Inter Press Service News Agency
Saturday, July 31, 2010   23:19 GMT    
   Homepage
   World Service
   East Africa
   Southern Africa
   West Africa
   Central Africa
 
   Environment
   Health-HIV/AIDS
   Education
   Rights
   Politics
   Economics
   and Finance
   Development
   Energy
   Population
   Culture
 
   Radio Service
 
   Français
 
   About IPS
 
   ENGLISH
   ESPAÑOL
   FRANÇAIS
   ARABIC
   ČESKY
   DEUTSCH
   ITALIANO
   JAPANESE
   NEDERLANDS
   POLSKI
   PORTUGUÊS
   SUOMI
   SVENSKA
   SWAHILI
PrintSend to a friend
Readers Opinions

UGANDA
Shinikizo Laongezeka Kufanya Mikataba ya Mafuta Kuwa Wazi kwa Umma
Na Joshua Kyalimpa

KAMPALA, Machi 4 (IPS) - Wabunge nchini Uganda wanashinikiza serikali kuweka wazi mikataba ya uzalishaji wa mafuta iliyosaini na makampuni mbalimbali ya mafuta ya kimataifa.

Wabunge wanashinikiza nyaraka hizo kuwekwa wazi kuwezesha bunge kupitia uzalishaji ambao utakuwa moja ya ugunduzi mkubwa zaidi wa mafuta katika Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara. (Mwaka 2009 kampuni moja ya mafuta ya kimataifa ilitangaza kugundua kile ilichokiita mafuta mengi zaidi kuwahi kugunduliwa nje ya ukanda wa pwani katika Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara katika kipindi cha miaka 20 iliyopita.)

Wasiwasi umeonyeshwa na maafisa mbalimbali wa serikali na asasi za kiraia (CSOs) juu ya kama kuna haki katika mpango huo baada ya taarifa kusikika kuwa Rais Yoweri Museveni alifanya mazungumzo ya moja kwa moja na wawekezaji katika sekta ya mafuta bila kushirikisha mashirika ya serikali.

John Arimpa Kigyagi, mjumbe wa kamati ya bunge inayohusika na maliasili, anasema wakati Feb. 21 kamati ilipata nakala za mikataba ya kugawana uzalishaji wa mafuta (PSAs) iliyosainiwa kati ya serikali na kampuni ya mafuta ya Tullow Oil, hawana uhuru wa kuelezea undani wa mikataba hiyo kwa wapiga kura wao. (Tullow Oil ni moja ya makampuni matano ya mafuta yaliyohusika katika PSAs nchini Uganda.) Kamati pia haina uhuru wa kutoa taarifa za undani juu ya mikataba hiyo kwa wabunge wengine.

Hata hivyo, wabunge 60 kati ya 300 wamesaini hati ya kupinga ambayo itawasilishwa bungeni kushinikiza serikali kutoa taarifa bungeni juu ya maudhui ya mikataba hiyo.

Hati hiyo ilianza baada ya mikutano ya ushauriano kufanyika na CSOs na wabunge – ikiwa ni pamoja na wale wanaotoka kamati za maliasili na uchumi wa taifa. Kamati hizi mbili zinashughulikia masuala yanayohusiana na sekta ya mafuta, ambayo imechukua nafasi kubwa tangu Uganda ilipogundua mafuta kwa mara ya kwanza mwaka 2006.

Ugunduzi wa mafuta nchini Uganda tayari unavutia washiriki wakubwa kama kampuni kubwa ya mafuta ya Italia ya Eni Spa, kampuni ya Kimarekani ya Exxon Mobil, kampuni ya Ufaransa ya Total na hivi karibuni kampuni ya Kichina ya National Offshore Oil. Nchi hiyo haina fedha kufadhili uzalishaji wa mafuta na badala yake imetia saini mikataba na makampuni makubwa ya mafuta inayoelezea jinsi gani mapato yatagawanywa na wawekezaji wenye nia ya kutoa fedha katika awamu ya uzalishaji.

Makampuni yatajenga mitambo ya kusafishia mafuta nchini Uganda na bomba la mafuta hadi katika Bandari ya Hindi. Hii itawezesha nchi hiyo isiyokuwa na bandari kuuza mapipa yake ya mafuta yasiyosafishwa yanayokadiriwa kuwa bilioni mbili kimataifa.

Hati ya upinzani ya wabunge ni ya karibuni zaidi katika upinzani dhidi ya PSAs. Mwishoni mwa mwaka jana, kwa kusaidiana na shirika la haki za binadamu la Human Rights Network (HURINET), waandishi wa habari Charles Mwangushya na Angelo Ezama walifikisha kesi mahakamani kutaka kushinikiza serikali kutoa taarifa za undani kuhusu mkataba wake na Tullow Oil.

Serikali ilishinda katika hukumu hiyo. Feb. 4 hakimu mkuu Deo Sejjemba, wa wilaya ya Nakawa katika mji mkuu wa Kampala, alikataa kutoa amri ya kushinikiza serikali akisema wapinzani wameshindwa kushawishi mahakama kuwa kupata nyaraka hizo kuna maslahi kwa umma na kwamba kungekuwa na faida kwa Waganda wote. Sejjemba alitoa uamuzi kuwa serikali hailazimishwi kutoa taarifa zote inazomiliki na ina haki ya kutokutoa taarifa kwa umma pale inapoamini kuwa kwa kufanya hivyo kutatishia usalama wa taifa.

Mbunge wa Kampala ya kati, Nabilah Sempala, anasema bado wabunge wanataka PSAs kuwekwa wazi kwa umma. "Tunasubiri tu kikao cha bunge kuwasilisha hati yetu ya upinzani na tuna imani hati hiyo itafanikiwa," anasema Sempala.

Suala la mikataba inayoelezea jinsi gani mafuta yatagawanya kati ya serikali na washirika wake wa madini baada ya uzalishaji limekuwa na msuguano kwasababu serikali ilikataa kuweka mikataba hiyo wazi tangu makampuni yaliyokuwa yakitafuta mafuta yalipogundua mafuta hayo tangu Februari 2008 katika eneo la Albertine Graben, mkoa katika upande wa magharibi wa bonde la ufa unaopakana na nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.

Serikali inasisitiza kuwa mikataba hiyo ina faida kwa Uganda lakini ni vema ikawa siri kwa sababu za kiusalama. Waziri wa Nchi anayehusika na nishati, Peter Lokeris, anasema Uganda haiwezi kuiweka wazi mikataba hiyo kwa umma kwasababu ya vifungu vya kutokutakiwa kuweka wazi mikataba hiyo.

"Makampuni ya mafuta yapo katika biashara na yasingependa kutoa taarifa za undani za mikataba yao ya mafuta na kujulikana kwa washindani wao katika biashara," anasema Lokeris.

Mohamed Ndifuna, mratibu wa taifa wa HURINET, aliiambia IPS kuwa kushindwa kwa kesi mahakamani kutoa taarifa za mkataba ni jaribio la Sheria ya Upatikanaji wa Habari ya mwaka 2005 nchini. Sheria inasema kuwa kila mwananchi ana haki ya kupata taarifa na rikodi za serikali au chombo chochote kile cha umma labda pale tu inapoingilia usalama wa nchi, uhuru wa nchi au haki ya mambo ya mtu binafsi. Ndifuna anasema tangu sheria hiyo ilipopitishwa na serikali haijatimiza jukumu lake la kutoa taarifa za serikali kwa umma kama inavyotakiwa na sheria.

Serikali ya Uganda tayari imeshapitisha ofa ya dola bilioni 1.5 kutoka kwa Tullow Oil kununua asilimia 50 ya hisa za mshirika mwingine wa uzalishaji wa mafuta nchini Uganda, Heritage Oil. Hii iliashiria mwisho wa msuguano kati ya makampuni ya mafuta baada ya Heritage Oil kutangaza kuuza asilimia 50 ya hisa zake kwa kampuni ya Italia ya Eni Spa kwa kiwango hicho hicho cha fedha.

Hata hivyo, mashirika ya kiraia yana wasiwasi kuwa wakati serikali inatakiwa kuanza uzalishaji wa awali, mikataba ya PSAs kati ya Uganda na makampuni ya mafuta bado inabakia kuwa siri. Ndifuna alisema ukweli kwamba Museveni alishiriki moja kwa moja ni dalili mbaya kwani hajahusisha mashirika ya serikali yanayohusika katika PSAs.

"Bunge halijashirikishwa, Mamlaka ya Uwekezaji Uganda (UIA) pia haijashirikishwa. Sasa ni nani atabakia (katika hali kama hiyo) kama mambo yatakwenda vibaya?" Ndifuna aliuliza.

(UIA ni mamlaka yenye madaraka nusu chini ya serikali ambayo inafanya kazi na sekta binafsi na serikali kuendeleza ukuaji wa uchumi na maendeleo.)

Dickens Kamugisha, afisa mtendaji mkuu wa Taasisi ya Utawala wa Nishati Afrika, ana imani kuwa mikataba inaweza kuwa na matatizo na kwamba serikali haitaki kutoa taarifa za maudhui yake.

"Kama ilivyo kwa mataifa mengi ya Kiafrika yanayozalisha mafuta, kuna njama kati ya makampuni makubwa ya mafuta na serikali kuburuza wananchi na usiri wa Uganda juu ya mikataba ya mgawanyo unatia shaka," Kamugisha anasema. Waziri wa nishati na madini wa Uganda, Hilary Onek, anasisitiza Uganda ina mgawo mkubwa katika mkataba huo na makampuni ya mafuta.

Anasema kama mikataba hiyo ingeonyeshwa kwa umma ingetishia wengine ambao wangekuja kuwa wawekezaji na ingekuwa kwenda kinyume na mikataba iliyosainiwa na makampuni ya mafuta ambayo inataka kuwepo na usiri. (END/2010)

 

 








 Latest News from Africa
News in RSS
BURKINA FASO: Race to Achieve Goals on Sanitation
MALAWI: Innovative Campaigning by Women Candidates
SOUTHERN AFRICA: Realising Trade in Virtual Water
KENYA: Claim Disputed that Trade Measures "Aid" Counterfeiters
POLITICS-GUINEA: Women Amongst Also-Rans in Presidential Elections
ZIMBABWE: Badly Needed Work Begins on Bulawayo Water System
MADAGASCAR: Women Form Own Political Parties for Fair Representation
HEALTH: Uganda Authority Finding Less Counterfeit Drugs
TRADE-NAMIBIA: EU Backs Off on EPA
TRADE: Malawi Stands Firm on Conditions for Signing EPA
More >>
  Dernières Nouvelles
News in RSS
BURKINA FASO: Race to Achieve Goals on Sanitation
MALAWI: Innovative Campaigning by Women Candidates
SOUTHERN AFRICA: Realising Trade in Virtual Water
KENYA: Claim Disputed that Trade Measures "Aid" Counterfeiters
POLITICS-GUINEA: Women Amongst Also-Rans in Presidential Elections
A lire également>>