Inter Press Service News Agency
Sunday, September 22, 2019   20:07 GMT    
   Homepage
   World Service
   East Africa
   Southern Africa
   West Africa
   Central Africa
 
   Environment
   Health-HIV/AIDS
   Education
   Rights
   Politics
   Economics
   and Finance
   Development
   Energy
   Population
   Culture
 
   Radio Service
 
   Français
 
   About IPS
 
   ENGLISH
   ESPAÑOL
   FRANÇAIS
   ARABIC
   DEUTSCH
   ITALIANO
   NEDERLANDS
   PORTUGUÊS
   SUOMI
   SVENSKA
   SWAHILI
   TÜRKÇE
PrintSend to a friend
Readers Opinions

TANZANIA
Ujasiriamali Unaozingatia Utunzaji wa Mazingira
Na Marko Gideon

BAGAMOYO, Julai 15, 2011 (IPS) - Juni 15, 2011 itakuwa siku ya kukumbukwa na wanawake na wanaume wa kijiji cha Mkange, kata ya Mkange wilayani Bagamoyo. Ni siku ambayo kulikuwa na uzinduzi rasmi wa UWAMKE (Ukombozi wa Wanawake Mkange) SACCOs – kikundi cha kuweka na kukopa kinachotarajiwa kuboresha maisha ya wananchi wa kijiji hicho na vijiji vya jirani ikiwa ni pamoja na kuhifadhi mazingira kwa ajili ya vizazi vijavyo.

Akizungumza wakati wa makabidhiano ya hundi ya sh. milioni moja kama fedha za mbegu kuongeza mtaji wa SACCOs hiyo, mratibu wa mradi kutoka Ushirika wa Kusimamia Hifadhi ya Mazingira na Rasilimali za Pwani na Bahari (TCMP), Bw Patrick Kajubili alisema kwa kuanzia Saccos hiyo itapatiwa fedha hizo ili kuwezesha wanachama kuendesha shughuli za kujipatia kipato na wakati huo huo wakijali utunzaji wa mazingira na rasilimali za pwani na bahari.

"Nia ni kuanzisha shughuli mbalimbali ambazo zitawaingizia kipato na wakati huo huo zikiwa pia ni rafiki wa mazingira," alisema Bw Kajubili, na kuongeza kuwa TCMP haiungi mkono shughuli zinazoharibu mazingira au zinazoangamiza rasilimali za pwani na bahari. Alizitaja shughuli ambazo TCMP inazipiga vita kuwa ni pamoja na biashara ya kuchoma mkaa, kutumia njia za uvuvi haramu au kuchoma moto ovyo wakati wa kusafisha mashamba kwa ajili ya kilimo.

Aliwaasa wananchi juu ya athari zinazotokana na uharibifu wa mazingira ambazo zinadhihirishwa wazi na kasi ya mabadiliko ya tabia nchi hata katika kata ya Mkange.

"Mabadiliko ya tabia nchi yanakuja kwa kasi kubwa. Hata Mkange ya miaka ya 80 ni tofauti na Mkange ya sasa," alisema. "Miaka ya nyuma inawezekana ilikuwa vigumu kufika nyumba ya jirani kwani lazima kungekuwa na kichaka, lakini sasa hali ni tofauti, mvua ni chache, alisema na kuitikiwa na wanachama na wananchi kwa njia ya ishara.

Aliwataka wakate mti, wapande miti ili watunze mazingira kwa ajili ya kuachia watoto urithi wa nchi. Aliwaasa kuwa hata kama wangewaachia watoto wao urithi wa elimu, bado hautatosha kwani hawataweza kula elimu.

"Hatutatarajii baada ya kupata fedha za TCMP unasema sasa naenda kuchoma gunia 50 za mkaa kwa ajili ya kupanua biashara yangu ya kuuza mkaa," alitahadharisha. "Ni lazima wana SACCOs kubuni shughuli za ujasiriamali ambazo ni rafiki wa mazingira," alisisitiza alipokuwa akizungumza na wanachama wa SACCOs hiyo ambao wengi wao ni wanawake siku moja kabla ya uzinduzi rasmi.

Kulingana na mwenyekiti wa SACCOs ya UWAMKE, Bi Mashavu Saidi, kikundi chake kimekuwa na historia ndefu kidogo hadi kilipofikia hapo kilipo sasa. Alisema wazo la kuwa na chombo kama hicho lilikuja baada ya yeye kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) kata ya Mkange mwaka 2009 ambapo aliwaomba wanawake wenzake kuunda kikundi cha kuweka na kukopa ili waweze kujikwamua kiuchumi na kuboresha maisha yao.

"Tulianza na wanawake 17 na tulikuwa tukichangia kila mmoja shilingi 1000. Awali tulianza kukopesha wanachama 5 kila mmoja shilingi 20,000. Baada ya kurejesha baada ya miezi 3, wanawake wengine walipewa katika mzunguko huo," alifafanua Bi Saidi.

Alisema waliendelea katika hali kama hiyo ya kukopeshana hadi mtaji ukawa na uwezo wa kukopesha wanachama 20 kwa wakati mmoja na kiwango cha juu cha kukopa kikawa sh. 40,000.

"Baada ya kufikia hatua hiyo ndipo tukakutana na mratibu wa miradi wa TCMP ambaye nilimweleza juu ya kikundi chetu na haja ya kuwa na SACCOs iliyosajiliwa rasmi," alielezea Bi Saidi.

Alisema hadi TCMP inawapatia hundi tayari wameshakuwa na mtaji wa jumla ya sh. 1,980,000 katika kikundi chao.

Alisema yeye kama mmoja wa wanachama wanaofaidika na SACCOs hiyo, ameweza kumsaidia mume wake ambaye ni mvuvi kusomesha watoto wao 4 wa kike katika shule za sekondari. "Nashukuru sasa namsaidia mzee katika malezi," alisema Bi. Saidi.

Kulingana na Bw Kajubili, katika awamu ya kwanza TCMP ingeipatia SACCOs kiasi hicho cha shilingi milioni moja kuongeza katika mtaji wao. Kama kikundi kitafanya vizuri kwa asilimia 95 kulingana na vigezo vilivyopo katika mkataba uliosainiwa baina ya TCMP na SACCOs, kiasi kingine cha shilingi milioni moja kitaongezwa.

" TCMP inasaidia tu kuongeza mtaji katika jitihada zenu za kutekeleza miradi inayozingatia uendelezaji wa rasilimali na kuhifadhi mazingira ya Pwani na Bahari," Bw. Kajubili aliwaambia wanachama.

SACCOs endelevu, mazingira endelevu

Mitaji inayotolewa na TCMP, ushirika wa serikali ya Tanzania kupitia Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) lililopo chini ya Ofisi ya Makamu wa Rais, serikali ya Marekani kupitia Shirika la Misaada ya Maendeleo ya Kimataifa (USAID) na Kituo cha Rasilimali za Pwani (CRC) cha Chuo Kikuu cha Kisiwa cha Rhode, pia ina lengo la kufanya shughuli za wananchi zinazozingatia hifadhi ya mazingira kuwa endelevu.

"Tunafanya kazi kwa karibu na serikali ya wilaya kuhakikisha miradi yenu inakuwa endelevu," Kajubili aliwahakikishia wanachama, huku akifafanua zaidi kuwa "Mratibu wa Uhifadhi wa Mazingira na Rasilimali za Pwani wa wilaya ya Bagamoyo ndiye mratibu wa SACCOs ili hata kama Mradi wa Pwani uliopo chini ya TCMP ukifikia ukomo, serikali ya wilaya inaweza kuendelea kuunga mkono shughuli SACCOs.

Matamshi ya Bw Kajubili yaliungwa mkono pia na mkuu wa wilaya ya Bagamoyo, Bw. Mlongo Magessa. Alipokuwa akihutubia wanachama na wananchi wa kata ya Mkange waliohudhuria uzinduzi huo, alionyesha kuunga mkono kwa vitendo jitahada hizo kwa kuahidi ofisi ya wilaya kutoa mchango wa shilingi laki nne (400,000).

"Muungano wenu una tija leo na siku zijazo …Serikali inasema hatuwezi kuwapa hela mtu mmoja mmoja, ila mkiungana ni rahisi kuwasaidia kwani mna jina, anuani, historia na ufadhili wa kwanza," alisema Bw. Magessa.

Aliwataka wanachama kufanya juhudi za makusudi na za pamoja kuhakikisha kuwa SACCOs inafikisha lengo la asilimia 95 ili iweze kupata pesa nyingine. "Msipofanya hivyo pesa zitaenda kwa wengine."

Akisisitiza juu ya suala la kuhakikisha SACCOs inakuwa endelevu, Bw Magessa alisema "Tutafanya kazi kwa karibu sana na SACCOs zinazoanzishwa, inawezekana wanachama tukafa lakini SACCOs ikabaki."

Alisema SACCOs nyingi zinakufa kutokana na uroho, ubinafsi na uongozi usiofuata kanuni. Mambo yanaweza kwenda kinyume kama kila mmoja anataka kuwa mkubwa – kuwa mbabe. Pia alitaja suala la kulipa madeni kuwa tatizo la SACCOs nyingi.

Akitoa mfano alisema wilaya ya Bagamoyo ilikuwa na jumla ya SSCCOs 97 siku za nyuma, lakini hadi sasa SACCOs hai hazifiki 30. "Wengine [wakati wa] kurudisha wanakuwa wababe hawataki kubishiwa mlango. Ukijua kwenda kuchukua lazima ujue pia kurudisha," alisema.

Katika kusisitiza suala la uendelevu, Mkuu wa Wilaya hiyo ilibidi awe mkali kidogo. Alisema kwa sasa serikali itatumia sheria kuwabana wanaokwenda kinyume na matakwa ya SACCOs.

"Ukifanya kinyume sheria inachukua mkondo wake," alisema na kuongeza, "watakaopata misaada ya wafadhili au serikali na kuitumia vibaya hatutawaacha watambe. Tukirudi tutawataka kujibu kutokana na msaada mmefanya nini?"

Kwa TCMP "tunaahidi kulinda mchango wenu ili siku moja mkipita muone mabadiliko. Nawaahidi mabadiliko yatafikiwa iwe kwa hiari ama kwa kutumia nguvu," alisema Bw Magessa. (END/2011)

 

 
 Latest News from Africa
News in RSS
XML error: The download of the specified resource has failed.
  Dernières Nouvelles
News in RSS
DEVELOPPEMENT: Nous devons penser autrement à la "sécurité"
AUSTRALIE: Le port de Newcastle bloqué par les Guerriers du changement climatique
IRAN: L’examen d’un document clé à l’AIEA suggère un coup d’Israël
PAKISTAN: Les Ahmadis confrontés à la mort ou à l’exil
ETATS-UNIS: Le budget de la défense peut accroître alors que le public est fatigué de la guerre
A lire également>>