPAÑOL
   FRANÇAIS
   ARABIC
   DEUTSCH
   ITALIANO
   NEDERLANDS
   PORTUGUÊS
   SUOMI
   SVENSKA
   SWAHILI
   TÜRKÇE
PrintSend to a friend
Readers Opinions


Wakulima wa DRC Wavuna Faida za Udongo Wenye Rutuba
Na Baudry Aluma

BUKAVU, RD Congo, Oktoba 9 (IPS) - Miaka miwli iliyopita, wakulima wa mpunga katika bonde la Ruzizi mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo walivuna tani 2.5 za mpunga kwa kila hekta moja. Matumizi ya mbinu mpya za kilimo yamesababisha mavuno yao kuongezeka kati ya tani sita na nane, huku wakulima wadogo wadogo pia wakiongeza mazao yao katika soko la ndani.

Nyuma ya mageuzi haya, kilomita 100 kusini mwa Bukavu, mji mkuu wa Jimbo la Kivu ya Kusini, kuna mpango wa CATALIST unaoendeshwa na IFDC (Kituo cha Kimataifa la Kutengeneza Mbolea au - International Fertiliser Development Centre), NGO ya Kiholanzi iliyoanza mafunzo kwa wakulima ya kuhifadhi ubora wa ardhi mwaka 2007.

CATALIST – ambayo kwa lugha ya kigeni inasimama kama Catalyse Accelerated Agricultural Intensification for Social and Environmental Stability – inakuza mbinu kadhaa zinazojulikana kama Muunganiko wa Usimamizi wa Ardhi yenye Rutuba. ISFM ni ufumbuzi endelevu wa usalama wa chakula na kuleta kipato kikubwa, kwa mjibu wa Bernard Assumani, mkaguzi wa kilimo wa jimbo. Hapo nyuma, alisema, wakulima walikuwa wakivuna tani 2.5 za mpunga kutoka katika eneo la hekta moja; lakini kutokana na kutumia ISFM, eneo kama hilo linaweza kutoa mavuno ya hadi tani 7.5.

Wakulima wadogo wadogo waliozungumza na IPS walithibitisha kuwa mpango huo una faida kwao. "Mavuno yanatofautiana kati ya tani sita hadi nane kwa hekta," alisema Louise Zawadi, mjumbe wa Chama cha Wakulima Wanawake kwa Maendeleo Vijijini (AFEDER). "Kutokana na mpunga kuuzwa kwa senti 80 za dola za Marekani kwa kilo, faida inakuwa kubwa."

Mavuno makubwa, kuongezeka kwa soko

IFDC imetumia miaka miwili ikifanya kazi pamoja na vyama vya ndani nane na vyuo vikuu viwili huko Bukavu katika kuanza mpango wao wa kuongeza uzalishaji wa mpunga katika bonde la Ruzizi.

Jambo la msingi katika mbinu za ISFM ni kutumia mbolea za viwandani, ambayo inaagizwa mashariki mwa DRC kutoka Tanzania. Hatua mbili zilianzishwa mwaka 2010 kuwezesha mbolea kupatikana kiurahisi: serikali ilikubali kuondoa ushuru wa forodha katika mbolea inayoingizwa wakati huo huo IFDC ikitoa ruzuku ya gharama za usambazaji. Jambo hili lilipunguza gharama ya mbolea hadi kufikia dola 1.80 kwa kilo moja.

Ruzuku hiyo imeshaondolewa, lakini inaonekana kufikia malengo yake, kwani kwa sasa mbolea hiyo inapatikana kiurahisi katika ukanda huo kwa bei ya dola 1.25 kwa kilo. Herman Mutabataba, ambaye anaratibu chama cha wasambazaji wa mazao ya vyakula na mbegu, anabainisha kuwa mbolea bado ina bei ya juu katika bonde la Ruzizi ikilinganishwa na katika eneo la mpakani na Tanzania na Rwanda, ambako wakulima wana uungwaji mkono mkubwa kutoka serikalini.

Baadhi ya wakulima wameanzisha vyama ili kuunganisha jitihada zao. Moja ya chama cha wakulima wadogo, ambacho kina nguvu na kuwa na wanachama 315, kilivuna tani 86 za mpunga – wenye thamani ya dola 17,200 – katika eneo la Luberizi katika msimu wa kwanza wa kilimo wa mwaka 2011, kwa mujibu wa mwanachama wa chama hicho Mukeba wa Rusatiza. Kwa kuongeza katika faida hizi, wazalishaji pia waliingiza mbegu za ubora wa juu.

Mpunga unaozalishwa ndani ya nchi unazidi kupata soko ambalo hapo kabla lilijaa mpunga kutoka Tanzania na Pakistan. Kiasi kikubwa cha mpunga kinaingizwa katika soko na katika eneo la Bukavu na Uvira, miji mikubwa zaidi katika jimbo. Wakulima wengine kwa sasa wanauzia kiwanda cha bia cha pekee katika jimbo hilo.

Kiwanda cha bia cha Bralima, ambacho kinamilikiwa na kampuni ya kimataifa ya bia ya Heineken, ni mshiriki muhimu katika kukuza uzalishaji wa mpunga. Mwaka 2010, kiwanda chake cha Bukavu kiliingiza zaidi ya asilimia 60 ya tani za mpunga 2,800 ambazo ilitumia kwa kuzalisha bia. Lakini Bralima ilijitolea kutumia mpunga wa ndani tu, na katika kipindi cha mwaka mmoja ilikuwa imeacha kuagiza mpunga kutoka nje na kununua mpunga wa ndani – ikiwa ni pamoja na kusaini mkataba wa kununua tani 350 za mpunga kwa mwaka kutoka kwa shirika la wakulima wadogo wadogo.

Upatikanaji wa ardhi Baraza la Kikanda la Mashirika Yasiyokuwa ya Kiserikali (CRONGD) limechukua uongozi katika kuendesha mradi huo. Delphin Zozo ambaye ni mkuu wa CRONGD anabainisha kuwa wakati mradi ulipaonza, zaidi ya nusu ya wakulima walishiriki katika kulima mpunga katika mashamba madogo madogo, ambayo mara nyingi waliyakodisha wakati wa msimu wa kilimo.

Upatikanaji wa ardhi ni changamoto kwa wakulima wadogo. Mwanachama wa AFEDER Espérance Matumaini, kutoka Luvungi, kijiji katika bonde la Ruzizi, alilalamika kuwa ukodishaji wa ardhi unawagharimu sana.

"Inatugharimu dola 200 kukodisha hekta moja. Kama mtaamua kununua ardhi hiyo kutegemeana na ubora wa eneo lenyewe, mnaweza kulipia kati ya dola 400 hadi 600 kwa hekta," aliiambia IPS.

Jocelyn Matabaro, mtaalam wa ardhi na maliasili na mtaalam mshauri wa kujitegemea katika IFDC, anasema kuwa mpango wa CATALIST umefanya mabadiliko katika ardhi kuonekana waziwazi. Lakini, aliiambia IPS, wakati wakisubiri kubadilishwa kabisa kwa mfumo wa umilikaji wa ardhi nchini DRC, hatua za muda mfupi zinapaswa kutekelezwa katika ngazi ya ndani ili kuboresha mahusiano kati ya wakulima ambao wanakodisha ardhi kubwa na wamiliki wakubwa wa ardhi.

Wakulima wengi wadogo wadogo wamepata faida kutokana na mavuno mazuri katika ardhi walizonunua. Zozo alisema kuwa kati ya wakulima 15,000 katika bonde hilo, 12,500 wameanza kutumia mbinu za kilimo za IFDC. Na zaidi ya nusu ya wakulima hao wanaotumia ISFM wameshanunua mashamba yao kutokana na faida kubwa. Pia ukubwa wa mashamba umeongezeka, huku wakulima wengi wakipanua ukubwa wa mashamba yao hadi kufikia hekta tano.

Wakulima wadogo wadogo pia wamejifunza jinsi ya kugawa gharama zao za uzalishaji. Dieudonné Shukuru, mmoja wa wanachama 350 wa chama cha wakulima cha Organisation of Producers for Intensifying Agriculture and Development – katika eneo la Luvungi, alisema gharama kwa kila kilo moja ya mpunga ni kuanzia senti 20 hadi 45.

Kwa mujibu wa mwanauchumi wa kilimo wa CRONGD, Galilée Ibochwa, kwa ujumla kuna misimu miwili ya kilimo kwa mwaka, lakini alisisitiza matatizo ya uhaba wa maji katika baadhi ya maeneo. "Mabwawa mengi yamechakaa au hayajatunzwa vizuri. Katika maeneo haya, tuna msimu mmoja tu wa kilimo," aliiambia IPS.

Wakatri ISFM imeleta faida inayoonekana katika jimbo la Ruzizi, wakulima wanasema bado kuna vikwazo vya kukabiliana navyo: uhaba wa mashine bora za kuandaa mpunga, ikiwa ni pamoja na mbolea za ruzuku na msaada mwingine kutoka serikalini, ambayo ilitenga kiasi kidogo cha asilimia 0.6 ya bajeti ya taifa kwa ajili ya kilimo mwaka 2012. (END/2012)

 

 








 Latest News from Africa
News in RSS
XML error: The element 'html' is used but not declared in the DTD/Schema.
  Dernières Nouvelles
News in RSS
DEVELOPPEMENT: Nous devons penser autrement à la "sécurité"
AUSTRALIE: Le port de Newcastle bloqué par les Guerriers du changement climatique
IRAN: L’examen d’un document clé à l’AIEA suggère un coup d’Israël
PAKISTAN: Les Ahmadis confrontés à la mort ou à l’exil
ETATS-UNIS: Le budget de la défense peut accroître alors que le public est fatigué de la guerre
A lire également>>