KUSINI MWA AFRIKA Vijana Rahisi Kujiingiza Kwenye Ghasia Zukiswa Zimela na Kelvin Kachingwe
JOHANNESBURG na LUSAKA, Jul 23 (IPS) - James Banda, 27, ni kijana ambaye hana ajira moja na kuna wakati anaajiriwa kwa muda kama kondakta wa basi katika Kituo cha Mabasi cha Kulima Tower mjini Lusaka. Inawezekana hana kazi ya kudumu, lakini ni rahisi kumpata. Kila mtu anayemhitaji inabidi kwenda kwenye kituo cha mabasi na kuuliza. Kila mtu anajua yupo wapi. Banda, au kama watu wanavyomwita ‘ba-Jay', ni kijana ambaye anaheshimika mno kwa marafiki.
Anaweza kushindwa kupata ajira kwa mwaka mzima, lakini wakati wa uchaguzi Banda anakuwa kijana ambaye huduma yake inahitaji mno. Anaajiriwa na marafiki zake na vyama mbalimbali vya siasa kufanya kampeni.
Lakini Banda siyo mwanachama wa chama chochote cha siasa. Na aina ya kampeni anazoajiriwa kufanya hazihusiki na kuelezea sera kwa wapiga kura lakini zinahusu kutishia wapinzani na wapiga kura. Maafisa wa chama wanampatia yeye na marafiki zake fedha, pombe na kukodisha gari kusafiri nao kuzunguka katika majimbo kuvuruga mikutano ya vyama pinzani na kutishia wapiga kura wa upinzani.
Wakati makada wa upinzani au wapiga kura wao wanapojibu mapigo, aidha wanawapiga au kuwatishia kwa mapanga.
"Kazi yetu ni rahisi, ni kushawishi tu watu kwa njia yoyote ile kupiga kura kwa chama tunachokiunga mkono katika uchaguzi huo. Chama chochote kinachokuwa cha kwanza, na ambacho kina fedha nzuri, tunaondoka," anasema.
Banda, kama ilivyo kwa vijana wengine katika miji mikubwa wanakosa fursa za ajira na hivyo sababu ni kwa nini wanaruhusu kutumiwa kufanya ghasia za kisiasa.
Na utafiti unaonyesha kuwa yeye hayupo pekee.
Ripoti ya shirika la Southern Africa Trust ‘Ending the Age of Marginal Majority', iliyotolewa Julai 20 iligundua kuwa vijana wengi katika Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) walikuwa wakikabiliwa na ghasia kama waathirika au wachochezi wa ghasia hizo wakati hawana mifumo wala mitandao ya kuiunga mkono.
Utafiti ulibainisha kuwa kanda ya SADC imekuwa na sifa ya ghasia na vita na ghasia hizi zimekuwa sehemu ya kawaida ya jamii katika kanda. Matokeo yake "ni mara chache sana watu wanaoshiriki au kuathirika na aina hii ya ghasia kama wahalifu."
Emily Mabusela, meneja mipango wa Mpango wa Kuzuia Ghasia kwa Vijana katika Kituo cha Utafiti wa Ghasia na Maridhiano anasema kuwa moja ya sababu ya vijana kusababisha ghasia ni kutokana na asili ya vitendo vya ghasia katika jamii yetu.
"Ghasia zipo katika kila mahali, majumbani, katika jamii zetu na mashuleni watoto wetu wanauawa, hatuwezi kuzuia. Tunawafundisha vijana nini wakati wanaona ubaguzi wa raia wa mataifa mengine na ghasia za ghadabu kubwa barabarani?" anauliza.
Mabusela alisema kama hatua hazitachukuliwa vijana wanaofanya fujo watakua wakiwa watu wazima wenye fujo.
"Kuwa na fujo ni kama kujifunza kusoma, wakati unapokuwa kijana siyo mzuri sana lakini unapokua unazidi kuwa mzuri. Unapoanza kuwa na fujo katika umri mdogo nafasi ya hali kuwa mbaya ni kubwa zaidi," alisema.
Kulingana na Helene Perold, mkurugenzi mtendaji wa shirika la Volunteer and Service Enquiry South Africa na mmoja wa watafiti wachangiaji wa ripoti, wakati wa ujana mara nyingine wanajaribu kukuza utambulisho wao na wanapitia katika kipindi cha kuchanganya cha mabadiliko.
Wakati huu vijana ni rahisi kushawishiwa. Pia alielezea kuwa ni muhimu kushirikisha vijana na kuwaingiza katika jamii kuu.
"Tunaishi katika jamii ambapo inakubalika wazazi kupiga watoto wao na wanaume kupiga wake zao. Tunasema kuwa kuna haja ya kuwa na njia ya kuhusisha vijana, vijana wengi wanahisi kuwekwa pembeni na jamii kwasababu masuala yao hayaingizwi katika muktadha," alisema.
Masebula alisema kuwa ni muhimu kuingilia kati kupunguza ghasia miongoni mwa vijana.
"Kama tunapuuzia ghasia inazidi kuwa mbaya na mbaya zaidi. Tunajua kuwa watu wanajifunza tabia ya fujo. Watoto wanaanza kushinikizana na hatimaye wanaanza kupigana makofi. Mara tu mtu akijua kuwa kufanya fujo kunawafanya kuwa na nguvu wanaona hilo kama njia ya kutatua matatizo yao siku zijazo."
Kwa sasa Afrika Kusini ina baadhi ya mipango na sera ambayo wanajaribu kujenga vijana.
Ansa Verster ni meneja wa Diversion Programme kwa vijana watoto katika Kituo cha Restorative Justice. Kazi ya kituo hicho ni kutafuta ufumbuzi kati ya waathirika na waanzilishi wa uhalifu na pia kutoa mafunzo ya ujuzi kwa vijana ambao wamekiuka sheria. Ana imani kuwa vijana wanaofanya fujo wanaweza kubadilika, kama wanapata msaada sahihi na ulinzi wa kutosha.
Matokeo ya utafiti uliendana na hili na ulitaka sera ya umma katika kanda kuzingatia mahitaji ya vijana na kushughulikia mazingira ambayo yalizuia vijana kupata ajira, miongoni mwa mambo mengine.
Na inaonekana kana kwamba inaweza kuwa ufumbuzi. Banda anakubaliana kuwa kama angekuwa na ajira ya kudumu asingetoa huduma yake kutishia wapiga kura.
"Kama tungekuwa na vyanzo vingine vya kipato, tusingefanya hili. Lakini hakuna ajira, tunachokifanya hapa katika kituo ni sehemu ya kazi tu, na fedha haiwezi kutosha. Lakini wanasiasa hawa wanapokuja, wanatupatia fedha nzuri, na pia wanatununulia bia," anasema.
Anaongeza kuwa anasubiri kwa hamu uchaguzi ujao mwaka kesho kwasababu utakuwa fursa ya kutengeneza fedha.
(END/2010)
|
|
|