Inter Press Service News Agency
Sunday, September 22, 2019   19:55 GMT    
   Homepage
   World Service
   East Africa
   Southern Africa
   West Africa
   Central Africa
 
   Environment
   Health-HIV/AIDS
   Education
   Rights
   Politics
   Economics
   and Finance
   Development
   Energy
   Population
   Culture
 
   Radio Service
 
   Français
 
   About IPS
 
   ENGLISH
   ESPAÑOL
   FRANÇAIS
   ARABIC
   DEUTSCH
   ITALIANO
   NEDERLANDS
   PORTUGUÊS
   SUOMI
   SVENSKA
   SWAHILI
   TÜRKÇE
PrintSend to a friend
Readers Opinions

TANZANIA
SACCOs Kupunguza Umaskini Wilayani Pangani
Na Marko Gideon

PANGANI, Julai 30 (IPS) - Umaskini ni adui namba moja nchini Tanzania. Kiongozi wa kwanza kutangaza vita dhidi ya umaskini ni Rais wa awamu ya kwanza hayati Julius Kambarage Nyerere, pale aliposema nchi inakabiliwa na maadui watatu ambao ni umaskini, ujinga na maradhi.

Tangu wakati huo, serikali mbalimbali zilizopokezana madaraka kwa awamu zimekuwa zikibuni mipango mbalimbali ya kuutokomeza umaskini. Na sasa nchi inaongozwa na serikali ya awamu ya nne, ambayo dhamira yake ya kuutokomeza umaskini ilionekana tangu kipindi cha kampeni za kuingia madarakani pale mgombea wake wa Urais, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete alipokuja na kaulimbiu ya "maisha bora kwa kila Mtanzania".

Akisisitiza kuwa maisha bora yataletwa na kila mwananchi, Rais Kikwete alisema wakati wa hotuba yake ya kwanza bungeni mjini Dodoma Disemba 30, 2005 "Maisha bora kwa kila Mtanzania yanawezekana, kila mmoja wetu atimize wajibu wake".

Hata hivyo, pamoja na jitihada hizi takwimu zinaonyesha kuwa bado Tanzania ni moja ya nchi maskini zaidi duniani huku Watanzania wengi hasa waishio katika maeneo ya vijijini wakiendelea kuishi katika umaskini uliokithiri. Kwa mujibu wa Utafiti wa Bajeti katika Ngazi ya Kaya wa mwaka 2007, "asilimia 34 ya Watanzania, hasa katika maeneo ya vijijini, wanaishi chini ya umaskini wa kuweza kupata mahitaji yao ya lazima".

Ni hali hii ya umaskini ambayo imefanya wadau mbalimbali wa maendeleo kubuni njia za kuwanasua wananchi hasa wa vijijini kuondokana na janga hili. Moja ya wadau hao ni Mradi wa Pwani wa Mpango wa Kusimamia Mazingira na Rasilimali za Ukanda wa Pwani (TCMP-Pwani) ambao unaendesha shughuli zake za kutunza mazingira kwa kuboresha maisha ya wananchi wa pwani ya Bahari ya Hindi.

Mradi huo unaofadhiliwa na Shirika la Misaada ya Kimataifa la Watu wa Marekani (USAID) na kupata msaada wa kiufundi kutoka Kituo cha Rasilimali za Bahari cha Chuo Kikuu cha Rhode Island, unaendesha shughuli mbalimbali za utunzaji wa mazingira kwa kuboresha vipato vya wananchi katika wilaya za Bagamoyo, Pangani na eneo la Ghuba ya Menai huko Zanzibar ili kupunguza utegemezi mkubwa katika mazingira na rasilimali za pwani na bahari ambazo matumizi yake makubwa yatasababisha vizazi vijavyo kukosa urithi wa rasilimali hizo.

Akizungumza hivi karibuni wakati wa mafunzo ya kuboresha utunzaji wa kumbukumbu wa vyama vya ushirika vya kuweka na kukopa (SACCOs) katika vijiji vya Sange, Mwembeni na Ushongo wilayani Pangani, Mratibu wa Kitengo cha Kujenga Uwezo wa Kiuchumi katika mradi wa TCMP-Pwani, Patrick Kajubili alisema "Sababu kubwa zinazosababisha kuendelea kuharibu mazingira ya ukanda wa pwani ni umaskini. Na umaskini kwa kiasi kikubwa unatokana na kukosekana kwa mtaji."

Alisema kuwa TCMP-Pwani inaunga mkono jitihada za wananchi za kuweka na kukopa kwa ajili ya kujipatia mtaji kwa kutoa mbegu ya milioni moja na nusu. Baada ya miezi sita na kuonekana maendeleo ni mazuri inaongeza tena kiasi kama hicho cha fedha.

Moja ya makundi yanayokabiliwa na umaskini mkubwa nchini ni wanawake. Takwimu zinaonyesha kuwa pamoja na wanawake kuwa mstari wa mbele katika kuendesha kaya nchini Tanzania, ndiyo wanaobeba mzigo mkubwa wa umaskini kuliko wenzao wanaume.

TCMP-Pwani inalitambua hilo ndiyo sababu moja ya malengo yake ni kuhakikisha watu kutoka makundi maalum ya walemavu, wajane, yatima na wanaoishi na virusi vya Ukimwi ambao wengi wao ni wanawake wanapewa kipaumbele cha kuongezewa mitaji wanapojiunga na SACCOs.

"Nimefurahi sana kuwa kati ya wanachama 40, wa SACCOs ya kijiji cha Mwembeni, 30 ni wanawake, huu ni ukombozi mkubwa sana kwa wanawake," alisema Kajubili.

Aliongeza kuwa katika kila kijiji TCMP-Pwani itasaidia watu 15 kutoka makundi maalum. Kwa kuwapatia mtaji watu kutoka makundi hayo itawasaidia kuanzisha shughuli za kujiingizia kipato ambazo ni rafiki wa mazingira na kupunguza mzigo kwa wananchi na uongozi wa kijiji kwani watu hawa wakianza kujitegemea wataweza kusaidia watoto wao, kuwasomesha na kuwapatia matumizi ya lazima.

Akiongea katika kijiji cha Ushongo, Afisa Ushirika wa Wilaya ya Pangani ambaye pia alikuwa mwezeshaji katika mafunzo ya siku tatu, Julius Chagama, alisema njia pekee ya kuwezesha watu wa kipato cha chini na hasa waliopo kijijini kuweza kupata maendeleo ni kujiunga na SACCOs.

"Hakuna njia ya kumkomboa Mtanzania ila SACCOs," alisema. "SACCOs iko katika msingi wa kisheria – kama ikifuata sheria – itaweka kumbukumbu vizuri, itakaguliwa kila mwaka na kutengenezewa hesabu za mwisho yaani balance sheet na inakuwa na uwezo wa kukopa katika vyombvo vikubwa vya fedha".

Aliongeza kuwa taasisi za fedha zinatafuta jinsi gani ya kusaidia watu wa kijijini ambao mali zao hazijarasimishwa, ila kupitia SACCOs ni rahisi kupata mikopo kutoka vyombo hivyo. Alisema kwa hali ilivyo sasa siyo rahisi kumpatia mtu chakula, unachotakiwa ni kumwezesha mtu ili ajisaidie mwenyewe.

Akitoa mfano wa TCMP-Pwani alisema mradi unataka kusaidia makundi maalum ili badala ya kuwasaidia watu hao misaada, wanapatiwa mitaji kupitia SACCOs na pia kuwawezesha kujiwekea akiba na hivyo kushindwa kuwa tegemezi. Alitoa wito kwa Halmashauri ya Wilaya na mashirika mengine kutambua kuwa hii ndiyo njia pekee ya kuwaondoa wananchi katika umaskini.

Akizungumzia manufaa aliyoyapata kutokana na mafunzo hayo, mshiriki wa mafunzo na mwanachama wa SACCOs ya Mwembeni, Shukura Mdoe Selemani alisema "Nilikuwa sijui kuwa nikiitoa hela yangu itakuwa salama, nilidhani italiwa na chama, lakini sasa nimeelewa. Nitazidi kuelimisha wale ambao hawakuhudhuria juu ya umuhimu wa kujiunga na SACCOs".

Kwa upande wake, Mweka Hazina wa SACCOs hiyo iliyoanzishwa mwaka jana, Zuhura Awadhi alisema "mafunzo yametusaidia sana, asilimia tisini ya wanachama hatukuwa tunajua umuhimu wa vyama hivi vya kuweka na kukopa. Sasa tunajua kuna umuhimu wa kuanzisha vyama ambavyo vitatuwezesha kupata misaada kutoka taasisi mbalimbali."

Alisema mtaji wa milioni moja na laki tano waliopatiwa na TCMP-Pwani utaongeza mtaji wao. Hii itawezesha kutoa mikopo kwa watu wengi zaidi kuliko ilivyokuwa hapo kabla. (END/2012)

 

 
 Latest News from Africa
News in RSS
XML error: The download of the specified resource has failed.
  Dernières Nouvelles
News in RSS
DEVELOPPEMENT: Nous devons penser autrement à la "sécurité"
AUSTRALIE: Le port de Newcastle bloqué par les Guerriers du changement climatique
IRAN: L’examen d’un document clé à l’AIEA suggère un coup d’Israël
PAKISTAN: Les Ahmadis confrontés à la mort ou à l’exil
ETATS-UNIS: Le budget de la défense peut accroître alors que le public est fatigué de la guerre
A lire également>>