Inter Press Service News Agency
Tuesday, June 19, 2018   19:13 GMT    
   Homepage
   World Service
   East Africa
   Southern Africa
   West Africa
   Central Africa
 
   Environment
   Health-HIV/AIDS
   Education
   Rights
   Politics
   Economics
   and Finance
   Development
   Energy
   Population
   Culture
 
   Radio Service
 
   Français
 
   About IPS
 
   ENGLISH
   ESPAÑOL
   FRANÇAIS
   ARABIC
   DEUTSCH
   ITALIANO
   NEDERLANDS
   PORTUGUÊS
   SUOMI
   SVENSKA
   SWAHILI
   TÜRKÇE
PrintSend to a friend
Readers Opinions

ZIMBABWE
Wasichana Wajawazito Wenye VVU Wakimbia Tiba kwa Kuhofia Unyanyapaa
Ignatius Banda

BULAWAYO, Jul 22 (IPS) - Katika kliniki ya wazazi katika moja ya vitongoji vyenye wakazi wengi jijini Bulawayo, wakunga wa ajdi wako katika maumivu makali kuelezea kwa msichana wa miaka 15 mwenye mimba ni kwa nini lazima apime VVU kabla ya kujifungua.

Lakini kijana huyo, ambaye anapigapiga kifua chake taratibu katika jitihada ya kuzuia kile kilichoonekana kama kikohozi kinachouma, asingesikia suala hilo. Anahofia kuwa hofu yake mbaya itathibitika kwani tayari anadhani ana VVU.

Manesi wana wasiwasi kuhusu afya ya msichana huyo na kuamua kumwita bibi yake ambaye anapewa kazi ya kuelezea kwa kijana ni kwa nini ni lazima apime.

Kupima ni njia pekee ya kupatiwa dawa ambayo haitatibu tu kikohozi, lakini pia kumpatia maisha marefu na kuhakikisha mtoto wake ambaye bado hajazaliwa kuweza kukua, bibi anamhakikishia. Ni baada tu ya hapo upimaji wa VVU uliendelea.

Ni mazingira ambayo Nontando Siziba, mkunga mwenye umri wa miaka 53 ameshakutana nayo mara kwa mara. Pamoja na kwamba hatoi takwimu, Siziba anasema kwa kukata tamaa kuwa hili siyo tukio la kipekee kwani idadi kubwa ya wasichana wadogo wenye mimba wanatembelea kliniki ya wazazi.

Siziba anaelezea kuwa baadhi ya mama hao wadogo bado hawataki na wanaogopa – kupata huduma za uzazi wakati wa ujauzito chini ya mpango wa kuzuia maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto (PMTCT).

"Sasa tunapima VVU wanawake wote wenye mimba kama sehemu ya kujaribu kulinda afya ya mama na mtoto lakini mara nyingine hili ni zoezi gumu mno tunapofanya kazi na vijana," Siziba alielezea.

Utafiti wa kitaifa wa kliniki uliofanywa na wizara ya afya na ustawi wa watoto mwaka 2002 ulikuta kuwa mahudhurio ya kliniki ni asilimia 25.7, huku wizara ikigundua kuwa hii iliongeza kuenea kwa virusi vya VVU kwa watoto wachanga wakati huduma bora za kliniki zingezuia haya.

Pia kuna wasiwasi miongoni mwa wanaharakati wa VVU/UKIMWI kuhusu kupelekwa mapema unyagoni kwa wasichana wadogo – wengine wakiwa na umri wa miaka kumi na tatu – na kuingia katika masuala ya ngono. Hii inatokana na masuala ya kijinsia ambapo wanaume wenye umri mkubwa wanadhibiti uhusiano wa kimapenzi na wana uamuzi kufanya ngono salama au hapana.

Wataalam wanasema hali ya wasichana hawa wadogo inazidishwa na kutokutumia programu za PMTCT hasa miongoni mwa wasichana wadogo ambao wanafuata huduma za afya kliniki.

Siziba anasema hii pia imesababishwa na kuendelea kwa unyanyapaa wa VVU/UKIMWI miongoni mwa wasichana wadogo wanaofanya ngono, kuhisi wametengwa na maarifa ya umma kuwa siyo tu kwamba wanafanya ngono lakini pia wanaishi na VVU.

"Pamoja na kwamba wanafanya ngono, siyo wote wanachukua wajibu wa kuchukua tahadhari," Siziba alisema.

"Tumewahi kuwa na wakati ambapo wasichana hawa wadogo wanaambiwa wasinyonyoshe lakini wanafanya hivyo kwani wanajua wanajumuiya wakijua hawanyonyeshi watoto wao watajua wanaishi na virusi. Imekuwa ikichanganya mno."

Mpango ujulikanao kama Regional Psychosocial Support Initiative (REPSSI) hivi karibuni ulitoa ripoti ambapo watafiti walibainisha kwa mashaka makubwa kuwa wasichana wengi wadogo wenye watoto wanatambua wana VVU wanapokuwa wajawazito, na mara nyingine wanajua hali yao wakati watoto wao wanapougua.

REPSSI ni NGO ambayo inafanya kazi ya kutoa huduma ya kisaikolojia, wanasaidia na kuangalia ustawi wa watoto walioambukizwa VVU/UKIMWI katika Afrika Mashariki na Kusini.

"Tunahisi kuna mapengo kuhusu huduma ya kisaikolojia na kusaidia vijana wa umri mdogo," alisema Brighton Gwezera, Meneja wa Kuendeleza na Kubadilishana Maarifa wa REPSSI. "Wao (vijana wadogo) bado wanashindwa kushughulikia masuala yanayohusiana na unyanyapaa na hii imewafanya kushindwa kufaidika kikamilifu na huduma za kliniki."

Mwingiliano wa vijana wanaoishi na VVU umebainishwa kama moja ya njia ambazo zinataka kuondoa uhusiano kati ya mimba na VVU, katika umri ambapo vijana wanakuwa wanajazwa taarifa mbalimbali kila siku.

"Tunachofanya ni kufanya kazi na vijana wadogo wanaoishi na VVU kupitia vikundi vya misaada ili waweze kuwasiliana masuala yao kiurahisi na maamuzi yanayozunguka VVU na mimba na pia mustakabali wao wa baadae," Gwezera alisema.

Pia kuna wasiwasi kuhusu masuala ya kitamaduni ambayo yamenyima vijana wadogo kupata msaada rasmi na usiokuwa rasmi, ambao watafiti wanasema unazuia jitihada za kutoa msaada wa afya ya uzazi.

"Ukweli kwamba wana mimba kunawafanya kuonekana kuwa wanafanya mapenzi jambo ambalo linawafanya kubeba unyanyapaa. Hivyo linapoingia suala jingine la kuwa na VVU, ni vema vijana hawa kuliweka suala hilo kuwa siri," alisema Jerome Siyasiya mshauri nasaha mdogo katika shirika la Kanisa la Romani la Sibambene AIDS Trust. Anaongeza kuwa huu ni wakati ambapo mama wenye umri mdogo wanahitaji msaada zaidi.

Gwezera anakubaliana: "Kuna taarifa chache zinazowafikia vijana wadogo kuhusu VVU na mimba na hii ndiyo sababu tunaona wakipinga huduma bora za kliniki. Linalotakiwa kufanyika kuanzisha makundi yanayotoa msaada kwa vijana wadogo ambapo wanaweza kujadili kwa uhuru masuala yanayohusu hali zao."

Kwa maskini kuelewa VVU/UKIMWI na uhusiano wake na huduma ya kliniki, itakuwa wakati kabla ya vijana kukubaliana moja kwa moja na madawa ya kupunguza kasi ya VVU wakati nchi ikielekea kwenye kutekeleza mpango wa afya kwa wote.

"Vijana wadogo wanashindwa kujilinda ulinzi dhidi ya VVU, sasa wanashindwa kulinda watoto ambao hawajazaliwa. Sitaki kuamini tunapoteza katika vita hivi," alisema Siziba.

(END/2010)

 

 
 Latest News from Africa
News in RSS
XML error: The element 'html' is used but not declared in the DTD/Schema.
  Dernières Nouvelles
News in RSS
DEVELOPPEMENT: Nous devons penser autrement à la "sécurité"
AUSTRALIE: Le port de Newcastle bloqué par les Guerriers du changement climatique
IRAN: L’examen d’un document clé à l’AIEA suggère un coup d’Israël
PAKISTAN: Les Ahmadis confrontés à la mort ou à l’exil
ETATS-UNIS: Le budget de la défense peut accroître alors que le public est fatigué de la guerre
A lire également>>