Inter Press Service News Agency
Sunday, September 22, 2019   19:48 GMT    
   Homepage
   World Service
   East Africa
   Southern Africa
   West Africa
   Central Africa
 
   Environment
   Health-HIV/AIDS
   Education
   Rights
   Politics
   Economics
   and Finance
   Development
   Energy
   Population
   Culture
 
   Radio Service
 
   Français
 
   About IPS
 
   ENGLISH
   ESPAÑOL
   FRANÇAIS
   ARABIC
   DEUTSCH
   ITALIANO
   NEDERLANDS
   PORTUGUÊS
   SUOMI
   SVENSKA
   SWAHILI
   TÜRKÇE
PrintSend to a friend
Readers Opinions

TANZANIA
SACCOS Zinavyosaidia Jamii za Pwani Kuhifadhi Mazingira, Kupambana na Umaskini
Na Marko Gideon

PANGANI, Oct 10 (IPS) - Miradi inayobuniwa kuhifadhi mazingira inaweza pia kuboresha kipato na kupunguza umaskini miongoni mwa jamii za pwani ya mashariki mwa Tanzania. Hii inatokana na kuhamasisha jamii hizo kutumia rasilimali za pwani na bahari kwa uangalifu zaidi.

Hata hivyo, miradi mingi ya aina hiyo inakabiliwa na kukosekana kwa mtaji wa kuiendesha na hivyo kufanya Vyama vya Kuweka na Kukopa (SACCOS) kuwa ufumbuzi wa kufadhili miradi hiyo.

Mradi wa Pwani unaoendeshwa na Ushirika wa Kusimamia Rasilimali za Pwani na Bahari (TCMP-Pwani), uliopo chini ya serikali ya Marekani kupitia USAID, serikali ya Tanzania kupitia Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) na Kituo cha Rasilimali za Pwani cha Chuo Kikuu cha Rhode, miongoni mwa mambo mengine, unatumia SACCOS kupunguza umaskini na kuinua hali ya maisha ya jamii kama njia ya kukabiliana na moja ya changamoto kubwa za kusimamia na kuhifadhi mazingira na rasilimali za pwani na bahari.

Kwa mujibu wa mkurugenzi wa ushirika huo, Jerremiah Daffa, Mradi wa Pwani unajishughulisha na maeneo makuu matatu- kuhifadhi mazingira na rasilimali za pwani, kuhifahi mazingira na rasilimali za bahari na kusaidia shughuli za kuinua kipato na kuboresha maisha ya watu. Katika eneo la kusaidia shughuli za kuinua kipato na kuboresha maisha ya watu, mradi wa Pwani umesaidia kuunda, kuanzisha na hata kufufua SACCOS kadhaa katika vijiji vya pwani kwenye wilaya za Bagamoyo, Pangani na Zanzibar. Hata hivyo, moja ya habari za mafanikio ni ile ya SACCOS ya Songambele katika kitongoji cha Sakura, kijiji cha Kwakibuyu wilayani Pangani.

Kwa mujibu wa mwenyekiti wa SACCOS hiyo, Salum Juma Lukindo, walianza mwaka 2008 wakiwa na shilingi za Kitanzania 800,000 na wanachama 7, lakini sasa wana mtaji wa zaidi ya shilingi milioni 22 na wanachama 106 baada ya kufanya kazi kwa miaka mitatu tu.

"Tunasaidia wanajamii wa vijijini wenye kipato cha chini, wanawake kwa wanaume ambao wanaweza kuathirika zaidi na kupungua kwa rasilimali za pwani na bahari kunakosababishwa na matumizi ya kupita kiasi na mabadiliko ya taifa nchi. Tunahitaji ufumbuzi wa kuhifadhi mazingira na rasilimali za pwani na bahari kuhusisha pia watu hawa," anasema Meneja wa Ukuaji wa Uchumi na Kuboresha Maisha ya Watu wa TCMP Pwani, Patrick Kajubili.

SACCOS ya Songambele ambayo imeanzishwa na wanakijiji wengi kutoka vijiji vya Kwakibuyu (Sakura) na Kipumbwi ambayo ilifaidika na fedha ya mbegu ya jumla ya shilingi milioni 2 kutoka TCMP, inatoa ruzuku kusaidia miradi kadhaa ya kuboresha maisha na kupunguza umaskini ambayo ni rafiki wa mazingira. Miradi hiyo ni pamoja na ufugaji wa nyuki, biashara ndogondogo, kilimo na ufugaji endelevu wa mifugo na kuku.

"Miradi inayofadhiliwa na TCMP inapunguza shinikizo la matumizi ya kupindukia ya rasilimali za pwani na bahari ikiwa ni pamoja shughuli zisizokuwa endelevu kama vile uvuvi wa kutumia mabomu na nyavu kubwa, uchomaji wa mkaa na kusafisha misitu kwa ajili ya kilimo cha mazao," anasema Lukindo.

SACCOS hiyo pia imeanzisha mpango wa upandaji miti ili kuhifadhi mazingira na wakati huo huo kuwaingizia wanachama kipato kinachotokana na mpango wa kupunguza hewa ukaa kwa kupanda miti (REDD).

"Tunatarajia hadi Februari mwaka ujao tutakuwa na kitalu cha miti,"anasema Lukindo. "Pia tunaunga mkono jitihada za mtu mmoja mmoja za kupanda miti ili kuhifadhi mazingira. Wanachama wetu wengi wana mashamba yao ya miti."

Miradi hii iliyojikita katika jamii pia ina lengo la kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi ambayo yanaelezwa kuwa moja ya changamoto kubwa zaidi za maendeleo ya jamii za pwani.

Lakini, isingekuwa rahisi kuendesha miradi hii bila ya kutumia SACCOS. Kuhakikisha mitaji inapatikana kwa urahisi miongoni mwa wakazi wa vijijini ni njia muhimu katika kuboresha maisha, kupunguza umaskini na pia kuhifadhi mazingira na kufanya miradi ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kutekelezwa hata katika ngazi ya kijiji.

Wakati karibu asilimia 80 ya Watanzania wanaishi katika maeneo ya vijijini ambako wanakabiliwa na ugumu wa kupata mikopo ya benki, SACCOS ni njia pekee ya kuwafanya waweze kuendesha maisha yao wakati huu wa mabadiliko ya mara kwa mara ya hali ya hewa na kupungua kwa rasilimali za pwani na bahari.

"Ni jambo jema kuona kuwa watu hawa wanaweza watu hawa wanaweza kuendesha maisha yao kama kawaida hata baada ya rasilimali za pwani na bahari zikiwa zimepungua kwa kiasi kikubwa," alisema raia wa Ghana Felix Nani wakati wa ziara ya mafunzo ya jinsi ya kusimamia na kuhifadhi vizuri mazingira ya pwani na bahari yaliyoandeshwa na TCMP Juni 2011.

Suala la hifadhi ya mazingira limepewa kipaumbele cha juu kitaifana kusisitizwa na mikakati na programu mbalimbali za maendeleo na hata viongozi katika ngazi ya mtaa na hata taifa.

"Ni maelekezo kutoka kwa Mungu kuwa tukaitumie ardhi na kuitunza, kama tukishindwa kufanya hivyo hakika tunapaswa kujiandaa na janga linalokuja," alisema rais wa zamani wa Tanzania, Banjamin Mkapa hivi karibuni.

Kulingana na Kajubili, zaidi ya wanakijiji 400 kutoka vijiji kadhaa vya Bagamoyo, Pangani na Zanzibar wanafaidika kiuchumi kutokana na miradi ya kusimamia rasilimali za pwani na bahari ambazo zina lengo la kuboresha maisha yao chini ya mradi wa miaka minne wa TCMP Pwani ambao unamaliza muda wake mwaka 2013. Wanavijiji hao, ambao wengi wao ni wanawake, wamejiunga katika vikundi vya wakulima wa mwani, biashara ndogondogo, ufugaji wa nyuki, utengenezaji wa mapambo na wakulima wa nusu lulu, uvuvi na ufugaji mifugo.

"Lengo la mwaka kesho ni kuongeza ushiriki wa jamii za wafugaji katika mradi ili kukuza moyo wa hifadhi ya mazingira miongoni mwa jamii hii", anasema Kajubili, akiongeza kuwa moyo wa hifadhi ya mazingira unakosekana miongoni mwa kundi hili kutokana na kukosekana kwa elimu na mtaji wa kuendesha shughuli mbadala za kujiingizia kipato ambazo ni muhimu katika hifadhi ya mazingira.

"Wakati huo huo tunataka kuanzisha mkakati wa kusaidia jamii za wavuvi kuongeza thamani ya bidhaa zao, kuhamasisha uuzaji bidhaa zao katika vyama vya ushirika na kuwafanya kuwa na sauti moja wakati wanapouza bidhaa zao," anaongeza Kajubili.

Kazi kubwa ya mradi wa TCMP Pwani ni kuwezesha uundwaji wa vikundi hivyo na kupatiwa usajili wa kudumu ili vitambulike kisheria, kutoa ruzuku kama mtaji wa awali na kuvijengea uwezo kupitia mafunzo kwa wanachama wa vikundi ya jinsi ya kutunza mahesabu, vitabu vya fedha, ujasiriamali, kusimamia biashara, njia bora za utunzaji wa mazingira na pia dhana ya uhusiano kati ya idadi ya watu, afya na mazingira.

"Wanachama wa SACCOS ni miongoni mwa walengwa wa mafunzo yanayotolewa chini ya mradi wa idadi ya watu, afya na mazingira (PHE), dhana ya maendeleo ambayo inataka kuendeleza uhusiano uliopo kati ya idadi ya watu, afya na mazingira na mabadiliko ya kiuchumi kwa ujumla wake ili kuboresha ustawi wa jamii ya watu wanaoishi katika maeneo yenye utajiri mkubwa wa rasilimali za bahari na ambao wanategemea rasilimali za pwani na bahari kwa ajili ya chakula, kipato na bidhaa nyingine na huduma," anasema meneja mradi wa Idadi ya Watu, Afya na Mazingira katika TCMP, Juma Dyegula.

"PHE ina lengo la kuzifanya jamii hizo kupata huduma endelevu za uzazi wa mpango na afya ya uzazi wakati huo huo ikiboresha usimamiaji wa maliasili katika njia ambayo inaboresha maisha yao na kutunza mazingira ambayo wanayategemea", anaongeza.

PHE inafaa zaidi kutumika katika nchi ambapo kuna ongezeko kubwa la idadi ya watu ambalo limesababisha kuharibu bayoanuwai na mazingira yanayotegemewa na binadamu na viumbe hai.

Mbali ya shughuli za ukuaji wa kiuchumi na kuboresha maisha ya watu, mradi wa TCMP Pwani pia unatekeleza idadi kadhaa ya miradi chini ya Mpango Mkakati wa Kitaifa wa Kusimamia Mazingira ya Pwani na Bahari kwa kuhamasisha wananchi wanaoishi katika vijiji vya pwani ya bahari ya Hindi kuhifadhi mazingira ya pwani kuzuia uharibifu na kupunguza shinikizo la kutegemea kwa kiasi kikubwa rasilimali za pwani na bahari. (END/2011)

 

 
 Latest News from Africa
News in RSS
XML error: The download of the specified resource has failed.
  Dernières Nouvelles
News in RSS
DEVELOPPEMENT: Nous devons penser autrement à la "sécurité"
AUSTRALIE: Le port de Newcastle bloqué par les Guerriers du changement climatique
IRAN: L’examen d’un document clé à l’AIEA suggère un coup d’Israël
PAKISTAN: Les Ahmadis confrontés à la mort ou à l’exil
ETATS-UNIS: Le budget de la défense peut accroître alors que le public est fatigué de la guerre
A lire également>>