Inter Press Service News Agency
Saturday, July 31, 2010   23:29 GMT    
   Homepage
   World Service
   East Africa
   Southern Africa
   West Africa
   Central Africa
 
   Environment
   Health-HIV/AIDS
   Education
   Rights
   Politics
   Economics
   and Finance
   Development
   Energy
   Population
   Culture
 
   Radio Service
 
   Français
 
   About IPS
 
   ENGLISH
   ESPAÑOL
   FRANÇAIS
   ARABIC
   ČESKY
   DEUTSCH
   ITALIANO
   JAPANESE
   NEDERLANDS
   POLSKI
   PORTUGUÊS
   SUOMI
   SVENSKA
   SWAHILI
PrintSend to a friend
Readers Opinions

KENYA
Mapendekezo ya Mabadiliko ya Katiba Yaweka Nyuma Haki za Wanawake
Susan Anyangu-Amu

NAIROBI, Machi 11 (IPS) - Lillian Mutuku, mama wa watoto watatu mwenye umri wa miaka 34, anaelezea nyumba yake katika eneo la Katine, katika Mkoa wa Mashariki mwa Kenya wa Tala, kama eneo baya kuishi. Ardhi ni duni, anasema, jua linaunguza bila huruma na uoto wa asili umetawanyika.

"Watu hapa wanakabiliwa na shida ya kupata mahitaji yao ya kila siku na kutafuta maji na chakula kwa ajili ya familia zao. Wakati wa msimu wa ukame hali ni mbaya zaidi, kwani mazao machache tunayopanda yanakufa, na kufanya chakula kuwa na gharama kubwa," alielezea. "Wanawake inabidi watembee maili nyingi kwa siku katika kutafuta kimiminika cha thamani – maji."

Ukweli kwamba vyama vya siasa nchini Kenya vimekuwa katika harakati za kuandika upya katiba ya nchi hiyo tangu Februari 2008 katika hali ya kukomesha ghasia za baada ya uchaguzi na kuboresha haki kuna maana kubwa kwa Mutuku, pamoja na ukweli kwamba anashindwa kuelewa maana ya maneno katika waraka huo. Ana imani kuwa Katiba mpya italazimisha serikali kuhakikisha familia yake inapata chakula, malazi na maji na huduma za afya.

"Masuala ambayo yamejaza akili yangu ni jitihada za kila siku kusaka chakula kwa ajili ya familia na watoto wangu kwenda shule. Wakati kuna mpango wa shule ya msingi bure, hakuna walimu wa kutosha katika eneo letu, na hivyo wazazi wanalazimika kulipia Shiligi za Kikenya 100 (dola 1.3) kwa mwezi kuwalipa walimu binafsi," Mutuku anasema.

Hizi ni fedha nyingi mno kwa Mutuku, mfanyakazi wa nyumbani, na mume wake, ambaye anafanya kazi kama kibarua. Wawili hao wanaingiza wastani wa dola 100 kwa mwezi, ambazo ni vigumu mno kuwawezesha kulisha familia yao.

Kama Kamati Teule ya Bunge (PSC), ambayo ilianzishwa kusimamia mchakato wa marekebisho ya Katiba, itafanikiwa, familia ya Mutuku haitaweza kuwajibisha serikali ili kupata haki zao za msingi.

PSC imekuwa ikikosolewa na mashirika mengi ya haki za wanawake kutaka kurahisishwa kwa lugha ya waraka huo, ambao uliandaliwa na Kamati ya Wataalam (COE). Waraka wa awali wa COE ulithibitisha kutoa haki za kijamii na kiuchumi kupitia Katiba, lakini PSC ilibadili lugha ya Vifungu vya Haki za Binadamu, na kuachia bunge madaraka ya kuhakikisha haki hizo.

PSC iliondoa mistari kadhaa inayozungumzia haki za msingi za binadamu, ikiwa ni pamoja na haki za hifadhi ya jamii na afya, ikiwa ni pamoja na huduma za afya, huduma za afya ya uzazi na tiba za dharula. Iliondoa haki ya elimu kwa Wakenya, ikiwa ni pamoja na haki ya elimu ya awali na ya msingi ya bure na lazima ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa elimu ya sekondari na baada ya sekondari. Haki ya nyumba, chakula na maji pia ziliondolewa katika waraka wa katiba.

Mwanasheria Catherine Mumma anasema hii ni hasara kubwa kwa wanawake wa Kenya ambao mara nyingi hubeba mzigo mkubwa wa kutunza familia zao: "Sura ya Haki za Binadamu kama ilivyoandikwa na COE ni moja ya mafanikio makubwa ya wanawake katika nchi hii. Mwanamke ambaye anatembea masaa mengi kwenda hospitalini na kuanguka na mtoto wake mgongoni kutokana na kukosa chakula hajali maneno magumu ya kisheria katika katiba. Anataka kusikia kuhusu dhamira ya serikali kuhakikisha anapata haki za msingi."

Akizungumza katika warsha ya siku moja iliyoandaliwa na mashirika kadhaa ya wanawake mjini Nairobi Februari kupitia rasimu za COE na PSC – Grace Maingi-Kimani, kaimu mkurugenzi wa shirika lisilokuwa la kiserikali la "Federation of Women Lawyers Kenya" alisema PSC iliruka jukumu lake kutokana na kurekebisha Haki za Binadamu.

"PSC ilifanya jambo lisilofikiriwa na kupendekeza kufutwa kwa jukumu la serikali la kuingiza haki za binadamu za kimataifa. Pia walifuta kifungu cha haki za kijamii na kiuchumi na kuachia bunge kuwa na nguvu ya kuamua kupitia sheria ni lini na jinsi gani haki na viwango vinaweza kutumiwa katika muktadha wa kitaifa," Kimani alielezea.

Pricilla Nyokabi, mkurugenzi mtendaji wa shirika la haki za wanawake la Kituo cha Sheria, alikubaliana kuwa bunge linapaswa kuachwa kupewa jukumu lolote isipokuwa kurejesha haki hizo katika rasimu.

"Kuingiza haki hizi za katiba kutalazimisha serikali kuhakikisha kuwa wananchi wote watapewa fursa sawa. Kama Katiba ingesema kila mtu ana haki ya kupata huduma hizi, mtu anaweza kutekeleza haki pale ambapo hazipo," alibainisha Nyokabi.

Mwenyekiti wa PSC Mohammed Abdikadir, hata hivyo, anasema katiba inapaswa kuwa waraka unaohusu kanuni pana na imani ambazo zinaongoza serikali. Undani wa nyongeza unapaswa kuelezewa katika sheria.

Wanaharakati wa haki za binadamu wana wasiwasi. "Tunaweza kuacha (haki zetu za binadamu) kwa wabunge ambao siku zote wanapiga kelele? Hapana, hatuwezi kuwaamini kutuamulia haki zetu za msingi," alisema mwanaharakati wa haki za binadamu Miriam Wanjiku.

Kwa sasa, rasimu ya karibuni zaidi ya Katiba inarekebishwa na Bunge, ambayo ina siku 30 kujadili waraka na kuamua kama utapitishwa. Wabunge wanahitaji kupata mbili ya tatu ya kura kubadili maneno ya rasimu.

Kuzuia waraka kutokupitishwa, mashirika ya haki za binadamu, ikiwa ni pamoja na FIDA Kenya, Urgent Action Fund, Centre for Rights Education and Awareness, Africa Woman and Child Feature Services, wamewasilisha waraka kwa bunge, wakidai kuwa waraka wa kwanza wa rasimu ya COE utumike.

"Wanawake wa Kenya wanadai kutambuliwa katika mikataba ya haki za binadamu ya kikanda na kimataifa ambayo Kenya imeridhia," waraka huo umesema.

(END/2010)

 

 








 Latest News from Africa
News in RSS
BURKINA FASO: Race to Achieve Goals on Sanitation
MALAWI: Innovative Campaigning by Women Candidates
SOUTHERN AFRICA: Realising Trade in Virtual Water
KENYA: Claim Disputed that Trade Measures "Aid" Counterfeiters
POLITICS-GUINEA: Women Amongst Also-Rans in Presidential Elections
ZIMBABWE: Badly Needed Work Begins on Bulawayo Water System
MADAGASCAR: Women Form Own Political Parties for Fair Representation
HEALTH: Uganda Authority Finding Less Counterfeit Drugs
TRADE-NAMIBIA: EU Backs Off on EPA
TRADE: Malawi Stands Firm on Conditions for Signing EPA
More >>
  Dernières Nouvelles
News in RSS
BURKINA FASO: Race to Achieve Goals on Sanitation
MALAWI: Innovative Campaigning by Women Candidates
SOUTHERN AFRICA: Realising Trade in Virtual Water
KENYA: Claim Disputed that Trade Measures "Aid" Counterfeiters
POLITICS-GUINEA: Women Amongst Also-Rans in Presidential Elections
A lire également>>