SOMALIA Marekani Inapaswa Kukubali Mamlaka ya Kiislam, Inasema Ripoti Na Charles Fromm na Mohammed A. Salih
WASHINGTON, Machi 11 (IPS) - Marekani inapaswa kukubali "Mamlaka ya Kiislam" nchini Somalia kama sehemu ya mkakati wa "kutokujihusisha shiriki" katika nchi yenye vita, kulingana na ripoti mpya iliyotolewa hapa na Baraza la Mahusiano ya Kigeni (CFR) siku ya Jumatano.
Ripoti yenye kurasa 39 inataka Marekani kutambua kuwa "Mamlaka ya Kiislam" hata kama inaihusisha al-Shabaab, au "vijana" wa Kiarabu, na kundi la waasi wa Kiislam ambalo limetangaza kuunga mkono al Qaeda.
Imesema mfumo wa sasa wa Marekani nchini Somalia wa kutaka kuwepo kwa Serikali ya Mpito ya Shirikisho (TFG) "haufanyi kazi". Siyo tu kwamba unaondoa sehemu kubwa ya Wasomali, lakini pia unagawa jumuiya ya Kiislam ambayo tayari imeshagawanyika na kuwa kile kinachojulikana kama kambi za "watu wa msimamo wa wastani" na "wenye msimamo mkali", inasema ripoti.
Wakati ripoti inahamasisha "dalili ya ushirikishwaji" na Marekani juu ya watu wenye msimamo mkali wa ndani, inapendekeza Marekani kuonyesha "kutokuvumilia' wahusika wa ndani wanaojaribu kutumia mgogoro wa Somalia kwa maslahi yao binafsi", wakati huo ikimaanisha al Qaeda.
"Shabaab kama umoja wa kujenga fursa utawala wake wa nchi ni dhaifu kuliko inavyoonekana kwa nje. Watu wenye msimamo mkali nchini Somalia – ambao dhamira zao kwa kiasi kikubwa ni za ndani – wana uwezekano wa kushirikiana na al-Qaeda na vyombo vingine vya kigeni wakati chombo cha kushirikiana kikizidi kufifia," inasema ripoti hiyo, iliyoandikwa na Bronwyn Bruton, mshirika wa masuala ya kimataifa wa CFR. "Marekani na washirika wake lazima wahamasishe masuala haya kupanuliwa."
Hata hivyo, David Shinn, balozi wa Marekani katika nchi jirani ya Ethiopia miaka ya 1990, anakubaliana kuwa uongozi wa al-Shabaab utakuwa tayari kuungana na mpangilio wowote ule wa siku za baadaye.
"Nadhani al-Shabaab imekuwa na msimamo mkali zaidi na sioni kiongozi yeyote yule anayefuata vitendo katika al-Shabaab. Wengi katika uongozi wanaweza kuwa watu wa vitendo, wabebaji wa bunduki, lakini siyo viongozi," alisema Shinn, ambaye pia ametumika kama balozi wa Marekani nchini Burkina Faso mwishoni mwa miaka ya 1980.
"Sioni upenyo katika uongozi na sioni uongozi wa vitendo. Sehemu kubwa ya ripoti imeandaliwa kwa dhana kuwa inawezekana kujadiliana na al-Shabaab na nadhani hayo ni mawazo ya kutaka itokee hivyo," alisema.
Ripoti pia inaonya dhidi ya kuendelea kupata msaada kwa TFG inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa kutokana na kwamba imeshathibitishwa "kutokufanya kazi ya gharama kubwa".
"TFG haina uwezo wa kuboresha usalama, kutoa huduma za msingi, au kukubaliana na koo za Somalia na vikundi vya upinzani kuwa watakuwa na msingi wenye nguvu wa utawala," inasema ripoti hiyo.
TFG iliundwa mwaka 2004 kupitia upatanisho wa Umoja wa Mataifa nchini Kenya katika jitihada za kukomesha mapigamno yanayoendelea nchini Somalia. Serikali ya TFG ilihamia nchini Somalia mwaka 2005 lakini haijaweza "kupata mafanikio yoyote yale ya kujenga taifa" kutokana na kuwepo kwa mgawanyiko wa ndani, shirika la kutatua migogoro lenye makao yake mjini Brussels la International Crisis Group (ICG) lilisema.
Kulikuwa na matarajio kuwa kuwekwa kwa Sharif Ahmed, mkuu wa zamani wa Muungano wa Mahakama za Kiislam, kama rais Januari 2009 kungevutia idadi ya kutosha ya viongozi wa Kiislam kujitenga au kuvigawa vikosi vya al-Shabaab. Lakini Shinn anasema TFG imekuwa "na nguvu kidogo" katika miezi ya karibuni.
"Yeye [Bruton] anaonekana kuanza na dhana kuwa TFG ina uwezekano wa kushindwa. Sijashawishika kuwa itashindwa," alisema Shinn, ambaye alikuwa mjumbe wa Kamati ya ushauri ya ripoti hiyo. "Ukweli kuwa TFG chini ya Rais Ahmed imekuwepo kwa zaidi ya mwaka kumeshangaza wengi wanaojulikana kama wataalam wa Somalia. Siyo sahihi kudhani kuwa itakuja kushindwa."
Ikiwa na jina la "Somalia , A New Approach", ripoti inakuja wakati mgumu katika mabadiliko ya sera za Marekani juu ya Somalia . Mapema wiki hii, gazeti la New York Times liliripoti kuwa Vikosi vya Oparesheni Maalum vya Marekani (SOF) vinasaidia serikali ya Somalia, ambayo ina askari wapatao 7,000 katika mji mkuu, mpango unaosubiri wa kijeshi wa TFG unaolenga katika kuwafagia wapiganaji wa al-Shabaab kutoka Mogadishu.
Ripoti inaandika kwa undani miongo miwili ya vita kali katika taifa hilo la Pembe ya Afrika, kuanzishwa kwa TFG, na kugombea madaraka kunakoendelea baina ya waasi wa al-Shabaab na washirika wao.
Bruton anasisitiza kuwa sera za Marekani za kutoa msaada wa kidiplomasia na kijeshi isiyokuwa ya moja kwa moja kwa TFG ni dhaifu na imekuwa na lengo la "kutenga serikali, na...kushinikiza ushirikiano miongoni mwa vikundi vyenye msimamo mkali vilivyogawanyika na vinavyopigana."
Ripoti inataka Marekani kufanya jaribio la mwisho kusaidia serikali ya Somalia kujenga kuungwa mkono na umma kwa kuingiza viongozi wa vikundi vingine vya Kiislam. Lakini inataka utawala wa Rais Barack Obama kufikiria mabadiliko makubwa ya kisera kama TFG ikishindwa au ikiendelea kutengwa kufikia kiasi cha kukosa nguvu kabisa.
TGF, ambayo inasaidiwa na baadhi ya askari 5,000 wa Umoja wa Afrika (AU) katika ujumbe wa kutafuta amani uliopewa mamlaka na Umoja wa Mataifa, inadhibiti tu majengo kadhaa katika mji mkuu wa Somalia wa Mogadishu na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Aden Adde, wakati al-Shabaab inadhibiti maeneo makubwa ya ardhi ya nchi hiyo hadi kusini, na maeneo ya mji mkuu huo.
Kihistoria, malashi ya Washington katika taifa tete la Afrika Mashariki yamejikita tu katika masuala ya kiusalama, na hivi karibuni ilikuwa inainyima kuwa maficho ya al Qaeda au vikundi vinavyounga mkono magaidi katika nchi ya Somalia. Katika miaka ya karibuni, Marekani imefanya mashambulizi kadhaa kulenga shabaha za Somalia zilizoaminika kuhusiana na al Qaeda.
Hata hivyo, baadhi ya wachambuzi wana imani kuwa msaada wa Marekani unaweza kuimarisha kiurahisi harakati za waasi katika mazingira ambayo tayari ni magumu.
"Utawala umeamua kuchukua hatua kali ya kusaidia TFG na inatoa mafunzo, ujasusi, ushauri wa kijeshi, na vifaa kwa jeshi la TFG katika mshambulizi makali ya TFG yanayotarajiwa dhidi ya al-Shabaab," alisema David R. Smock, makamu wa rais wa Kituo cha Amani cha Marekani cha Upatanishi na Ufumbuzi wa Migogoro.
"Hii ni kamali kubwa ya Marekani ambayo inaweza kushindwa. Mashambulizi yanaweza kushindwa kiurahisi, jambo linaloweza kusababisha Marekani kushiriki zaidi. Tumechomwa vibaya nchini Somalia hapo kabla, na tunaweza kuchomwa tena," aliongeza.
Mwishoni mwa mwaka 1992, utawala wa Rais wa zamani George H. W. Bush ulipeleka askari Somalia kama sehemu ya oparesheni iliyoidhinishwa na Umoja wa Mataifa kulinda usambazaji wa misaada ya kibinadamu na chakula kwa wanajumuiya waliokuwa na njaa. Lakini, katika oparesheni ya "kujenga taifa" iliyoshindwa, jeshi la Marekani lilijitumbukiza zaidi katika vita kati yao na miongoni mwa koo ambazo zilisababisha kupinduliwa kwa serikali ya Siad Barre mwaka 1991.
Rais wa wakati huo Bill Clinton alianza kuondoa askari wa Marekani baada ya askari 18 wa SOF kuuawa wakati wa shambulizi kali la helikopta dhidi ya kiongozi mmoja wa ukoo mjini Mogadishu Oktoba 1993 na kujiondoa kabisa mapema mwaka 1994.
Ripoti ya CFR pia inapendekeza mkakati wa maendeleo uliotenganishwa kwa kushirikiana na "mamlaka yasiyokuwa rasmi na ya jadi" yaliyopo nchini. Inatoa wito wa kuzuia Ethiopia, ambayo imekuwa ikijihusisha na mgogoro wa Somalia kwa miaka kadhaa.
Bruton anapendekeza kuwa Marekani inapaswa "kutokumiliki mgogoro wa Somalia" na inapaswa kuanzisha kampeni ya kidiplomasia kushirikisha nchi za Ulaya na Mashariki ya Kati kusaidia kuleta utulivu wa Somalia na kutafutia ufumbuzi mahitaji yake ya kibinadamu na kimaendeleo.
Ripoti ya Umoja wa Mataifa ya Jumatano ilidai kuwa hadi nusu ya chakula cha msaada kilichotolewa na Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) kwenda Somalia kinaelekezwa kwa wakandarasi wanaokula rushwa, wafanyakazi wa ndani wa Umoja wa Mataifa na wanamgambo wa Kiislam nchini humo. WFP imekanusha madai hayo, na kuyaita "yasiyothibitishwa".
(END/2010)
|
|
|