Inter Press Service News Agency
Sunday, September 22, 2019   19:47 GMT    
   Homepage
   World Service
   East Africa
   Southern Africa
   West Africa
   Central Africa
 
   Environment
   Health-HIV/AIDS
   Education
   Rights
   Politics
   Economics
   and Finance
   Development
   Energy
   Population
   Culture
 
   Radio Service
 
   Français
 
   About IPS
 
   ENGLISH
   ESPAÑOL
   FRANÇAIS
   ARABIC
   DEUTSCH
   ITALIANO
   NEDERLANDS
   PORTUGUÊS
   SUOMI
   SVENSKA
   SWAHILI
   TÜRKÇE
PrintSend to a friend
Readers Opinions

TANZANIA
Kuhifadhi Kasa kwa Kutumia Teknolojia ya Satelaiti
Na Marko Gideon

DAR ES SALAAM, Septemba 6 (IPS) - Asasi isiyokuwa ya kiserikali inayojihusisha na hifadhi ya kasa katika pwani ya Bahari ya Hindi nchini Tanzania imeanza kutumia teknolojia ya Satelaiti kuboresha hifadhi ya wanyama hao wa baharini waliopo katika hatari ya kutoweka.

Akizungumza hivi karibuni wakati wa mkutano wa nusu mwaka wa washirika wa mradi wa Pwani unaopata ufadhili kutoka Shirika la Misaada la Watu wa Marekani (USAID), Afisa wa shirika la Sea Sense, Boniventure Mchomvu alisema shirika lake "linatumia teknolojia ya kisasa zaidi ya kufanya utafiti muhimu juu ya tabia za kasa kwa kutumia teknolojia ya satelaiti."

Aliongeza kuwa katika kipindi cha miezi minne iliyopita, vibandiko vyenye uwezo wa kuwasiliana na mitambo ya satelaiti na kutoa taarifa za mwenendo wa kasa vimeshafungwa kwa kasa sita. Vibandiko hivyo, kwa mujibu wa Mchomvu, huwasilisha taarifa kwenye mitambo ya satelaiti kila mara baada ya kasa kujitokeza nje ya maji kwa ajili ya kupumua, na hivyo rahisi kutoa taarifa mahali ambapo kasa yupo.

"Katika kipindi cha wiki chache tu, kasa waliovikwa vibandiko hivyo wameshatoa taarifa muhimu sana juu ya mwenendo wao. Mmoja wa kasa, mwenye jina la Mwisho ameshasafiri kuelekea eneo la malisho kaskazini mwa Mombasa wakati mwenzake Zianna kwa sasa anaogelea kupitia mwambao wa Kenya kuelekea nchini Somalia na haonyeshi dalili ya kuhitimisha safari yake. Tulia ameamua kuelekea upande wa kusini na alikuwa akipita eneo la Kilwa", alisema.

Kwa mujibu wa Mchomvu, kuelewa mwenendo wa kasa ni jambo muhimu mno kujua maisha ya viumbe hao. "Mfano, tumeshagundua kuwa kuna eneo la Temeke ambalo kasa wote, wawe wanaelekea kaskazini au kusini, ni lazima wapitie hapo ndipo waanze safari yao. Utafiti utatusaidia kujua eneo hilo lina nini hadi kuwa makutano ya kasa wote," alisema. Kupata taarifa kutasaidia Sea Sense kubaini maeneo muhimu ya malisho nchini Tanzania na katika ukanda mzima pia".

Alisema taarifa hizo pia zitasaidia kujua ni maeneo gani hatari zaidi kwa kasa wanaosafiri kutoka eneo moja kwenda jingine na kuelekeza jitihada katika kupunguza hatari katika maeneo hayo, hasa katika maeneo yenye hatari ya kasa kunasa kwenye nyavu za wavuvi," alisema.

Pamoja na kasa, Sea Sense pia inashirikiana na jamii za pwani ncini Tanzania kuhifadhi wanyama wengine waliopo katika hatari ya kutoweka kama vile nguva, nyangumi, pomboo na papa nyangumi.

Kwa mujibu wa tovoti ya shirika hilo, "viumbe hawa, pamoja na makazi yao wanakabiliwa na mustakabali wa maisha usiokuwa na uhakika, hasa kutokana na shughuli za mwanadamu katika ukanda wa pwani. Maisha yao yanawezekana tu kama kuna jitihada za kuhifadhi eneo zima la pwani ikiwa ni pamoja na baoanuai ya bahari na kuboresha maisha ya watu wanaoishi katika maeneo ya mwambao."

Kasa ni miongoni mwa viumbe wa bahari waliopo katika hatari ya kutoweka, kwani tafiti duniani kote zinaonyesha kuwa miaka hamsini iliyopita kulikuwa na kasa wengi katika bahari, lakini kutokana na sababu nyingi idadi ya kasa wamezidi kupungua. Baadhi ya sababu hizo ni pamoja na watu kupendelea kula nyama ya kasa, mayai na kujenga hoteli katika fukwe zinazotumiwa na kasa hao kwa ajili ya kutaga na kutotoa watoto.

Wakati maendeleo ni muhimu katika maeneo ya mwambao wa pwani, ni muhimu kuhifadhi kasa kwani wanasaidia sana katika hifadhi ya mazingira ya bahari. Baadhi ya aina ya kasa wanafanya kazi kubwa ya kusafisha matumbawe na hivyo kuleta usawa wa baoanuai. (END/2012)

 

 
 Latest News from Africa
News in RSS
XML error: The download of the specified resource has failed.
  Dernières Nouvelles
News in RSS
DEVELOPPEMENT: Nous devons penser autrement à la "sécurité"
AUSTRALIE: Le port de Newcastle bloqué par les Guerriers du changement climatique
IRAN: L’examen d’un document clé à l’AIEA suggère un coup d’Israël
PAKISTAN: Les Ahmadis confrontés à la mort ou à l’exil
ETATS-UNIS: Le budget de la défense peut accroître alors que le public est fatigué de la guerre
A lire également>>