Inter Press Service News Agency
Thursday, June 21, 2018   09:51 GMT    
   Homepage
   World Service
   East Africa
   Southern Africa
   West Africa
   Central Africa
 
   Environment
   Health-HIV/AIDS
   Education
   Rights
   Politics
   Economics
   and Finance
   Development
   Energy
   Population
   Culture
 
   Radio Service
 
   Français
 
   About IPS
 
   ENGLISH
   ESPAÑOL
   FRANÇAIS
   ARABIC
   DEUTSCH
   ITALIANO
   NEDERLANDS
   PORTUGUÊS
   SUOMI
   SVENSKA
   SWAHILI
   TÜRKÇE
PrintSend to a friend
Readers Opinions

VVU/UKIMWI
Kukataliwa Ufadhili Kwawatia Wasiwasi Wanaharakati
Lameck Masina

BLANTYRE, Malawi, Jan 3 (IPS) - Wanaharakati wa masuala ya afya nchini Malawi wameonyesha wasiwasi wao juu ya tukio la hivi karibuni la kukataliwa kwa mchanganuo wa mradi wa nchi hiyo wa karibu dola milioni mia sita uliopelekwa kwa Mfuko wa Kimataifa wa Kupambana na VVU, Kifua kikuu na Malaria kati ya mwaka 2011 na 2016.

Lakini serikali inazidi kusisitiza kuwa hakuna haja ya kuwa na wasiwasi. Katibu Mtendaji wa Kamati ya Uratibu wa Mfuko wa Dunia nchini Malawi Edith Mkawa aliwaambia waandishi wa habari Jumanne iliyopita katika mji mkuu wa Lilongwe kuwa mchanganuo wa nchi hiyo ulikataliwa tena.

Mchanganuo ulilenga zaidi katika kukabiliana na maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto kwa kutoa tiba ya kurefusha maisha kwa wanawake wote wenye mimba ambao wanaishi na VVU. Malawi ilikuwa na matarajio ya kupanua usambazaji wake wa madawa ya ARVs kutoka 287,000 hadi 537,000 ifikapo mwishoni mwa mwaka wa fedha.

Malawi pia ilikuwa na mpango wa kupanua huduma ya kutahiri kwa hiari wanaume ili kusaidia kupunguza maambukizi ya VVU ambayo yamekalia katika asilimia 12 tangu mwaka 2007. Karibu wanaume milioni moja wangetahiriwa katika kipindi cha utekelezaji.

Mkawa alisema hakuna sababu zilizotolewa za kukataliwa kwa mchanganuo. "Bado hatujapokea sababu za ni kwa nini mchanganuo wa mradi umekataliwa na chombo hicho cha dunia," aliwaambia waandishi wa ndani. Hata hivyo, kwa baadhi kukataliwa huko hakujawashangaza.

Shirika la huduma za kibinadamu la kimataifa la Médecins Sans Frontières (MSF), ambalo linajulikana kama Madaktari Wasiokuwa na Mipaka, lilishatoa tahadhari katika makala yake kwenye tovuti Desemba 8 kuwa kutokana na kupungua kwa bajeti, nchi kadhaa za Afrika "zinaweza kushindwa kupata fedha za mfuko wa VVU/UKIMWI siku za usoni za karibu".

"MSF ina wasiwasi mkubwa kuwa nchi kadhaa za kipato cha chini zenye maambukizi makubwa ya VVU kama vile Malawi, Zimbabwe, Msumbiji, Swaziland na Lesotho zina hatari ya kunyimwa ufadhili wa VVU na Kifua Kikuu katika awamu hii," inasomeka sehemu ya makala hiyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Malawi Health Equity Network, Martha Kwataine, anasema habari hizo zinakatisha tamaa. "Madhara yake ni makubwa. Asilimia ipatayo 90 ya shuguli za VVU nchini Malawi zinategemea fedha za wafadhili. Hivyo hii ina maanisha kuwa kutakuwa na kikwazo katika kupambana na VVU.

Matokeo yake tunaweza kuona takwimu zetu za VVU zikipanda tena ", anasema. Kwataine anasema hali ya sasa inatakiwa kuwa na tahadhari kwa upande wa serikali ili kuzuia kutegemea zaidi fedha za wafadhili.

"Hatuwezi kuegemea kwenye fedha za wafadhili. Na hawa ni watu wetu ambao wanahitaji ARVs wakati wote. Mara zote nilisema kuwa Wamalawi siyo watu wa Mfuko wa Kimataifa. Ni watu wa serikali. Serikali inawajibika kutoa huduma za afya kwa wananchi wake ", anasema.

VVU/UKIMWI umehusishwa na asilimia 59 ya vifo miongoni mwa wananchi wenye umri kati ya miaka 15 hadi 59 nchini Malawi, ambayo ina wakazi wapatao milioni 13. Kulingana na Kwataine kukataliwa huko kutahatarisha haki ya watu wengi wa Malawi.

"Hiyo ni hatari mno kwasababu kama unasitisha kutumia ARVs kwa kipindi cha miezi mitatu zinakuwa sugu na wanaishia kufariki. Kwa upande mwingine, tumekubaliana na mwongozo wa WHO. Sasa ni jinsi gani tutatekeleza miongozo mipya? Ni changamoto ya kweli kwasababu hatutapiga hatua yoyote mbele," anasema.

Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Taifa cha Watu Wanaoishi na VVU/UKIMWI nchini Malawi, Amanda Manjolo, anasema kukataliwa kupewa fedha hizo kutakuwa na madhara makubwa katika maisha ya wale ambao wanatumia ARVs.

"Kutokana na kwamba lengo kuu la mchanganuo huo ni kuhusu ununuzi wa ARVs, hii ina maana kuwa kutakuwa na uhaba wa ARV katika siku zijazo", anasema.

Akikubaliana na Kwataine, Manjolo anasema hii itaathiri mpango wa serikali wa kuzingatia miongozo mipya ya WHO kuwa watu wanapaswa kuanza kutumia ARVs wakati kiwango chao cha chembe za CD4 ni 350.

Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais na baraza la mawaziri anayeshughulikia Programu za Lishe na VVU/UKIMWI, Mary Shawa, anakanusha hofu hizo.

"Pamoja na kwamba hayo ni matokeo ya kusikitisha, kukataliwa kwa mchanganuo hakutakuwa na madhara ya mara moja kwasababu kwa sasa tuna rasilimali za kutosha kutupeleka hadi mwaka 2012. Lakini tunachukulia suala hilo kama tahadhari kwasababu tunahitaji kuendelea kutoa ARVs kwa watu wenye VVU", anasema.

Shawa anasema serikali ina mikakati ya kutafuta wafadhili ambao siyo wa jadi ili kurejesha programu ya VVU. Kama ilivyo kwa nchi nyingine katika kanda ya SADC, Malawi imeanza kutoa tiba kwa wanawake wenye VVU kulingana na mapendekezo ya WHO kuhusu CD4 kuwa 350, lakini kiasi cha kawaida cha idadi ya CD4 ili kuanza ARV inabakia kuwa 250.

"Tutaendelea na miongozo ya WHO. Tuna fedha za kutosha ambazo tumezipata kutoka kwa wafadhili wengine, ikiwa ni pamoja na Benki ya Dunia na DFID", anasema Shawa.

Kulingana na Mfuko wa Dunia, ni michanganuo 79 tu kati ya 150 imepewa fedha mwaka huu. Nchi nyingine ambazo zimenyimwa ufadhili ni Swaziland, Msumbiji, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Zimbabwe.

Zimbabwe, kama ilivyo kwa Malawi, imekuwa ikipata msaada wa Mfuko wa Kimataifa tangu mwaka 2002.

Manjolo anasema kutokana na pengo la ufadhili, ambalo limetokana na Mfuko wa Dunia, watu wenye VVU nchini Malawi wanaweza kuteseka zaidi na magonjwa nyemelezi na hata kufariki mapema. Ametoa wito wa kuanzishwa kwa haraka kwa duru mpya ya ufadhili kuruhusu michanganuo iliyokataliwa kuwasilishwa tena. (END/2011)

 

 
 Latest News from Africa
News in RSS
XML error: The element 'html' is used but not declared in the DTD/Schema.
  Dernières Nouvelles
News in RSS
DEVELOPPEMENT: Nous devons penser autrement à la "sécurité"
AUSTRALIE: Le port de Newcastle bloqué par les Guerriers du changement climatique
IRAN: L’examen d’un document clé à l’AIEA suggère un coup d’Israël
PAKISTAN: Les Ahmadis confrontés à la mort ou à l’exil
ETATS-UNIS: Le budget de la défense peut accroître alors que le public est fatigué de la guerre
A lire également>>