Inter Press Service News Agency
Sunday, September 22, 2019   20:11 GMT    
   Homepage
   World Service
   East Africa
   Southern Africa
   West Africa
   Central Africa
 
   Environment
   Health-HIV/AIDS
   Education
   Rights
   Politics
   Economics
   and Finance
   Development
   Energy
   Population
   Culture
 
   Radio Service
 
   Français
 
   About IPS
 
   ENGLISH
   ESPAÑOL
   FRANÇAIS
   ARABIC
   DEUTSCH
   ITALIANO
   NEDERLANDS
   PORTUGUÊS
   SUOMI
   SVENSKA
   SWAHILI
   TÜRKÇE
PrintSend to a friend
Readers Opinions

TANZANIA
Inawezekana Kutunza Pwani Yetu, Kama Kila Mtu Atatimiza Wajibu
Na Marko Gideon

PANGANI,, MACHI 16 (IPS) - Viongozi na watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani, mkoani Tanga, wametakiwa kushirikiana katika kutunza mazingira na rasilimali za pwani kwa ajili ya kizazi cha sasa na kijacho.

Akizungumza wakati wa kufungua mkutano wa wajumbe wa kamati ya kusimamia mazingira na rasilimali za ukanda wa pwani (ICM) wilayani humo, mkurugenzi wa wilaya hiyo, Rashid Neneka aliwataka wajumbe kutoka sekta mbalimbali na viongozi wa halmashauri kushirikiana katika kuhakikisha shughuli zote zinazohusu utunzaji wa mazingira na rasilimali za ukanda wa pwani zinatekelezwa kikamilifu na kwa mafanikio.

Katika mkutano huo uliokuwa na lengo la kuwasilisha kwa halmshauri ya wilaya mpango kazi wa mwaka 2012 wa Mpango wa Kusimamia Mazingira ya Ukanda wa Pwani (TCMP-Pwani), unaofadhiliwa na serikali ya Marekani kupitia Shirika la Misaada ya Kimataifa (UASID) na kupata msaada wa kiufundi kutoka Kituo cha Rasilimali za Pwani cha Chuo Kikuu cha Rhode Island (CRC-URI), vikundi kazi viwili vilianzishwa miongoni mwa watendaji wa kisekta wa Hamashauri ya Wilaya hiyo kusaidiana na TCMP-Pwani kutekeleza, baadhi ya mambo mengine, mpango kazi wa mabadiliko ya tabia nchi na ufugaji wa viumbe bahari.

Mkurugenzi huyo aliwataka wajumbe wa ICM kutimiza wajibu wao bila kuwa kikwazo kwa wengine. "Kati ya sisi sote kila mtu ana nafasi yake, lakini tunafanya kazi kama timu moja," alisema na kuongeza kuwa "Tukishinda tunapaswa kushinda wote na kama tutashindwa, tunapaswa kushindwa wote. Lengo lisiwe kukwamishana, bali liwe kusaidiana".

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mradi TCMP-Pwani, Baraka Kalangahe, mradi una lengo la kuhakikisha kuwa mazingira ya pwani yanakuwa endelevu. "Tunalenga katika kuhakikisha kuwa yale ambayo tunayapata katika mazingira yetu ya pwani tunayadumisha. Kuhakikisha kuwa mwelekeo wa uharibifu wa mazingira ya pwani unapungua kwa kiasi kikubwa," alisema Kalangahe.

Alisema hilo linawezekana tu kwa kuhakikisha kuwa Mradi TCMP-Pwani unasaidia wananchi katika kuibua miradi yao wenyewe ya kuboresha maisha yao, ambayo kwa kiasi kikubwa haitegemei sana katika rasilimali za pwani. Shughuli hizo za kuboresha maisha pia zinapaswa kuzingatia kwa kiasi kikubwa kuhifadhi mazingira.

"Huwezi kuboresha maisha ya watu, wakazi wa maeneo ya pwani, huwezi kuzungumzia mambo ya kuhifadhi mazingira bila kumgusa mhifadhi mwenyewe," alisema Kalangahe.

Akizungumza kwa mifano, Kalangahe alisema "Huwezi kumshirikisha mtu katika kuhifadhi msitu akiwa ana njaa, kumshirikisha katika kuhifadhi bahari akiwa ana njaa".

Alisema mradi huo unafanya kazi katika ukanda wa pwani, katika wilaya za Bagamoyo na Pangani na eneo la Menai Bay huko Zanzibar. Pia alitaja kazi za Mradi huo wa miaka minne, kuanzia mwaka 2009 kuwa ni pamoja na kuhifadhi rasilimali za misitu, wanyama na mito, kuhifadhi bayoanuwai ya bahari na kulinda viumbe waliopo katika hatari ya kutoweka ambapo ni pamoja na kasa na nguva na samaki wengine na shughuli zinazomlenga binadamu moja kwa moja ambazo zinahusu masuala ya afya, mazingira, idadi ya watu, VVU/UKIMWI na kuinua uchumi wa wanajamii.

Katika suala la mabadiliko ya tabia nchi, kikundi kazi kilichoundwa kinatarajiwa kutekeleza shughuli za kubainisha vijiji vinavyokabiliwa na madhara ya mabadiliko ya tabia nchi ili kupata picha halisi ya ukubwa w atatizo wilayani humo na kubainisha vijiji viwili vya kutekeleza mradi wa majaribio wa kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabai nchi. Pia vijiji hivyo viwili vitashirikishwa katika kubuni miradi yao wenyewe ya kukabiliana na kupunguza athari za mabadiliko ya tabia nchi katika eneo lao.

Kwa upande wa ufugaji wa viumbe bahari, kikundi kazi kilichoundwa kitatekeleza shughuli za kubainisha vijiji ambavyo vina fursa za kuanzisha mabwawa ya kufugia samaki wa maji chumvi. Vijiji hivyo pia vitajengewa uwezo wa kuwa na utaratibu wa kutoa vibali kwa wafugaji wadogo wadogo wa samaki hao ili kuzuia kuendesha shughuli za ufugaji bila ya kuwa na utaratibu, na hivyo kukosa tija kwa walengwa na kuongeza shinikizo la uharibifu wa mazingira.

Pamoja na shughuli za mabadiliko ya tabia nchi na ufugaji wa viumbe bahari ambazo zinaanza kutekelezwa mwaka huu katika wilaya ya Pangani, mradi pia unatekeleza shughuli nyingine ambazo zilianza mapema mradi ulipoanza. Shughuli hizo ni pamoja na kusaidia wanajamii katika kukuza uchumi wao na mradi wa afya, watu na mazingira ambao una lengo la kuunganisha shughuli za afya, uzazi wa mpango na utunzanji wa mazingira. Mradi mwingine ni ule wa kuhifadhi kasa – moja ya viumbe waliopo katika hatari ya kutoweka na kuhifadhi rasilimali za misitu, wanyama na maji ya mito.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa TCMP-Pwani, mradi unatambua fika kuwa kila linalofanyika ni kwa ajili ya jamii ya watu wa Pangani, hivyo aliahidi mradi kuendelea kufanya kazi kwa karibu na jamii ili kuwapatia uwezo wa kuibua wao wenyewe vipaumbele vyao.

"Tutaboresha mawasiliano ili wanajamii kujua Mradi wa TCMP-Pwani unafanya nini ili tunapokwama tujue kwa pamoja ni jinsi gani tutatatua matatizo yetu," alisema. Tunatakiwa sote kwa pamoja tuwajibike katika kuhifadhi mazingira ya pwani. Tusipofanya hivyo tutaulizwa duniani na hata mbele ya haki; tumefanya nini kuhifadhi rasilimali ambazo tumepewa na Mwenyezi Mungu?," alihitimisha.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Wilaya ya Pangani ana imani kuwa kwa kufanya kazi na wajumbe wa ICM, vikundi kazi na wanajamii, shughuli za mradi zitaweza kufikia mafanikio yanayotakiwa.

"Inawezekana, timiza wajibu wako," alisema akimnukuu Rais wa Kwanza wa Tanzania, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. " Sisi sote tunaweza kama tutatimiza wajibu wetu." (END/2012)

 

 
 Latest News from Africa
News in RSS
XML error: The download of the specified resource has failed.
  Dernières Nouvelles
News in RSS
DEVELOPPEMENT: Nous devons penser autrement à la "sécurité"
AUSTRALIE: Le port de Newcastle bloqué par les Guerriers du changement climatique
IRAN: L’examen d’un document clé à l’AIEA suggère un coup d’Israël
PAKISTAN: Les Ahmadis confrontés à la mort ou à l’exil
ETATS-UNIS: Le budget de la défense peut accroître alors que le public est fatigué de la guerre
A lire également>>