Inter Press Service News Agency
Sunday, September 22, 2019   19:39 GMT    
   Homepage
   World Service
   East Africa
   Southern Africa
   West Africa
   Central Africa
 
   Environment
   Health-HIV/AIDS
   Education
   Rights
   Politics
   Economics
   and Finance
   Development
   Energy
   Population
   Culture
 
   Radio Service
 
   Français
 
   About IPS
 
   ENGLISH
   ESPAÑOL
   FRANÇAIS
   ARABIC
   DEUTSCH
   ITALIANO
   NEDERLANDS
   PORTUGUÊS
   SUOMI
   SVENSKA
   SWAHILI
   TÜRKÇE
PrintSend to a friend
Readers Opinions

TANZANIA
Ufugaji Viumbe Bahari, Muhimu Kuongeza Kipato, Kutunza Mazingira
Marko Gideon

BAGAMOYO, Mei 7 (IPS) - Kwa miaka mingi wakazi wa pwani wamekuwa wakitegemea zaidi kujipatia kipato na chakula kutokana na kuendesha shughuli za uvuvi aidha katika mabwawa au kwenye Bahari ya Hindi. "Lakini kutokana na kuongezeka kwa watu samaki wamepungua kwa kiasi kikubwa katika bahari na katika mabwawa ya asili na mahitaji yamezidi kuongezeka," alisema Mkurugenzi wa Mradi wa Pwani wa Mpango wa Kusimamia Mazingira na Rasilimali za Pwani (TCMP – Pwani), Baraka Kalangahe.

"Kufuga ni njia pekee ya kuziba pengo la wale samaki wanaokosekana baharini na katika mabwawa ya asili na hii ndiyo hali katika dunia nzima," aliongeza Kalangahe.

Akizungumza wakati wa kuwasilisha ripoti ya Utengaji wa Maeneo ya Kufugia Viumbe Bahari iliyoandaliwa na Mradi wa Pwani unaofadhiliwa na USAID na kupata msaada wa kiufundi kutoka Kituo cha Rasilimali za Pwani cha Chuo Kikuu cha Rhode Island kwenye mkutano wa Kamati ya Kusimamia Mazingira ya Pwani ya Wilaya ya Bagamyo mwezi Machi mwaka huu, Kalangahe alisema kuwa kama ilivyokuwa kwa uvuvi wa samaki baharini ambao unaendeshwa kwa njia isiyokuwa endelevu, ufugaji wa viumbe bahari pia ukiendeshwa bila kudhibitiwa unaweza kukiuka taratibu za uhifadhi wa mazingira na hivyo kushindwa kuwa endelevu.

"Kila kitu kina uzuri na ubaya wake," alisema. "Kama ilivyokuwa baharini ambapo uvuvi siyo endelevu, na katika ufugaji wa viumbe bahari tahadhari inapaswa kuchukuliwa ili tusiingie katika yale yanayojitokeza baharini."

Alisema kutokana na kuwa lengo kubwa la TCMP-Pwani ni hifadhi ya mazingira na rasilimali za pwani, mradi unachochea ufugaji wa samaki katika ukanda wa pwani kwa lengo la kuhakikisha wanajamii katika ukanda huo wanajiingizia kipato na wakati huo huo kuhakikisha hakuna uharibifu wa mazingira.

"Hatutaki ufugaji kuendeshwa kiholela, tunataka ufugaji kufuata utaratibu ili kuhakikisha kuna utunzaji wa mazingira," alisema Kalangahe.

Mradi wa TCMP-Pwani unakuza ufugaji wa viumbe bahari kwa wafugaji wadogo wadogo kwa kutambua kuwa kwa kufanya hivyo ni rahisi kuinuia kipato na kupunguza umaskini katika ngazi ya kaya.

Kwa kufanya hivyo mradi unachangia jitihada za kitaifa za kupunguza umaskini katika nchi ambayo wananchi wake wengi, hasa wale wanaoishi maeneo ya vijijini wanaishi chini ya dola moja kwa siku. Kwa mujibu wa utafiti wa bajeti katika ngazi ya kaya wa mwaka 2007, asilimia 34 ya Watanzania, hasa katika maeneo ya vijijini, wanaishi chini ya umaskini unaowafanya hata kushindwa kupata mahitaji yao ya lazima. Wakazi wa maeneo ya vijijini katika maeneo ya pwani ni miongoni mwa maskini hao.

"Utaratibu tunaouwakilisha ni wa wafugaji wadogo wadogo ambao wakiachwa kuendesha ufugaji kiholela wanaweza kuchangia katika uharibifu wa mazingira," alifafanua Kalangahe.

Uandaaji wa Ripoti Akiwasilisha ripoti hiyo kwa kikundi kazi cha ufugaji wa viumbe bahari wilayani Bagamoyo, mjumbe wa kikundi kazi cha wataalam wa ufugaji viumbe bahari cha wilaya ya Bagamayo, Ambakisye Simtoe alisema kazi ya uandaaji wa ripoti hiyo haikuwa rahisi kwani ilihusu kutembea kwa miguu kutoka kijiji cha Kiharaka hadi Saadani katika mwambao wa pwani.

"Tulitembea kama kilomita 30 tukiangalia mabwawa ya chumvi na kuchukua vipimo vya kijiografia, aina ya udongo, shughuli zinazoendelea katika ufugaji wa samaki" alisema Simtoe. Pia timu iliangalia umiliki kama ni wa mtu binafsi, wa kijiji ama wa kampuni.

Alisema taarifa zilizopatikana zilitumika kuandaa ramani na kuzirejesha kwa vijiji husika ili kuzipitia na kuwafahamisha walichokiona na wakaridhia taarifa hizo kuwa ni sahihi.

Baada ya kuandaa ripoti hiyo kwa kutembelea vijiji kadhaa vya mwambao wa pwani wilayani Bagamoyo kujua fursa zilizopo kuendesha ufugaji wa viumbe bahari, matokeo kadha wa kadha yalionekana.

Moja ya matokeo hayo ni uharibifu mkubwa wa mazingira ikiwa ni pamoja na kukatwa kwa mikoko na kuzuia maji baridi yasiingie katika baadhi ya maeneo ya mikoko hiyo. Maeneo yaliyoathirika ni pamoja na Kiharaka, Changwaela, Chalawe katika mdomo wa Mto Ruvu.

Pia utafiti uligundua kuwa ufugaji wa samaki kwa kiasi kikubwa haupo rasmi. Kutokana na ufugaji kutokuhusisha wataalam, ulichangia kwa kiasi kikubwa katika uharibifu wa mazingira kama vile ukataji wa mikoko na kuangamiza mikoko kwa kuzuia maji baridi yasifikie mabwawa ya samaki.

Utafiti huo pia uligundua kuwa kuna migogoro mikubwa ya ardhi katika maeneo ya pwani.

Mapendekezo Ripoti ya kuandaa utaratibu wa ufugaji wa viumbe bahari inaonyesha haja ya kuwa na Mpango Mkakati wa Ufugaji Samaki katika mwambao wa Bagamoyo. "Ila kuna haja ya kuweka udhibiti ili kuwe na uzingatiwaji wa sheria," alisema Simtoe.

Wadau katika mkutano huo walitaka kuwepo kwa mtaalam wa ufugaji wa samaki katika kila kijiji kusimamia Mpango Mkakati huo. "Kama ilivyo kwa mabwana shamba, na wafugaji wa samaki wasiachwe peke yao, awepo mtu wa kuwasimamia wakati wote," alisema mmoja ya washiriki wa mkutano.

Hata hivyo, Bagamoyo ina bahati kwani kuna chuo cha Mbegani ambacho kinatoa mafunzo ya maafisa ugani wa ufugaji wa samaki. Katika chuo hicho, pia kuna mabwawa darasa kwa ajili ya wanafunzi.

"Tatizo tulilonalo kitaifa ni kwamba wakati tulipoanza kuhamasisha wananchi kuanzisha ufugaji wa viumbe bahari, sekta ilikuwa nyuma sana, kulikuwa hakuna wataalam wa ufugaji," alielezea Mkurugenzi wa TCMP, Jeremiah Daffa. "Vyuo vilitoa mafunzo ya jinsi ya kuvua, lakini sasa mtaala unaanza kutoa mafunzo ya jinsi ya kufuga."

Hata hivyo, changamoto iliyopo ni kwamba hadi sasa maafisa ugani wa samaki waliopo ni wale ambao wana taaluma ya kuvua na wala siyo kufuga samaki, aliongeza Daffa. Aliwaasa maafisa ugani wa samaki kuongeza elimu zaidi ili wawe maafisa ugani samaki wazuri katika ngazi ya wilaya. (END/2012)

 

 
 Latest News from Africa
News in RSS
XML error: The download of the specified resource has failed.
  Dernières Nouvelles
News in RSS
DEVELOPPEMENT: Nous devons penser autrement à la "sécurité"
AUSTRALIE: Le port de Newcastle bloqué par les Guerriers du changement climatique
IRAN: L’examen d’un document clé à l’AIEA suggère un coup d’Israël
PAKISTAN: Les Ahmadis confrontés à la mort ou à l’exil
ETATS-UNIS: Le budget de la défense peut accroître alors que le public est fatigué de la guerre
A lire également>>