Inter Press Service News Agency
Saturday, July 31, 2010   23:11 GMT    
   Homepage
   World Service
   East Africa
   Southern Africa
   West Africa
   Central Africa
 
   Environment
   Health-HIV/AIDS
   Education
   Rights
   Politics
   Economics
   and Finance
   Development
   Energy
   Population
   Culture
 
   Radio Service
 
   Français
 
   About IPS
 
   ENGLISH
   ESPAÑOL
   FRANÇAIS
   ARABIC
   ČESKY
   DEUTSCH
   ITALIANO
   JAPANESE
   NEDERLANDS
   POLSKI
   PORTUGUÊS
   SUOMI
   SVENSKA
   SWAHILI
PrintSend to a friend
Readers Opinions

AFYA-UGANDA
EU Yaunga Mkono Sheria Inayotishia Uhaba wa Madawa
Na Wambi Michael

KAMPALA, Machi 15 (IPS) - Umoja wa Ulaya (EU) unafadhili Uganda kuandaa rasimu ya sheria yenye utata ya Bidhaa Bandia, sheria ambayo imesababisha kilio kwani inatishia upatikanaji wa madawa ya kuresha maisha katika taifa hilo la kipato cha chini la Afrika Mashariki. Baadhi ya asilimia 90 ya madawa yanayotumiwa katika mfumo wa huduma za afya nchini Uganda yanaagizwa kutoka nje, ambapo asilimia zipatazo 93 ni dawa za kurefusha maisha.

IPS ilipata taarifa kuwa sehemu ya euro milioni tano ambazo wizara ya utalii, biashara na viwanda ya Uganda ilipata kutoka EU katika mkataba wa ufadhili wa Julai 2009 ilifadhili kuandikwa kwa rasmi ya sheria hiyo tata ambayo imekuwa ikikosolewa mno kuwa tishio la utoaji wa tiba.

Mkataba wa ufadhili una lengo la kusaidia Uganda kutekeleza mikataba ya ushirikiano wa kiuchumi (EPA) kati ya EU na Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Simon Lokodo, waziri wa nchi anayehusika na viwanda nchini Uganda, alikiri katika mahojiano na IPS kuwa mchakato wa kuandaa muswada huo umefadhiliwa na EU.

"Tunapata msaada kutoka Umoja wa Ulaya. Kutokana na msaada tunaopata kutoka kwao tumeweza kuajiri mtu ambaye atasaidia kwenda kiundani katika jambo hilo na kufanya kazi na washirika wengine kuandaa muswada ambao upo katika ngazi ya baraza la mawaziri sasa," alisema.

Lokodo aliiambia IPS kuwa hakuna jambo la kipekee juu ya sera za EU za kufadhili kupambana na bidhaa bandia kama sehemu ya msaada katika sekta ya biashara.

"Umeona jinsi masoko yetu yanavyojaa bidhaa bandia. Bidhaa hizo siyo tu kwamba zinaathiri maisha yetu lakini zinaua viwanda vyetu pia. Nadhani ni vema kufanya kazi na EU na washirika wengine kupambana na bidhaa hizi," alisema.

Lakini wanaharakati wameshangazwa na dhamira ya serikali ya Uganda kupitisha sheria ambayo inafasili bidhaa bandia kwa upana kwa kufanya kosa la jinai kuzalisha na kuingiza kutoka nje madawa ambayo hayapatikani kwa mamilioni ya watu nchini ambao wanaandamwa na VVU na UKIMWI na malaria.

Hatua hii imekuwa ikichanganya mno kwani Uganda, kama nchi yenye maendeleo duni, inapaswa kukaa hadi mwaka 2016 kabla ya kulazimika kutoa hati miliki ya kulinda bidhaa zake za madawa kama inavyotakiwa na Mpango wa Hati Miliki Zinazohusiana na Biashara (TRIPS) katika Shirika la Biashara Ulimwenguni.

Harvey Rouse, mkuu wa kitengo cha siasa na biashara cha ujumbe wa EU nchini Uganda, aliithibitishia IPS kuwa sehemu ya ufadhili wa euro milioni tano kufadhili mkataba huo iliingia nchini Uganda mwezi Julai 2009 na itafadhili utungwaji wa sheria ya kupambana na madawa bandia.

Alisema, "tunaunga mkono wizara ya bishara ... kufanyia mageuzi sera zake na sera za usimamiaji wa sheria, (ikiwa ni pamoja na) bidhaa bandia... Msaada huu upo chini ya EPA (mkataba wa ushirikiano wa kiuchumi) katika mpango unaohusiana na biashara na maendeleo ya sekta binafsi... (unaotekelezwa) katika miaka minne ijayo."

Akijibu maswali mengine kuhusu kama ujumbe wa EU ulikuwa unajua vikwazo katika huduma za afya ambazo muswada huo unaweza kusababisha, Alex Nakajjo, afisa oparesheni za biashara katika ujumbe wa EU mjini Kampala, alisema kuwa muswada huo "unalenga watu ambao wanakiuka sherai ya hati miliki … EU haiungi mkono biashara ya bidha bandia na bidhaa bandia zinapaswa kutokuchanganywa na … madawa ya kurefusha maisha".

Zaidi ya hapo, alisema, EU hapo awali "imeshinikiza kifungu cha upatikanaji kwa urahisi wa madawa ya kurefusha maisha katika nchi zinazoendelea chini ya Mkataba wa TRIPS. EU ikiwa kama moja ya mfadhili mkuu duniani katika kukuza upatikanaji wa madawa ya kurefusha maisha katika nchi zinazoendelea".

Hata hivyo, sheria za Uganda, kama ilivyo kwa sheria ya Kenya iliyopitishwa hivi karibuni na sheria inayosubiri kupitishwa ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika, haiweki utofauti kati ya madawa ya kurefusha maisha halali na bandia, kulingana na Program on Information Justice and Intellectual Property (PIJIP) katika Taasisi ya Sheria ya Washington, DC.

PIJIP inaongoza programu ya mafunzo juu ya matumizi ya mabadiliko ya hati miliki (IP) kuhakikisha kuwa madawa ya kurefusha maisha yanapatikana.

Wanaharakati pia wanasema kuwa, wakati madawa bandia na yasiyokidhi kiwango hayapaswi kuvumiliwa, sheria inayopendekezwa haitashughulikia tatizo la ubora duni kwani inachanganya na haki za IP kuhusu viwango vya ubora.

Mtaalam wa haki miliki Sisule Musungu alisema kuwa rasimu ya sheria inahusu maslahi ya biashara na wala siyo viwango vya usalama: kupeleka sheria hiyo kwa wizara ya biashara badala ya wizara ya afya ambayo imekuwa ikifanya kazi ya viwango vya usalama wa madawa kwa miaka mingi; na ushirikishwaji wa forodha na polisi badala ya mamlaka ya afya.

Dalili nyingine ni kwamba ufadhili wa sheria unatokana na fedha zilizotengwa kwa ajili ya biashara badala ya sera ya afya.

Musungu alielezea shinikizo lililopo nyuma ya sheria kama ifuatavyo: kama ubinafisishaji wa biashara katika bidhaa za kilimo na viwandani kutaendelea, hatimaye itakuwa na maana kuwa EU na Marekani hawataweza kushindana katika kilimo na Brazili na viwanda vya China na India.

Yote hayo yanabakia kwa EU na Marekani katika suala la kulinganisha faida katika haki miliki ya hudumu na maarifa.

"Haki miliki ya maarifa imekuwa sehemu muhimu mno ya sera za kigeni za EU... wahusika wakauu wa Mgharibi hawawezi kufika mbali kama wanatumia viwango vya IP vya chini kwasababu ya ufahamu ambao upo katika nchi nyingi zinazoendelea kuhusu madhara ya IP katika upatikanaji wa madawa na mambo mengine.

"Na kwa hiyo, matumizi ya lugha ya bidhaa bandia kimkakati yanahusu kupitia njia nyingine ya kufikia katika kupata sheria ya IP," alihitimisha.

IPS imechunguza mwenendo wa sheria hiyo na kukuta kuwa kujihusisha kwa EU katika sheria ya kupambana na bidhaa bandia kuna historia ndefu. EU ilifadhili mkutano wa kutathmini sekta ya biashara wa wizara ya biashara Oktoba 30, 2008 kupitia mpango wa "misaada ya kiufundi katika kukamilisha mikataba ya ushirikiano wa kiuchumi".

Katika mkutano huo rasimu ya kwanza ya Muswada wa Bidhaa Bandia ilijadiliwa baada ya kuwasilishwa na mwenyekiti wa Mfuko wa Sekta Binafsi Uganda (PSFU) na waziri wa zamani wa fedha wa Uganda Gerald Ssendaula.

PSFU, ambayo inawasilisha vyama vya wafanyabiashara 81 na mashirika ya umma, imekuwa moja ya mashirika ya msingi nchini Uganda yanayofanya kazi na mashirika mengine ya Afrika Mashariki kushinikiza sera za kitaifa na kikanda juu ya bidhaa bandia.

Wakati huo Ssendaula alibainisha bidhaa bandia kama changamoto kubwa katika mazingira ya biashara nchini Uganda.

Alisema kuwa, "sekta binafsi inatambua kwa wasiwasi mkubwa kuwa adhabu katika muswada wa kupambana na bidhaa bandia haitoshi kuzuia bidhaa bandia na makosa dhidi ya nembo ya biashara. Tunatoa wito kwa serikali kupitia upya vifungu vinavyohusika ili kuvifanya kutoa adhabu."

Ssenduala alipendekeza kifungo jela kwa miaka mitano na kuundwa kwa uhusiano wa kikanda na kimataifa na vyombo vingine kukabiliana na uingizaji wa bidhaa feki.

Rouse, mjumbe wa EU aliiambia IPS kuwa Uganda inakosa sheria za kujitosheleza na kushinikiza utekelezwaji wa haki za IP na ina hatua dhaifu za kutoa adhabu ambazo zinahamasisha biashara bandia. Uganda pia inahitaji taasisi maluum yenye kazi ya kupambana na bidhaa bandia. Msimamo huu umewekwa katika Muswada wa Bidhaa Bandia.

Nchi nyingi nyingine zinaweka suala la "kudanganya kwa makusudi" au kughushi "kwa ajili ya kujinufaisha kibiashara" kama ukiukwaji wa IP ya bandia. Shirika la Afya Ulimwenguni pia limeweka hatua ya chini ya kutumia bidhaa bandia kama vile "kwa makusudi na kwa udanganyifu kuweka kibandiko bandia" na "kuficha utambulisho au chanzo".

Lakini katika suala la Afrika Mashariki, kufanya kosa bila kujua ni kosa la jinai. Katika suala la Uganda muswada unaweka faini kubwa na hata kifungo cha jela cha hadi miaka 20. Hii ni kinyume na matumizi ya njia za kiraia za kutatua tatizo ambazo zinakubaliwa kimataifa katika suala la kukiuka IP, alisema Musungu.

Wataalam wa sheria wamesema kuwa Uganda ina sheria zinazofaa kushughulikia bidhaa bandia, mfano Sheria ya Haki Miliki, Sheria ya Nembo ya Biashara, Sheria ya Siri za Biashara na vifungu katika Utaratibu wa Makosa ya Jinai ambavyo vinasema ni kosa la jinai kuuza bidhaa bandia. (END/2010)

 

 








 Latest News from Africa
News in RSS
BURKINA FASO: Race to Achieve Goals on Sanitation
MALAWI: Innovative Campaigning by Women Candidates
SOUTHERN AFRICA: Realising Trade in Virtual Water
KENYA: Claim Disputed that Trade Measures "Aid" Counterfeiters
POLITICS-GUINEA: Women Amongst Also-Rans in Presidential Elections
ZIMBABWE: Badly Needed Work Begins on Bulawayo Water System
MADAGASCAR: Women Form Own Political Parties for Fair Representation
HEALTH: Uganda Authority Finding Less Counterfeit Drugs
TRADE-NAMIBIA: EU Backs Off on EPA
TRADE: Malawi Stands Firm on Conditions for Signing EPA
More >>
  Dernières Nouvelles
News in RSS
BURKINA FASO: Race to Achieve Goals on Sanitation
MALAWI: Innovative Campaigning by Women Candidates
SOUTHERN AFRICA: Realising Trade in Virtual Water
KENYA: Claim Disputed that Trade Measures "Aid" Counterfeiters
POLITICS-GUINEA: Women Amongst Also-Rans in Presidential Elections
A lire également>>