Inter Press Service News Agency
Saturday, July 31, 2010   23:18 GMT    
   Homepage
   World Service
   East Africa
   Southern Africa
   West Africa
   Central Africa
 
   Environment
   Health-HIV/AIDS
   Education
   Rights
   Politics
   Economics
   and Finance
   Development
   Energy
   Population
   Culture
 
   Radio Service
 
   Français
 
   About IPS
 
   ENGLISH
   ESPAÑOL
   FRANÇAIS
   ARABIC
   ČESKY
   DEUTSCH
   ITALIANO
   JAPANESE
   NEDERLANDS
   POLSKI
   PORTUGUÊS
   SUOMI
   SVENSKA
   SWAHILI
PrintSend to a friend
Readers Opinions

MAENDELEO-KENYA
Ongezeko la Kasi la Idadi ya Watu Latishia Maendeleo
Na Susan Anyangu-Amu

NAIROBI, Machi 15 (IPS) - Margaret Atieno, mama wa watoto sita mwenye umri wa miaka 38, alisema alitaka kuzuia mimba yake ya mwisho. Lakini kutokana na kukosekana kwa huduma za uzazi wa mpango kunakojitokeza mara kwa mara katika kituo chake cha afya katika eneo la kijijini la Siaya, magharibi mwa Kenya, hakukumpatia fursa ya kuchagua lakini kupata mimba tena, pamoja na ukweli kwamba hakutaka mtoto mwingine.

"Mume wangu, ambaye ana wake wengi, mimi na wake wengine wawili, hataki mpenzi wake yeyote yule kutumia uzazi wa mpango. Hivyo mfanyakazi wa afya ya jamii aliniambia kuwa nianze kutumia uzazi wa mpango wa kuingiza kwenye njia ya uzazi (IUCD), mume wangu asingegundua kitu. Lakini nilipotembelea kituo cha afya mara tatu, niliambiwa IUCDs zimeisha," alisema Atieno.

Alipotembelea mara ya nne, hatimaye alipata IUCDs, hakukuwa na glavu – na matokeo yake, wafanyakazi wa afya wasingeweza kutumbukiza kifaa hicho. Atieno alipata mimba kabla ya kutembelea tena kituo cha afya.

Atieno anasema hakutaka kuwa na watoto wengi kwasababu mume wake, ambaye ni mshona viatu, tayari alikuwa anapata shida kutunza watoto 13 ambao anao na wake zake watatu. Kuishi katika mila na katika jamii ya kijijini, kumefnaya kujiona hana haki ya kujua ni kiasi gani mume wake anaingiza, pamoja na kwamba ni vigumu mno kupata mahitaji ya lazima, Atieno na wake wengine hawaruhusiwi kufanya kazi kuchangia katika kipato cha kaya.

"Watoto wangu wawili wenye umri mkubwa zaidi, wa miaka 17 na 15, wangeshakuwa katika shule ya sekondari, Lakini ilibidi waache kutokana na kukosa fedha. Tunataka shida kila siku kusaka fedha na nguo kwa ajili ya kulisha watoto wangu, ukiachana na kuwapeleka shule," analalamika.

Wataalam wa jamii wametambua kuwa kukosekana kwa uzazi wa mpango ni moja ya sababu kuu zinazosababisha umaskini nchini kote Kenya. Ripoti ya Novemba 2009 ya Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID) inaonya kuwa Kenya haitaweza kuleta maendeleo ya kitaifa katika kiwango cha sasa cha ongezeko la watu.

Kama nchi inataka kufanikisha lengo la elimu ya msingi kwa wote, usalama wa chakula, huduma za afya ya msingi kwa wote na kupunguza vifo vya uzazi na watoto wachanga, wanandoa wanapaswa kuwa na familia ndogo, watafiti wa USAID walibainisha.

Serikali ya nchi hiyo pia imelichukulia kwa uzito suala la uhusiano kati ya umaskini na ongezeko la watu. Dk Boniface K’Oyugi, afisa mtendaji mkuu wa Shirika la Uratibu wa Taifa wa Idadi ya Watu na Maendeleo (NCAPD), alionya kuwa kasi ya ongezeko la idadi ya watu nchini Kenya ya asilimia tatu kwa mwaka, ilihitaji kupunguzwa angalau kwa theluthi moja.

"Katika nchi zilizoendelea watu wana mtoto mmoja au wawili tu, lakini hapa, mwanamke mmoja ana watoto watano na zaidi. Kama tunataka kuwa kama nchi zilizoendelea, tunatakiwa kwa haraka kupunguza idadi yetu ya ongezeko la watu," K’Oyugi alisema katika mkutano kwenye Hoteli ya Hilton mjini Nairobi mwezi Februari.

Alitoa wito wa kuboreshwa kwa utoaji wa huduma za afya ikiwa ni pamoja na huduma za uzazi wa mpango, kusaidia wanandoa kusimmia vizuri afya yao ya uzazi na mimba.

"Uamuzi wa idadi ya watoto ni wa mtu binafsi. Lakini familia ndogo zitasababisha faida kwa mtu binafsi, kaya na hata ngazi ya kitaifa," alielezea.

K’Oyugi ana imani serikali ya Kenya inaweza kujifunza kutoka nchi za Asia, kama vile Thailand, Malaysia, Korea Kusini, Taiwan na Singapore, ambazo ziliweza kuimarisha uchumi wao kwa kupunguza kiwango cha ongezeko la watu.

Hata hivyo, ni vema kutambua kuwa ongezeko la idadi ya watu ni moja tu ya sababu nyingi zinazodumaza maendeleo nchini Kenya. Kupitia mkakati wa kupunguza umaskini 2003-2007, serikali iliweka wazi kuwa utawala bora, elimu ya msingi, usawa wa jinsia na kuzuia maambukizi ya VVU, ikiwa ni pamoja na viwango vya juu vya rushwa ni miongoni mwa vikwazo vinavodumaza ukuaji wa kiuchumi.

Bado idadi ya watu nchini inatoa uamuzi wa ni kiasi gani cha bajeti kinahitajika kwa ajili ya huduma kwa kila mtu.

Kulingana na Taasisi Kuu ya Takwimu ya Kenya, Kenya ilikuwa na watu milioni 38 mwaka 2008 – ongezeko la theluthi nzima tangu mwaka 1999. Makadirio ya USAID ni kwamba kama kiwango cha ongezeko la idadi ya watu kitabakia palepale, idadi ya Wakenya itaongezeka hadi milioni 82 ifikapo mwaka 2040.

"Watu wengi ina maana shinikiza zaidi katika mazingira, kwani mahitaji ya chakula, ardhi, maji safi na rasilimali za nishati vinakuwa haba. Kwa kupungua kwa rasilimali, kuna hatari halisi ya kuibuka kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe kwani watu watapigania rasilimali haba," K’Oyugi alionya.

Ongezeko la idadi ya watu pia litaongeza uhamaji wa watu kutoka vijijini kwenda mijini, kulingana na USAID. Hii itaongeza shinikizo katika miundombinu ya mijini, na hatimaye kusababisha kuibuka kwa makazi duni na umaskini. Tayari nchini Kenya makazi duni yana sifa ya kuwa na watu wengi kupita kiasi, makazi yasiyotosheleza, kukosekana kwa maji safi ya kunywa ya kutosha na usafi wa mazingira, kukosekana kwa usalama, unyonyaji na unyanyasaji.

NCAPD kwa sasa inashinikiza uzazi wa mpango kuchukua jukumu la kati katika ajenda ya sera za serikali kupunguza umaskini na kubadili nchi kuwa ya kipato cha kati yenye maisha bora na ulinzi wa mazingira, kama ambavyo Dira ya nchi 2030 inataka.

"Lengo ni kufufua kampeni ya uzazi wa mpango katika kiwango cha miaka ya 1980, ambapo katika kipindi hicho kiwango cha uzazi kilishuka kutoka watoto 6.7 kwa mwanamke mwaka 1989 hadi 5.4 mwaka 1993 na 4.7 mwaka 1998," alisema NCAPD afisa wa vyombo vya habari David Kinyua.

Aliahidi kuwa, katika mwaka mpya wa fedha unaoanza Juni, ongezeko la bajeti litatengwa kwa ajili ya uzazi wa mpango, lakini hakuweza kuelezea ni kiasi gani cha fedha kitatumika na wapi.

(END/2010)

 

 








 Latest News from Africa
News in RSS
BURKINA FASO: Race to Achieve Goals on Sanitation
MALAWI: Innovative Campaigning by Women Candidates
SOUTHERN AFRICA: Realising Trade in Virtual Water
KENYA: Claim Disputed that Trade Measures "Aid" Counterfeiters
POLITICS-GUINEA: Women Amongst Also-Rans in Presidential Elections
ZIMBABWE: Badly Needed Work Begins on Bulawayo Water System
MADAGASCAR: Women Form Own Political Parties for Fair Representation
HEALTH: Uganda Authority Finding Less Counterfeit Drugs
TRADE-NAMIBIA: EU Backs Off on EPA
TRADE: Malawi Stands Firm on Conditions for Signing EPA
More >>
  Dernières Nouvelles
News in RSS
BURKINA FASO: Race to Achieve Goals on Sanitation
MALAWI: Innovative Campaigning by Women Candidates
SOUTHERN AFRICA: Realising Trade in Virtual Water
KENYA: Claim Disputed that Trade Measures "Aid" Counterfeiters
POLITICS-GUINEA: Women Amongst Also-Rans in Presidential Elections
A lire également>>