Inter Press Service News Agency
Sunday, September 22, 2019   19:41 GMT    
   Homepage
   World Service
   East Africa
   Southern Africa
   West Africa
   Central Africa
 
   Environment
   Health-HIV/AIDS
   Education
   Rights
   Politics
   Economics
   and Finance
   Development
   Energy
   Population
   Culture
 
   Radio Service
 
   Français
 
   About IPS
 
   ENGLISH
   ESPAÑOL
   FRANÇAIS
   ARABIC
   DEUTSCH
   ITALIANO
   NEDERLANDS
   PORTUGUÊS
   SUOMI
   SVENSKA
   SWAHILI
   TÜRKÇE
PrintSend to a friend
Readers Opinions

Tanzania
Kuyafanya Maisha ya Kijijini Kuwa Rahisi
*Na Marko Gideon

DAR ES SALAAM, Oktoba 1 (IPS) - Rukia Seif ni muelimishaji rika wa masuala ya idadi ya watu, afya na mazingira (PHE) ambaye anaifanya dhana hii rahisi ya kiuchumi, kimazingira na kiafya kuwa rahisi kueleweka na hivyo kuwa na mantiki katika jamii anamoishi.

Kwa kiwango chochote kile, eneo la Mkalamo ambako Rukia anaishi ni kijiji halisi kinachotegemea kilimo nchini Tanzania. Katika suala jingine muhimu kulielewa, kijiji hicho ni tofauti mno na vijiji vingine. Mkalamo inapakana na Mbuga ya Taifa ya Saadani ambayo imejaa utajiri wa baoanuwai—mbuga pekee nchini Tanzania inayopakana na bahari.

Katika uhalisia, badala ya mbuga hii kufanya maisha kuwa rahisi, inayafanya kuwa magumu zaidi kwa wanajamii wa kijiji cha Mkalamo. Mbuga imepiga marufuku ukataji wowote ule wa kuni kwa ajili ya nishati na matumizi mengine, na hivyo kufanya kuwa vigumu kupata kuni za kutosha kwa ajili ya nishati ya kupikia. Pia ongezeko la idadi ya wanyama pori mara nyingine huvamia kijiji na kuharibu mazao ya wanakijiji hao. Akiwa kama muelimishaji rika wa PHE, Rukia anazungumza na wanajamii wenzake kuhusu masuala rahisi kuyafanya ili kuboresha maisha yao . Ujumbe wake unaeleweka vizuri: kwa kupanga familia, wanawake wanaweza kujihakikishia afya zao na za watoto wao kuwa bora na kuamua idadi ya watoto wanaoweza kuwazaa na kuwalea. Pia kwa kutumia majiko banifu, wanawake wanaweza kutumia muda mchache wa kwenda kuokota kuni na hivyo kuwa na muda wa kufanya shughuli nyingine za nyumbani au za kuwaingizia vipato. Kwa kufanya hivyo pia watakuwa na fursa ya kupunguza kiwango cha kuni kinachohitajika kwa ajili ya nishati na hivyo kusaidia kuifanya misitu kuwa na matumizi endelevu kwa ajili ya kizazi cha sasa na kijacho.

Ujumbe wa Rukia hauishii hapo. Anawapatia wanajamii wenzake ujumbe wa kujiunga na vikundi vya kuweka na kukopa vinavyojikita katika jamii. Anawahamasisha kuwa wanawake na wanaume wanapojiunga na vikundi hivyo watapata mtaji wa kuwasaidia kuwaongezea kipato katika shughuli zao za sasa au kuwa na vyanzo vipya vya kipato.

Rukia ni mfano mzuri wa jinsi gani masuala haya madogo madogo yanaweza kuboresha maisha ya familia na wakati huo huo yakilinda mazingira. Akiwa na umri wa miaka 36, ana watoto watatu wa kike, wenye umri wa miaka 14, 12, na mwingine mwaka mmoja na nusu.

Rukia na mume wake, Seif Ramadhani, wanachukua hatua za kupanga familia yao. Rukia alitumia vidonge vya uzazi wa mpango kabla hawajaamua kuwa na mtoto wao wa mwisho. Kwa sasa wanatumia mipira ya kiume kujikinga wakati Rukia akiwa ananyonyesha. Katika kazi yake, Rukia hukutana na kuzungumza na watu wengi kila siku. Anazungumzia uzazi wa mpango na kama mtu amevutiwa na mazungumzo na kutaka kuchukua hatua, anamwagiza kwenda kwa wasambazaji wa huduma za uzazi wa mpango katika jamii au kwenye zahanati ya karibu inayotoa huduma hizo.

"Nazungumza na watu wa rika langu juu ya kupanga familia zao ili tuweze kuwa na maliasili za kuweza kutosheleza mahitaji ya wanakijiji ambao wanategemea katika maliasili hizi," alisema Rukia na kuongeza, "Pia kwa kupanga familia yako, utapata muda wa kutosha wa kufanya shughuli zako nyingine."

Akiwa mwanachama hai wa kikundi cha kuweka na kukopa katika jamii yao, ambapo pia anafanya kazi kama mhasibu wake, Rukia anadhihirisha kuwa kweli ana muda wa kutosha wa kufanya mambo mengine. Kwa mtindo wa kuweka na kukopa, Rukia ameweza kujiongezea vyanzo vya mapato yake kwa kununua mashine ya kushona nguo na jiko banifu ambalo halitumii kuni nyingi.

Leo hii, anazalisha kipato kutokana na ufugaji wa ng’ombe na kuku, ushonaji, utengenezaji wa mikate, uuzaji wa vinwaji baridi na utengenezaji wa majiko banifu. Kwa ongezeko hili la kipato, Rukia na mume wake wameweza kuezeka nyumba yao kwa kutumia bati na kumpeleka binti wao wa kwanza shule ya sekondari —mafanikio makubwa katika nchi ambayo idadi ndogo ya watoto wa kike wanaendelea na masomo yao ya sekondari baada ya kumaliza elimu yao ya msingi.

"Kutokana na umaskini, watoto wengi wa kike wanaacha shule kabla ya kumalizan elimu yao ya msingi. Katika baadhi ya matukio wanafanya hivyo kutokana na kupoteza wazazi wao pengine kutokana na magonjwa ya malaria, VVU/UKIMWI au magonjwa mengine. Wengine ni maskini mno kumudu kununua sare za shule, vitabu au kumudu usafiri wa kwenda shule. Wengine wana mzigo mkubwa wa kazi za nyumbani, au katika nyumba ya jirani, wakifanya kazi kwa ajili ya kusaidia kuendesha maisha yao na hivyo kukosa muda wa kwenda shule," linasema shirika la Nurturing Minds katika tovuti yake.

Rukia anaonyesha majiko yake banifu mawili ambayo huyatumia kwa kuokea mikate na keki. Jiko moja ni rahisi ambalo limetengenezwa kwa udongo na hulitumia kwa kupikia nyumbani kwake. Majiko ya udongo ambayo yanagharimu chini ya dola za Kimarekani 2, yameanza kuwa maarufu katika jamii. Linaokoa matumizi ya kuni nyingi, linatoa moshi mchache na hivyo kupunguza hatari za kiafya zinazotokana na moshi na linatumia muda mchache kuivisha chakula.

"Naweza hata kuvaa nguo zangu nzuri na kupaka rangi za mdomoni wakati wa kutumia jiko hili kwasababu halitoi moshi," anaelezea Rukia huku akicheka.

Kutokana na kuona faida za majiko banifu, Rukia amewahamasisha watoaji huduma za uzazi wa mpango katika jamii na viongozi wa vijiji vitano kujiunga na timu ya watu wanaotangaza teknolojia ya majiko banifu. Yeye amekuwa mfano mzuri wa watu ambao wanafanya kwa vitendo kile wanachohubiri. Anaboresha maisha yake na ya familia, anasaidia wengine kujifunza kutoka kwake na kuhifadhi maliasili ambazo karibu kila mmoja katika jamii ya kijiji cha Mkalamo anazitegemea. *Makala hii hapo awali iliandikwa na Elin Torell wa Kituo cha Rasilimali za Pwani cha Chuo Kikuu cha Kisiwa cha Rhode (URI-CRC) ambacho hutoa msaada wa kiufundi kwa Shirika la Kuhifadhi Mazingira ya Ukanda wa Pwani (TCMP) katika utekelezaji wa mradi wa Watu, Afya na Mazingira na miradi mingine ya hifadhi ya mazingira chini ya ufadhili wa USAID. (END/2012)

 

 
 Latest News from Africa
News in RSS
XML error: The download of the specified resource has failed.
  Dernières Nouvelles
News in RSS
DEVELOPPEMENT: Nous devons penser autrement à la "sécurité"
AUSTRALIE: Le port de Newcastle bloqué par les Guerriers du changement climatique
IRAN: L’examen d’un document clé à l’AIEA suggère un coup d’Israël
PAKISTAN: Les Ahmadis confrontés à la mort ou à l’exil
ETATS-UNIS: Le budget de la défense peut accroître alors que le public est fatigué de la guerre
A lire également>>