Inter Press Service News Agency
Saturday, July 31, 2010   23:12 GMT    
   Homepage
   World Service
   East Africa
   Southern Africa
   West Africa
   Central Africa
 
   Environment
   Health-HIV/AIDS
   Education
   Rights
   Politics
   Economics
   and Finance
   Development
   Energy
   Population
   Culture
 
   Radio Service
 
   Français
 
   About IPS
 
   ENGLISH
   ESPAÑOL
   FRANÇAIS
   ARABIC
   ČESKY
   DEUTSCH
   ITALIANO
   JAPANESE
   NEDERLANDS
   POLSKI
   PORTUGUÊS
   SUOMI
   SVENSKA
   SWAHILI
PrintSend to a friend
Readers Opinions

NAMIBIA
Mwanamuziki wa Kike wa Hip-Hop Apinga Ubaguzi
Na Servaas van den Bosch

WINDHOEK, Machi 9 (IPS) - Muziki wa miondoko ya hip-hop barani Afrika ulianza kujikita katika kuwaonyesha wanawake kwa mtizamo chanya, lakini mitizamo ya kitamaduni ya jadi dhidi ya wanawake bado imejikita katika sekta hiyo, anasema mwanamuziki mwanamke wa Namibia.

Kilichoanza katika mwishoni mwa miaka ya sabini kama kuonyesha kunyimwa haki kwa vijana wa Marekani wenye asili ya Kiafrika katika jiji la New York, kilichukua nafasi katika miji ya Kiafrika kwa kasi. Katika vitongoji vya miji ya Afrika Kusini na Namibia, muziki wa hip-hop ulijijenga katika aina inayojulikana kama kwaito na afropop na kuonyesha zama baada ya ubaguzi wa rangi.

Pamoja na kwamba harakati za uhuru na kukimbia nchi ambako kuliacha mitandao ya kijamii ikiwa imetawanyika kulijenga nafasi kwa wanawake wa Namibia kujinasua na jadi na kuanza kujiunga na fani ya muziki, uhuru huu umejawa na utata.

"Hakuna maeneo mengi katika Afrika kama vile Namibia ambapo tunaweza kuruka katika jukwaa huku tukiwa tumevalia mavazi yetu mafupi bila kusababisha kelele," anasema Frieda Haindaka kutoka kundi la wasichana wawili la Gal Level. "Wakati huo huo changamoto yetu kuu ni kuwa wanawake katika sekta iliyojaa wanaume. Kila mara tunatakiwa kudhihirisha kuwa tunaweza. Watu wanataka tu kuona wasichana wawili wanaovutia kimapenzi wakiwa jukwaani na hawafikirii tunaweza kufanya kitu."

Wanasanaa wengine wanawake wanahisi ugumu kutoka katika jadi za Namibia.

"Ni kweli tunahisi ni dhaidu mbele ya wanaume," anakubali mwimbaji, Sally.

"Nilikuwa naogopa wanaume. Ningekwenda kwenye onesho na kukutana na mvulana mmoja hadi mwingine anayeshangiliwa na watazamaji na naanza kuwaza nitafanya nini? Nafikiri kuondoka na kutokomea mbali.’

"Na wanaume hawana msaada," anaongeza. "Nakwenda kwenye studio na nakutana na wanaume saba huku wakiwa wamekaa na mtizamo wao wa kwaito huku hip-hop yao ikiendelea, na wanakuangalia tu kama vile wanasema: ‘Wacha…. Utafanya nini mama?’ Inanifanya nikimbilie kujibanza kwenye kona mara moja."

Pamoja na ubaguzi, baadhi ya wanasanii wa muziki wa hip- hop wa kike wanafanya kile wanachoweza kufanya kutengeneza muziki ambao unapeleka ujumbe kwa wasikilizaji vijana wa kike ambao unawavutia na pia ambao ni chanya.

"Katika mashairi yangu nahamasisha wanawake kufanya kazi wakiwa na pipi zao mdomoni, na wasitegemee kupendelewa," anasema mshindi mara mbili wa Tuzo ya Muziki ya Channel O ‘Lady May’ (23), ambaye alitoa albamu yake ya tatu mwaka jana.

Moja ya singo yake moja iliitwa Chokola (viatu vya visigino virefu) "Unapovalia viatu vya visigino virefu unahisi kuwa na nguvu, unahisi mwenye mvuto wa kimapenzi, unahisi kana kwamba unaweza kuteka ulimwengu mzima. Viatu vya visigino virefu vinafanya mwanamke kujiamini, lakini pia vinahitaji kuwa na malengo na nidhamu, au utaweza kuanguka," anaeleza.

Muziki wa Sally, ‘dollhouse’, unahusu mwanamke ambaye anavunja uhusiano wa kunyanyaswa. "Kutokana tu na kwamba wewe ni mwanaume hutaki kuniambia niwe nani," anaimba.

Lakini mahitaji ya sekta na ushindani wa mauzo katika biashara ambapo viwango vya wanaume ambavyo tayari vimeshawekwa vinasababisha kuwepo kwa nafasi ndogo mno ya uanaharakati.

"Ningependa kuimba nyimbo ambazo zina ujumbe, lakini, unapaswa pia kuwafanya watu wacheze," Sally anaiambia IPS.

"Tuna wasanii wanawake wachache tu ambao wameweza kuingia kwenye fani nchini Namibia na hakuna hata mmoja kati yao amefanikiwa kama walivyokuwa wanaume," anasema DJ Chè Ulenga wa redio ya jamii ya Base FM iliyopo katika kitongoji cha Katutura. Ulenga ameona wanawake wengi wanaoweza kupata mafanikio wakitelekeza ndoto zao za kuwa wasanii wanaouza zaidi.

Ulenga aliiambia IPS malipo ni madogo katika sekta, huku mameneja kila mara wakipokea asilimia 50 ya ada, kama wanawake wanalipwa.

"Wanawake wanafanya kazi katika nyimbo au video ambazo zinapata umaarufu lakini hawajawahi kupata kutambuliwa. Wanaume hawawachukulii kwa uzito na wanakataa kuwekeza katika wasichana hata kama wanaimba nyimbo nzuri."

"Wasichana mara zote wanadanganywa," anasema Sally. "[Waandaaji] wanakuambia utakuwa na albamu yako, utakuja kuwa nayo, utakuwa nyota. Lakini mara tu mwandaaji anapoanza kukutaka na kukupata muziki unaishia hapo."

Unyanyasaji na unyonyaji ambao Sally anauelezea umeenea katika sekta ya muziki ambapo wanawake vijana, wakiwa na njaa ya kupumzika na waandaaji maarufu, hawaulizi maswali mengi.

"Hasa kama ukiwa si kitu na unafurahia kuwa nyuma ya kipaza sauti," anasema Sally.

(END/2010)

 

 








 Latest News from Africa
News in RSS
BURKINA FASO: Race to Achieve Goals on Sanitation
MALAWI: Innovative Campaigning by Women Candidates
SOUTHERN AFRICA: Realising Trade in Virtual Water
KENYA: Claim Disputed that Trade Measures "Aid" Counterfeiters
POLITICS-GUINEA: Women Amongst Also-Rans in Presidential Elections
ZIMBABWE: Badly Needed Work Begins on Bulawayo Water System
MADAGASCAR: Women Form Own Political Parties for Fair Representation
HEALTH: Uganda Authority Finding Less Counterfeit Drugs
TRADE-NAMIBIA: EU Backs Off on EPA
TRADE: Malawi Stands Firm on Conditions for Signing EPA
More >>
  Dernières Nouvelles
News in RSS
BURKINA FASO: Race to Achieve Goals on Sanitation
MALAWI: Innovative Campaigning by Women Candidates
SOUTHERN AFRICA: Realising Trade in Virtual Water
KENYA: Claim Disputed that Trade Measures "Aid" Counterfeiters
POLITICS-GUINEA: Women Amongst Also-Rans in Presidential Elections
A lire également>>