Inter Press Service News Agency
Sunday, September 22, 2019   19:40 GMT    
   Homepage
   World Service
   East Africa
   Southern Africa
   West Africa
   Central Africa
 
   Environment
   Health-HIV/AIDS
   Education
   Rights
   Politics
   Economics
   and Finance
   Development
   Energy
   Population
   Culture
 
   Radio Service
 
   Français
 
   About IPS
 
   ENGLISH
   ESPAÑOL
   FRANÇAIS
   ARABIC
   DEUTSCH
   ITALIANO
   NEDERLANDS
   PORTUGUÊS
   SUOMI
   SVENSKA
   SWAHILI
   TÜRKÇE
PrintSend to a friend
Readers Opinions

Tanzania
Wanakijiji Waandaa Sheria Ndogo Kutunza na Kuhifadhi Maliasili za Pwani na Bahari
Na Marko Gideon

DAR ES SALAAM, Nov 17 (IPS) - Wanakijiji katika kijiji cha Kiharaka, Wilayani Bagamoyo wametunga sheria ndogo ya kutunza na kuhifadhi maliasili za Pwani na Bahari. Sheria ndogo ya kusimamia na kutunza mazingira ya kijiji cha Kiharaka, miongoni mwa madhumuni mengine, inataka kuwezesha na kuimarisha ushiriki wa wananchi katika kutunza, kutumia na kuhifadhi maliasili zilizopo katika kijiji cha Kiharaka.

Sheria hiyo ndogo ya kijiji cha Kiharaka imeandaliwa na wanakijiji kwa kujengewa uwezo na Ushirika wa Kusimamia Rasilimali na Mazingira ya Pwani na Bahari (TCMP) kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID) Madhumuni mengine ni kusaidia utunzaji wa ikolojia katika misitu ya pwani na bahari katika kijiji na kuchukuliwa kwa hatua za kisheria katika kusimamia maliasili zilizopo ikiwa ni pamoja na uwezo wa kutoa adhabu kwa wale wanaokiuka taratibu za usimamizi shirikishi wa mipango ya maliasili ya kijiji cha Kiharaka. Sheria hiyo ndogo inaunda kamati ya maliasili ambayo imepewa jukumu la kusimamia shughuli za maliasili kwa niaba ya serikali ya kijiji kwa kuhakikisha kuwa kikosi cha doria kimechagua kamanda wa doria na kwamba kinatekeleza wajibu wake ikiwa ni pamoja kwenda doria angalau mara nne kwa mwezi, kukutana angalau mara mbili kwa mwezi ikiwa ni pamoja na kutembelea misitu na maeneo tengefu ya bahari, kuwashughulikia watuhumiwa kwa mujibu wa kanuni, taratibu, sheria ndogo na sheria zote mama zinazohusu maliasili na mazingira. Kamati pia ina kazi ya kuweka takwimu na kutunza kumbukumbu sahihi za masuala yote yanayohusiana na utunzaji wa maliasili, kuandika na kutoa taarifa ya utekelezaji wa shughuli za maliasili kwa serikali ya kijiji na Halmashauri ya Wilaya na kuhamasisha wananchi kupanda miti nje na ndani ya hifadhi ya mikoko, katika mialo na kushiriki katika kuzima moto unapotokea.

Sheria pia inaipatia kamati jukumu la kuteua wawakilishi kufungua akaunti ya maliasili ambao saini zao ndizo zitakazotambulika benki kwa ajili ya kutoa fedha, kuhimiza na kusimamia uendelezaji wa kuhifadhi maliasili zilizopo na kukusanya, kudhibiti na kutolea taarifa za mapato na matumizi ya fedha za kamati na taarifa juu ya maendeleo ya uhifadhi wa maliasili kwa halmashauri ya kijiji na serikali ya kijiji. Usimamizi wa maliasili za pwani na bahari Katika suala la kusimamia maliasili za pwani na bahari, sheria inaweka bayana kuwa hakuna mtu yeyote atakayeruhusiwa kuingia ndani ya msitu wa hifadhi ya mikoko bila kibali kutoka ofisi ya mikoko ya wilaya ya Bagamoyo kupitia kamati ya maliasili ya kijiji. Hakuna mtu yeyote anayeruhusiwa na sheria hiyo ndogo kuvuna mikoko bila ya kuwa na leseni. Kwa upande wake jamii imepewa jukumu la kisheria la kutoa taarifa za uhalifu unaofanyika ndani ya msitu kwa serikali ya kijiji, uongozi wa kitongoji au kamati ya maliasili. Kwa mujibu wa sheria mtu yeyote atakayekutwa akivuna mbao, magogo, mijengo, kuwinda wanyama, kuchoma mkaa, kuchunga mifugo, kuanzisha njia, kuwa na silaha msituni, kuanzisha makazi, kufungua mashamba katika msitu wa hifadhi ya mikoko atakuwa amekwenda kinyume na sheria.

Pia si ruhusa kwa mtu au kikundi cha watu kuhamisha, kuharibu alama za mpaka au mpaka wa hifadhi ya mikoko na maeneo yaliyotengwa kwa shughuli maalum au vielelezo vilivyopo ndani ya msitu wa hifadhi ya mikoko, kuanzisha moto ndani ya msitu wa hifadhi au misitu mingine katika kijiji cha Kiharaka na mtu yoyote atakayetaka kuchoma moto shambani mwake atatakiwa kutoa taarifa kwa uongozi wa kijiji au kitongoji na kuorodheshwa kwenye daftari la kumbukumbu.

Kwa mujibu wa sheria hiyo, uvunaji wa mbao na mkaa utakaoruhusiwa nje ya msitu wa hifadhi ya mikoko kwa sheria ya misitu namba 14 ya mwaka 2002, atakayeruhusiwa kuvuna atatakiwa kutoa ushuru wa kijiji wa shilingi 300/= kwa kila kipande cha ubao na shilingi 400/= kwa gunia la mkaa.

Sheria hiyo pia imeliangalia suala la madini. Kwa mujibu wa sheria hiyo, mtu yeyote au kikundi cha watu au kampuni aliyepewa kibali cha kufanya uchunguzi wa madini ndani ya msitu wa hifadhi atatakiwa kulipa kijiji shilingi 10,000/= kila siku za utafiti. Iwapo eneo hilo litagundulika kuwa na madini kijiji kitafaidika na rasilimali hiyo kuwa na hisa ya asilimia 20% katika mradi huo.

Adhabu kwa wakiukaji wa sheria Kulingana na sheria hiyo, mtu, kikundi cha watu au kampuni yeyote itakayotenda kinyume na sheria ndogo hiyo atakuwa ametenda kosa na atapaswa kupewa adhabu. Moja ya adhabu zilizoanishwa na sheria hiyo ni pamoja na faini ya shilingi 20,000 au kwenda jela miezi sita au vyote kwa pamoja kama adhabu ya kukutwa na mijengo au fito au kuni ndani ya msitu wa hifadhi. Adhabu nyingine zilizoanishwa na sheria ndogo ya kijiji ni faini ya shilingi 50,000/= au kwenda jela miezi sita kwa mtu atakayefungua shamba au kuweka makazi ndani ya msitu wa hifadhi, kubomoa majengo yake na kuondoa mazao na kupanda miti kwenye eneo hilo. Pia adhabu kama hiyo itatolewa kwa mtu atakayekutwa akichoma mkaa ndani ya msitu, kusogeza au kubadili alama za msitu au kusogeza mpaka wa msitu, kuchoma moto na kukata miti na kupasua mbao. Adhabu inaongezeka kwa mtu atakayekutwa na hatia ya kuchimba mchanga, mawe, udongo au madini ndani ya msitu bila ya kibali au kuchunga mifugo ambapo atatozwa faini ya shilingi 100,000 au kwenda jela miezi sita au vyote kwa pamoja. Sheria muafaka, kwa wakati muafaka Sheria inakuja wakati ambapo suala la hifadhi ya mazingira limekuwa likipewa kipaumbele katika ajenda za maendeleo za serikali za mitaa, serikali za kitaifa na kimataifa kutokana na madhara makubwa yanayosababishwa na uharibifu wa mazingira kwa kizazi cha sasa na kijacho. Kwa mujibu wa Sera ya Mazingira ya Taifa ya Mwaka 1997, hifadhi ya mazingira ina malengo ya kuhakikisha matumizi endelevu na salama ya rasilimali na yanayozingatia usawa na mahitaji ya vizazi vya sasa na vijavyo bila kuharibu mazingira wala kuhatarisha afya za watu. Pia ina lengo la kuhifadhi mazingira na urithi wa asili na unaotokana na shughuli za binadamu ikiwa ni pamoja na viumbe mbalimbali na bayoanuwai ya kipekee nchini Tanzania. Sheria ya Mazingira ya Taifa ya mwaka 2004 inatoa haki na kuhimiza wajibu wa kutunza mazingira. Kwa mujibu wa sheria hiyo, kila mtu anayeishi nchini Tanzania ana haki ya kupata maji safi na mazingira salama na yenye afya. Kwa upande wa wajibu, sheria inasema kila mtu anayeishi nchini Tanzania ana wajibu wa kulinda na kihifadhi mazingira na kutoa taarifa kwa mamlaka husika juu ya shughuli yoyote au hali inayoweza kuathiri mazingira kwa kiasi kikubwa.Kwa upande wake, Mratibu wa Shughuli za upangaji na usimamiaji wa matumizi ya rasilimali za pwani na bahari wa TCMP, Alieth Mutatina, anasema sheria hiyo imekuja wakati ambapo kumekuwepo na uharibifu wa mazingira katika kijiji cha Kiharaka hasa msitu wa mikoko. "Kutokana na utafiti wa kutenga maeneo ya ufugaji wa viumbe wa bahari hasa samaki wa mabwawa uliofanyika mwaka 2010, tuligundua kuna uharibifu mkubwa wa mazingira ", anasema Mutatina. "Tukaamua kuhamasisha wananchi wa kijiji kipya cha Kiharaka ambacho kilimegwa kutoka kijiji cha Mapinga kutumia sheria ndogo ya kijiji cha Mapinga kutunga sheria yao." Sheria hiyo itapitia ngazi mbalimbali kabla haijapitishwa kuwa sheria kamili. Kutoka katika ngazi ya kijiji itakwenda katika ngazi ya timu ya kiufundi ya wilaya, halafu timu ya mazingira na maliasili ya madiwani wa wilaya ya Bagamoyo na mwisho itapitishwa na mkutano mkuu wa halmashauri ya wilaya. Kuandaa sheria ndogo ndogo kama ya kijiji cha Kiharaka ni miongoni mwa shughuli zinazofanywa na TCMP katika kusaidia serikali za mitaa kutekeleza Mkakati wa Kitaifa wa Kusimamia Mazingira ya Pwani (NCS) wa mwaka 2003. (END/2011)

 

 
 Latest News from Africa
News in RSS
XML error: The download of the specified resource has failed.
  Dernières Nouvelles
News in RSS
DEVELOPPEMENT: Nous devons penser autrement à la "sécurité"
AUSTRALIE: Le port de Newcastle bloqué par les Guerriers du changement climatique
IRAN: L’examen d’un document clé à l’AIEA suggère un coup d’Israël
PAKISTAN: Les Ahmadis confrontés à la mort ou à l’exil
ETATS-UNIS: Le budget de la défense peut accroître alors que le public est fatigué de la guerre
A lire également>>