Inter Press Service News Agency
Tuesday, June 19, 2018   21:25 GMT    
   Homepage
   World Service
   East Africa
   Southern Africa
   West Africa
   Central Africa
 
   Environment
   Health-HIV/AIDS
   Education
   Rights
   Politics
   Economics
   and Finance
   Development
   Energy
   Population
   Culture
 
   Radio Service
 
   Français
 
   About IPS
 
   ENGLISH
   ESPAÑOL
   FRANÇAIS
   ARABIC
   DEUTSCH
   ITALIANO
   NEDERLANDS
   PORTUGUÊS
   SUOMI
   SVENSKA
   SWAHILI
   TÜRKÇE
PrintSend to a friend
Readers Opinions


Kuelewa Mizizi ya Ajira kwa Watoto Nchini Ghana
Portia Crowe

KUMASI, Ghana, Oktoba 9 (IPS) - Akiwa na umri wa miaka kumi na moja, Thema, raia wa Kumasi, ana matumaini ya kuwa nesi atakapokuwa mkubwa. Hata hivyo, kwa sasa ameajiriwa akitembea kutoka teksi moja hadi nyingine au gari la abiria moja hadi jingine katika masaa ya abiria wengi, akibeba kontena lake la barafu kichwani huku akiziuza kwa wapita njia kwa pesewas 10 kila moja. Anapita katikati ya magari katika mji wa pili kwa ukubwa nchini Ghana; na amekuwa akifanya hivyo kwa miaka minne.

Ajira kwa watoto zinaongezeka nchini Ghana, hasa katika maeneo ya mijini. Kwa mujibu wa ripoti ya hali ya watoto duniani ya Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) ya mwaka 2012, asilimia 34 ya watoto nchini Ghana wenye umri kati ya miaka mitano na 14 wanatumika katika ajira – ongezeko kutoka asilimia 23 mwaka 2003. Emilia Allan, Ofisa wa Kutetea Watoto katika UNICEF Ghana, alibainisha kuwa Kumasi pekee ina asilimia nane ya takwimu hiyo.

Alielezea baadhi ya madhara ya ajira kwa watoto.

"Inakiuka haki za watoto, inaathiri afya zao, na inawaweza kuwajeruhi," alisema. "Inazuia na kuingiliana na elimu yao, na inasababisha baadhi ya madhara kama vile kunyonywa kingono, kufanyiwa ukatili na kusafirishwa kwa watoto."

Lakini kwa ujumla watoto kufanya kazi ni jambo linalokubalika nchini Ghana, na fasili ya ajira ya utotoni inajadiliwa kwa kina. Pamoja na kuwa umri wa chini kisheria kwa mtu kuajiriwa ni miaka 15, Sheria ya Watoto ya mwaka 1998 inasema kuwa watoto wenye umri wa miaka 13 na zaidi wanaweza kufanya baadhi ya kazi nafuu. Na Mpango wa Utekelezaji wa Kitaifa wa Kutokomeza Ajira Mbaya kwa Watoto wa hivi karibuni, unaojikita katika Mkataba Na. 182 wa Shirika la Kazi Duniani (ILO), ambao unatambua changamoto za kutokomeza kabisa ajira kwa watoto; umebuniwa, badala yake, kulinda watoto kutokana na kazi ambazo zinaweza kuathiri maendeleo yao kimwili au kielimu.

Moja ya suala lenye utata ni kazi za majumbani, kama vile kupika, kusafisha nyumba, kuuza maduka, na kutunza ndugu wadogo. Prince Ohene-Koranteng, mkurugenzi wa mawasiliano katika shirika la kulinda watoto la "Defense for Children International" nchini Ghana, alielezea kuwa kazi hizo mara nyingine zinakubalika.

"Mambo hayo yanawezekana, na hayafai kukomeshwa, ikiwa kama hayazuii mtoto kupata elimu bora," alisema. "Lakini yanatakiwa kuwa na kikomo mahali fulani, kwasababu katika mahali fulani mtoto anatakiwa kufanya kazi zake za shule," aliongeza.

Allan wa UNICEF alisema kuwa baadhi ya kazi za nyumbani zinaweza kuchangia watoto kuchangamana na wengine au kupata mafunzo, lakini anabainisha ni wakati gani hata kazi rahisi zinaweza kukiuka haki za watoto.

"Nchini Ghana, watoto wanasaidia familia zao," alielezea. "Msaada huo unapokuwa na athari katika afya ya mtoto, au katika elimu ya mtoto, inaonekana kama ajira kwa mtoto," alisema, akiongeza kuwa kila mtoto ana haki ya kulindwa kutokana na kufanya kazi ambazo zinatishia afya, elimu au maendeleo yake.

Watoto wengi pia wanasaidia wanafamilia wao kwa kufanya kazi za muda mfupi, na kuhudhuria shule katika mfumo wa kupokezana (shift). Wanaweza kwenda shule asubuhi na kufanya kazi mchana, au kufanya kazi siku fulani na kusoma siku nyingine. Lakini hili pia linaweza kuzuia maendeleo yao na kuonekana kama ajira kwa mtoto, kwa mujibu wa Allan.

"Kama mtoto . . . anakwenda kuuza vitu halafu anakwenda shule katika mfumo wa kupokezana, atakwenda shule akiwa amechoka na kuwa na usingizi. Hii inaathiri elimu ya mtoto, kwasababu akili inakuwa haifanyi kazi," alisema, akiongeza kuwa hawana muda wa kufanya kazi zao za shule.

Pia alibainisha kuwa wakati mtoto anapatiwa mzigo wa kubeba kichwani, pamoja na kuonekana kuwa kazi rahisi, inaweza kuathiri ukuaji wao wa kimwili na kuwa na athari katika maendeleo yao.

Uelewa wa Allan wa sheria za kitaifa unashabihiana na Ohene-Koranteng. Alisema kuwa aina yoyote ile ya kazi mbaya, iwe "rahisi" au "hatari," ni ajira kwa mtoto – na hivyo kuwa kinyume cha sheria. Lakini, alisema, sheria inatekelezwa mara chache.

"Hata kama sheria iko katika vitabu vyetu, vyombo vya utekelezaji vinapaswa kufanya kazi kubwa zaidi kuweza kulinda watoto," alisema.

"Kama tutaachia hili kwa wazazi pekee, kutokana na watoto kuwasaidia kufikia mahitaji yao ya kila siku, wataendelea kuwaingiza katika mitaa."

Kwa mujibu wa Jacob Achulu, mkurugenzi wa kanda ya Ashanti katika Wizara ya Ajira na Ustawi wa Jamii, matatizo hayo ya utekelezaji yanatokana na kukosekana kwa fedha.

"Mfumo wa sheria upo," alisema. "Tatizo ni utekelezaji – na nadhani inatokana na umaskini kuenea sana katika maeneo mengi ya nchi yetu."

Kukosekana kwa usalama wa fedha kunamzuia Aku kwenda shule. Ana umri wa miaka 10, na anahudhuria shule anapoweza, lakini wakati wazazi wake wanaposhindwa kulipia ada anauza pilipili katika soko la Kejetia.

"Alikwenda shule leo, lakini mwalimu alimfukuza kutokana na kushindwa kulipa ada," alielezea mwanamke katika soko hilo.

"Wanataka kwenda kesho, lakini kutokana na pesa—ada za shule—mama alisema watakwenda katika huduma badala yake," alitafsiri.

Achulu alitoa wito wa hatua kali zaidi kuchukuliwa.

"Miradi ya ILO na ya NGO inakaribishwa, lakini kuna haja ya kuwa na shughuli endelevu ambazo zitahakikisha kuwa familia zinaweza kuwabakisha watoto wao shule," alielezea.

Shirika la kutetea haki za watoto la "Ghana Children’s Rights Protection Foundation’, au GCRPF, ni shirika ambalo lina lengo la kufanya kazi kwa kutafutia ufumbuzi wa ajira kwa watoto kuanzia katika mzizi. Wanachama wake wanatoa vifaa vya shule na kufadhili wanafamilia wa kipato cha chini, na kusaidia wazazi kuingiza kipato cha nyongeza kupitia miradi mbalimbali ya moja kwa moja. Katibu wake, Osborn Kwasi-Sarpong, alibainisha umuhimu wa kuongeza kipato cha familia.

"Ni jinsi gani mtoto anaweza kwenda shule kesho kama ataacha kuuza maji leo?" aliuliza. "Jambo la msingi ambalo tunapaswa kufanya ni kuona ustawi wa mama, mzazi, kuweza kutafuta kitu cha kufanya kwa mikono yake," alielezea.

Na hatimaye, alisema mkurugenzi wa GCRPF, Mchungaji Christian Antwi-Boasiako, kuwaondoa watoto wengi mitaani na kuwapeleka shule kutakuwa na faida siyo tu kwa mtoto, lakini pia kwa taifa zima kwa ujumla.

"Mtoto anapaswa kuwa na elimu nzuri, na afya bora," alisema, "halafu wakati anapokua, atachangia pia katika maendeleo ya taifa." (END/2012)

 

 
 Latest News from Africa
News in RSS
XML error: The element 'html' is used but not declared in the DTD/Schema.
  Dernières Nouvelles
News in RSS
DEVELOPPEMENT: Nous devons penser autrement à la "sécurité"
AUSTRALIE: Le port de Newcastle bloqué par les Guerriers du changement climatique
IRAN: L’examen d’un document clé à l’AIEA suggère un coup d’Israël
PAKISTAN: Les Ahmadis confrontés à la mort ou à l’exil
ETATS-UNIS: Le budget de la défense peut accroître alors que le public est fatigué de la guerre
A lire également>>