Inter Press Service News Agency
Thursday, April 02, 2015   10:46 GMT    
   Homepage
   World Service
   East Africa
   Southern Africa
   West Africa
   Central Africa
 
   Environment
   Health-HIV/AIDS
   Education
   Rights
   Politics
   Economics
   and Finance
   Development
   Energy
   Population
   Culture
 
   Radio Service
 
   Français
 
   About IPS
 
   ENGLISH
   ESPAÑOL
   FRANÇAIS
   ARABIC
   DEUTSCH
   ITALIANO
   JAPANESE
   NEDERLANDS
   PORTUGUÊS
   SUOMI
   SVENSKA
   SWAHILI
   TÜRKÇE
PrintSend to a friend
Readers Opinions


Uzalishaji wa Nafaka kwa Ajili ya Watoto Wenye Upungufu wa Lishe Bora Nchini Mali
Soumaila T. Diarra

BAMAKO, Oktoba 9 (IPS) - Mtama umekuwa kitu muhimu katika unga wenye virutubisho katika jitihada za ndani na endelevu za kukabiliana na utapiamlo nchini Mali.

Katika jiji la Kati, baadhi ya kilomita 15 kutoka mji mkuu, Bamako, idadi ya wanawake wana kazi nyingi wakisindika nafaka hizo kuwa "Misola".

Mpango wa Misola, uliojengwa na chama cha Kifaransa chenye jina kama hilo, ni mradi wa afya ya umma ambao una lengo la kupunguza upungufu wa lishe bora miongoni mwa watoto wa umri mdogo.

"Tunanunua mtama, zao muhimu katika kuboresha unga wetu tunaozalisha, kutoka kwa wafanyabiashara wa nafaka katika jiji hapa," alisema Ramata Traoré, ambaye anaongoza mtambo wa uzalishaji wa Kati.

Unga umetengenezwa kwa mtama kwa asilimia 60, soya kwa asilimia 20, na karanga kwa asilimia 10. Vitamini na madini ya chumvi yanaongezwa katika unga huu ili kuwa na mlo kamili ambao unatumika kukomesha upungufu wa virutubisho mwilini.

Mahitaji ya unga yanazidi kuongezeka nchini Mali, kufuatia mavuno duni katika msimu uliopita. Utapiamlo ni tatizo kubwa katika nchi hii ya hali ya jangwa katika Afrika Magharibi, ambako usalama wa chakula umeathiriwa zaidi na ukame wa miaka ya karibuni – hali ambayo imezidishwa na uasi unaoendelea katika upande wa kaskazini.

Katika mwezi Desemba, Wizara ya Kilimo ilisema kuwa nchi imevuna zaidi ya milioni tano za nafaka, dhidi ya kiwango kilichokadiriwa cha tani milioni nane.

"Mgogoro wa chakula unaozidi kukua unaongeza hatari ya utapiamlo katika mikoa kadhaa ya Mali, ikiwa ni pamoja na Kayes (kusini magharibi), Koulikoro na Ségou (kusini)," alisema Aminata Sissoko, mtaalam wa lishe katika shirika la Msalaba Mwekundu Mali.

Aliongeza kuwa kuwekwa kwa mikoa mitatu ya kaskazini ya Kidal, Timbuktu na Gao chini ya makundi ya Kiislam na waasi kutoka kundi la National Movement for the Liberation of Azawad (MNLA) kumezidisha hali ya uhaba wa chakula.

"Kutokana na hali hiyo, hatujaweza kwenda katika maeneo yanayodhibitiwa na vikundi vya waasi kutathmini mahitaji. Lakini tunasaidia watu walioyakimbia makazi kutokana na vita kwa kuwapatia unga wa Misola," Sissoko aliiambia IPS.

Moja katika kila watoto watano wa Mali ana upungufu wa lishe bora mwilini, kwa mujibu wa Abdoulaye Sangho, mratibu wa tawi la Misola nchini Mali.

"Sisi ni NGO ambayo inasaidia wanawake wazalishaji wa unga wa Misola," Sangho aliiambia IPS. "Lengo letu ni kuboresha viwango vya lishe vya wakazi wote, kwa kulenga watoto wa kati ya umri wa miaka sita na miezi 60, na wanawake wajawazito na wanaonyonyesha."

Kituo cha uzalishaji wa Misola kilianzishwa mwaka 1993 katika eneo la Diafarabé, katika mkoa wa kati. Mpango huo ulikua kwa kasi, na leo hii kuna viwanda vidogo 19 vilivyoenea katika mikoa yote ya nchi isipokuwa Kidal, katika upande wa kaskazini.

Mradi unakwenda mbali hadi kuvuka mipaka ya nchi. Uzalishaji wa unga wenye virutubisho ulianza nchini Burkina Faso mwaka 1982, na unga huo wenye lishe sasa unatengenezwa nchini Senegal, Niger na Benin.

Nembo moja inaunganisha makampuni yanayotengeneza unga wa Misola. "Wanawake wanaofanya kazi katika kila mradi pia wanakuza njia bora za kutengeneza unga wa lishe kwa majirani zao. Wanaandaa mikutano ya maonesho katika vituo vya afya au katika maeneo mengine ya umma," alisema Sangho.

"Alipokuwa na umri wa miezi saba, mtoto wangu alikuwa mgonjwa sana na pia mkondefu. Lakini sikujua tatizo lilikuwa ni utapiamlo. Ni wakati wa maonesho ya Misola katika soko niliweza kujua tatizo hilo," alisema Assetou Traoré, muuza viungo vya chakula.

Kwa kuwafunza wanawake hawa kutengeneza unga huu – ambao unatumika kwa uji – ikiwa ni pamoja na kukuza matumizi yake katika jumuiya zao, chama cha Misola kinajenga uelewa mpana wa suala zima la lishe na uelewa wa jinsi ya kufikia jambo hili, kwa kujikita katika vifaa vya uzalishaji.

Katika eneo lililozungushiwa ua huko Kati, Traoré na wenzake wametandaza mtama ambao wameuosha kwa umakini mara kadhaa ili kuuanika juani katika maturubai. "Kutokana na kuwa tunachozalisha kinatakiwa kutumika kwa chakula cha watoto, tunakuwa makini sana na usafi," alisema Traoré, akielezea ni kwa nini hakuna anayeruhusiwa kuingia katika ghala akiwa amevaa viatu.

Chata Mariko, nesi katika kituo cha afya cha Bamako aliiambia IPS kuwa njia zinazopendekezwa kuzuia utapiamlo zinapatikana kiurahisi. "Paketi ya chakula hiki inagharimu siyo zaidi ya faranga za CFA 500 (kama dola moja). Lakini kwa bahati mbaya, kuna wazazi ambao hawataki kuwaleta watoto wao katika vituo vya afya kwa wakati unaotakiwa," alisema. (END/2012)

 

 
 Latest News from Africa
News in RSS
Lawyers, Rights Groups Rally Around Author of ‘Blood Diamonds’, Facing Jail
Former Military Man Declares Victory in Nigerian Polls
Activists Protest Denial of Condoms to Africa’s High-Risk Groups
Decent Employment Opportunities for Young People in Rural Africa
Kenya Struggles with Rising Alcoholism
Smugglers Peddle ‘Conflict Diamonds’ from Central African Republic, Ignoring Ban
Winners Announced for Free Expression Prize
Gates Foundation Slammed for Plan to Privatise African Seed Markets
Opinion: Water and Sanitation in Nigeria – Playing the Numbers Game
High-Tech to the Rescue of Southern Africa’s Smallholder Farmers
More >>
  Dernières Nouvelles
News in RSS
Lawyers, Rights Groups Rally Around Author of ‘Blood Diamonds’, Facing Jail
Former Military Man Declares Victory in Nigerian Polls
Activists Protest Denial of Condoms to Africa’s High-Risk Groups
Decent Employment Opportunities for Young People in Rural Africa
Kenya Struggles with Rising Alcoholism
A lire également>>