Inter Press Service News Agency
Sunday, September 22, 2019   19:38 GMT    
   Homepage
   World Service
   East Africa
   Southern Africa
   West Africa
   Central Africa
 
   Environment
   Health-HIV/AIDS
   Education
   Rights
   Politics
   Economics
   and Finance
   Development
   Energy
   Population
   Culture
 
   Radio Service
 
   Français
 
   About IPS
 
   ENGLISH
   ESPAÑOL
   FRANÇAIS
   ARABIC
   DEUTSCH
   ITALIANO
   NEDERLANDS
   PORTUGUÊS
   SUOMI
   SVENSKA
   SWAHILI
   TÜRKÇE
PrintSend to a friend
Readers Opinions

TANZANIA
Lulu Yainua Kipato Cha Wanawake Zanzibar
Na Marko Gideon

DAR ES SALAAM, Juni 27 (IPS) - Wakati Watanzania wengi wanabuni njia mbalimbali za kuboresha hali ya maisha yao ambayo imekuwa ikizidi kuwa duni siku hadi siku, miaka hadi miaka, uandaaji na utengenezaji wa mapambo yatokanayo na nusu lulu umeonyesha kuwa njia muafaka ya kuboresha kipato cha wanawake katika Eneo la Hifadhi ya Ghuba ya Menai huko Zanzibar.

Mamia ya wanawake waliokusanyika katika vikundi kama vile Chaza Imara, Ukweli ni Njia Safi, Mapambo Bweleo, Jitegemee, Nia Safi, Chaza Mali na Chaza Mpya kutoka vijiji vya Fumba, Bweleo, Chaleni, Unguja Ukuu, Chamanzi, Kikungwi na Kizingo ambao wengi wao wanajishughulisha na utengenezaji wa mapambo yatokanayo na nusu lulu, wanakiri kupata mafanikio kutokana na shughuli hizo.

Wakiongea katika mkusanyiko wa pamoja walipotembelewa na ujumbe wa kamati inayosimamia utekelezaji wa miradi ya mazingira inayofadhiliwa na Shirika la Misaada la Watu wa Marekani (USAID) mwaka jana, wanawake hao wamesema shughuli hizo zimewasaidia kujipatia kipato kwa ajili ya kuwasomesha watoto wao, kuwapeleka hospitalini, kupata mahitaji mbalimbali ya kifamilia na hata kujenga nyumba zao wenyewe.

"Kwa kweli utengenezaji wa mapambo yatokanayo na nusu lulu umeboresha maisha yangu na ya familia yangu kwa kiasi kikubwa," anakiri mama Safia Mnyecha . "Nimeweza kusomesha watoto wangu na nimeanza mradi wa ujenzi wa nyumba ya kuishi."

Akitaja historia fupi ya vikundi hivyo, Dk. Narriman Jidawi alisema shughuli zilianza mwaka 2003 kwa ufugaji wa chaza, halafu mradi wa SUCCESS chini ya Mpango wa Kusimamia Mazingira ya Ukanda wa Pwani na Bahari (TCMP) mwaka 2005 uliendelea kusaidia shughuli za utengenezaji wa lulu na mapambo kabla ya mradi wa RecoMap kuingia na kuendeleza shughuli hizo. Kwa sasa shughuli hizo zipo chini ya mradi wa Pwani ambao pia upo chini ya TCMP.

Kwa mujibu wa Bi. Mnyecha, kikundi chake cha Ukweli ni Njia Safi, mbali na kujishughulisha na utengenezaji mapambo pia kinauza sabuni za mwani na liwa na kuuza liwa za unga.

Alisema wanakikundi wanashiriki kwenye maonesho ndani na nje ya nchi kutangaza biashara zao. Ili kuhakikisha jitihada zinakuwepo, kila mmoja anaendesha shughuli zake mwenyewe na kuweka hisa kwenye kikundi.

"Mradi umeniinua sana sana, sana. Sasa nyumba yangu imebakia madirisha na milango ya chumbani tu ili nihamie," alikiri Bi Mnyecha. Aliongeza kuwa kipato anachokipata kimemuwezesha kuwasomesha watoto wake katika shule za binafsi na ameweza kuwanunulia baiskeli ili waweze kuwahi shule.

"Wanawake tulikuwa tegemezi, tulikuwa tukitegemea waume zetu tu na mishahara yao midogo," alisema. "Lakini maisha tumeshaweza kuyakaba sasa hivi, zamani wanawake wa Zanzibar mambo hayo hatukuyaweza, lakini sasa tunaweza".

Wengine katika vikundi hivyo wanajivunia shughuli za mapambo kuweza kuwapeleka mahali kama Marekani kwenda kutafuta elimu. Kwa mujibu wa Dk. Jidawi, wanawake watano wamepata fursa ya kusafiri kwenda nchini Marekani kujifunza zaidi jinsi ya kutengeneza mapambo. Elimu hiyo imewafanya kuwa na ujuzi wa kutengeneza mapambo kama vile kidani zenye uwezo wa kuuzwa hata zaidi ya dola 2000.

Shughuli zinazoendeshwa na mamia ya wanawake hao ambao kati yao wanaume ni wanne tu zimebuniwa kuongeza kipato ili kupunguza utegemezi mkubwa wa rasilimali za pwani na bahari ambazo zinapaswa kutumika kwa njia endelevu kwa ajili ya kizazi cha sasa na kijacho. Shughuli hizo zinasaidia kutunza mazingira na rasilimali za pwani kwa kuanzisha maeneo tengefu baharini. Vikundi vinashiriki kikamilifu kuweka maeneo tengefu ili kuongeza kuzaliana kwa chaza baharini.

Kwa mujibu wa vikundi hivyo, kuna maeneo tengefu manne ambayo yamegawanyika katika vijiji vinne. Katika kila eneo tengefu, kuna eneo la kuchukua chaza (makarogwe) ambazo hutumika kutengeneza nusu lulu na hatimaye mapambo na pia kwa chakula. Vijiji ambavyo maeneo tengefu hupatikana ni pamoja na Bweleo, Fumba, Nyamanzi na Chaleni.

"Tunaendeleza maeneo tengefu kwani bila kuhifadhi bahari ni sawa na kuruhusu matumizi ya msitu ambapo watu wanakata miti hadi msitu unaisha. Lakini kwa kuendeleza maeneo tengefu, tunaweza kuhifadhi chaza kwa kutumia sheria ndogondogo ambapo mtu akikutwa anavua katika maeneo tengefu anapigwa faini na fedha zinazopatikana zinakwenda kuendeleza skuli na nyingine zinabakia katika serikali ya kijiji," anaeleza Ikiwa Abdallah Ali kutoka Shehia ya Fumba Bondeni.

Bi Rahma Musa kutoka Fumba ameenda mbali zaidi ya utengenezaji wa mapambo. Anasema mbali na kutengeneza mapambo, amejifunza lugha ya Kiitaliano na pia ujuzi wa kukaribisha na kuwakabili wateja.

"Nimenufaika sana na mapambo, nashukuru, nilikuwa niko mbali sana lakini sasa nipo karibu," anasema Bi Musa. "Nimejifunza lugha ya biashara, nimejifunza kuwa mjasiriamali hupaswi kuonyesha uso wa kununa, unapaswa kuwa na sura ya furaha unapokuwa katika biashara yako. Pia nimejifunza lugha ya Kiitaliano kwa ajili ya biashara na nilipata fursa ya kwenda Marekani kujifunza masuala ya mapambo.

"Kutokana na mume kunipatia ruksa kila ninapotakiwa kutoka, nimeamua kumnunulia ngarawa kwa ajili ya kuvulia samaki," alisema Bi Musa kwa furaha.

Lakini katika kila penye maendeleo hapakosi changamoto zake. Vikundi vyote vimesema vinakabiliwa na changamoto ya uhaba wa vifaa na hivyo kutumia vifaa duni kama vile misumeno ya bati ambayo ni duni mno ikilinganishwa na ile inayotumiwa na watengezaji wa biashara ambao wanaweza kutengeneza lulu wanayoweza kuuza hadi dola 2000.

Changamoto nyingine ni ushindani ambapo kuna ushindani wa ndani unaotokana na wafanyabiashara wakubwa na ushindani wa nje ambapo baadhi ya mapambo kutoka Kenya huuzwa kwa bei ya chini mno ikilinganishwa na mapambo ya wanavikundi hao. Mbali ya changamoto za vifaa na masoko, wanavikundi wametoa wito wa kupatiwa utaalam zaidi wa kutengeneza mapambo ili kuhimili zaidi ushindani. (END/2012)

 

 
 Latest News from Africa
News in RSS
XML error: The download of the specified resource has failed.
  Dernières Nouvelles
News in RSS
DEVELOPPEMENT: Nous devons penser autrement à la "sécurité"
AUSTRALIE: Le port de Newcastle bloqué par les Guerriers du changement climatique
IRAN: L’examen d’un document clé à l’AIEA suggère un coup d’Israël
PAKISTAN: Les Ahmadis confrontés à la mort ou à l’exil
ETATS-UNIS: Le budget de la défense peut accroître alors que le public est fatigué de la guerre
A lire également>>