Inter Press Service News Agency
Saturday, July 31, 2010   23:30 GMT    
   Homepage
   World Service
   East Africa
   Southern Africa
   West Africa
   Central Africa
 
   Environment
   Health-HIV/AIDS
   Education
   Rights
   Politics
   Economics
   and Finance
   Development
   Energy
   Population
   Culture
 
   Radio Service
 
   Français
 
   About IPS
 
   ENGLISH
   ESPAÑOL
   FRANÇAIS
   ARABIC
   ČESKY
   DEUTSCH
   ITALIANO
   JAPANESE
   NEDERLANDS
   POLSKI
   PORTUGUÊS
   SUOMI
   SVENSKA
   SWAHILI
PrintSend to a friend
Readers Opinions

ZIMBABWE
Katiba Yaangaliwa Tena
Vusumuzi Sifile

HARARE, Machi 3 (IPS) - Mchezo mpya, kuhusu Katiba inayosubiriwa umevutia wengi miongoni mwa wanasiasa na mashirika ya kiraia ambao wanataka kutoa maoni yao juu ya rasimu mpya ya katiba inayokuja.

Mchezo huo, ambao ulifanyika mjini Harare Feb. 23, unaigiza mkutano wa kifamilia ambapo binti Constance ambaye ndoa yake inataka kujadiliwa anasubiriwa. Lakini binti hakutokea. Anachelewa: kutokana na kuwa na kazi nyingi katika kamati inayoandaa mikutano ya ushauriano na umma juu ya katiba mpya.

Mchezo unatumia mgawanyiko wa familia juu ya mipango ya ndoa ya Constance – kama vile kutokukubaliana juu ya kiasi gani kitozwe kama mahari, na nani apewe kiasi gani cha mahari – kuonyesha misimamo inayosigishana ambayo imeibuka juu ya katiba mpya ya Zimbabwe.

"Mchezo unauliza maswali mengi muhimu, halafu unajaribu kujibu maswali hayo juu ya jinsi gani sheria kuu mpya inaendeshwa na watu," mwongozaji Tafadzwa Muzondo aliiambia IPS. "Bado watu wana maswali juu ya masuala ya msingi ya mchakato huo, na kama mchango wa watu wa kawaida utathaminiwa."

"Mchezo unaangalia masuala ya watu hao ni akina nani, ni misingi gani na itikadi zinasababisha katiba kuwa ya kidemokrasia, umuhimu wa kuhakikisha uhuru wa kujieleza na maoni mbalimbali na mawazo yanayotoka kutoka pande mbalimbali za jamii."

Muzondo, mwigizaji maarufu nchini Zimbabwe, anasema wakati inaweza isiwe muhimu kutoa majibu, mchezo utaleta jukwaa jipya la mjadala kuhusu masuala mazito. Na wahusika wenye ujuzi katika utengenezaji wa filamu wanatekeleza kile kilichokusudiwa.

Katika jukwaa, familia ya Constance yenye hasira inauliza maswali juu ya nini kimetokea katika katiba ya sasa, kama katiba mpya ni muhimu, ni nini kimesababisha kukataliwa kwa rasimu ya katiba mwaka 2000 na matarajio ya kuwa na katiba inayotokana na watu.

Douglas Mwonzora, mmoja wa wenyeviti watatu wa Kamati ya Bunge ya katiba – kamati ya ndani ya bunge yenye kazi ya kuendesha mchakato – alikuwa na matumaini kuwa mchezo huo ungejenga sura mpya ya mchakato huo.

"Wao (wanasanaa) wamekuwa wa manufaa mno katika mapinduzi, vita na maendeleo mengine ya kihistoria ya kitaifa. Nina imani kazi ya sanaa kama hiyo itakuwa na jukumu muhimu katika kuhamasisha watu wetu juu ya haja ya kushiriki katika mradi huu wa kipekee kitaifa. Inatia moyo sana unapoona wanasayansi wanaleta matunda katika mradi."

Uandikishwaji wa katiba mpya ni miongoni mwa kazi kuu za vyama mitatu vya siasa vinavyounda serikali ya umoja wa kitaifa, chama cha Zimbabwe African National Union Patriotic Front (ZANU PF) na vyama viwili kutoka chama cha Movement for Democratic Change (MDC). Mchakato umecheleweshwa mara kadhaa kutokana na kukosekana kwa fedha na migogoro baina ya vyama.

Wakati kuanza kwa ushauriano wa umma nchini umecheleweshwa, shirika la Crisis in Zimbabwe Coalition (CZC) linaona mchezo huo kama mfumo mpya wa kuanza kuhamasisha mawazo na kukusanya maoni ya watu wa kawaida; shirika hilo linashirikiana na watengenezaji wa mchezo, Rooftop, kuupeleka nchini kote. Mchezo huo pia utatafsiriwa kwa lugha za kienyeji.

"Haihusu tu kuupeleka mchezo kwa watu, inahusu pia masuala ya msingi kuhusu watu," alisema MacDonald Lewanika, mkurugenzi wa CZC.

"Tunaona michezo ya kuigiza kama njia ya kuchochea mjadala juu ya mchakato na maudhui. Kitu ambacho mchezo unataka kufanya ni kuonyesha masuala ya msingi katika mchakato. Tunajaribu kufanya hivyo kwa njia ambayo haifafanui kwa undani na isiyoegemea upande wowote ule."

Lewanika alisema uchaguzi wa michezo ya kuigiza kama njia ya kuhamasisha mjadala juu ya katiba mpya kulijikita zaidi katika kutambua kuwa "jamii yetu haifanani", hivyo haja ya kuonyesha ujumbe kwa njia tofauti. Baada ya wiki mbili za kuonyesha mchezo katika Ukumbi wa Harare katika Kiwanja, CZC itashirikiana na watengenezaji kuueneza mchezo katika safari ya nchi nzima.

"Kama mashirika ya kiraia, kazi yetu kimsingi ni kuhusu kushirikisha watu katika masuala ambayo yanawaathiri. Kimsingi tunapeleka mjadala kwa watu. Kuna masuala yanayopingwa waziwazi katika mchezo katika mchakato huo," alisema Lewanika.

Kusubiri Katiba ni mchezo wa pili wa Chifunyise katika masuala ya wakati huo. Mwaka jana, aliandika mchezo mwingine wenye jina la "Heal the Wounds", ambao umelenga katika mchakato wa uponyaji wa serikali kitaifa, na masuala mbalimbali kuzunguka mradi huo.

Mchezo wao sasa upo wazi na kuangalia masuala nyeti ya sasa kama vile ushiriki wa wanawake katika mchakato huo, kukataliwa kwa rasimu mbalimbali zilizoandaliwa, mgawanyiko ambao umekumba mashirika ya kiraia kutokana na mchakato, matumizi ya nguvu kwa watu wa kijijini na vyombo mbalimbali vya siasa, ushiriki wa Wazimbabwe walioko uhamishoni katika mchakato, muundo wa timu zinazoshiriki katika mchakato, na haki ya makundi ya wachache wenye jinsi tofauti.

Kuna burudani kubwa wakati wanafamilia wanapojadili masuala "yaliyoelezewa" katika rasimu mbalimbali, na jinsi gani haya yanaweza kuathiri thamani ya jadi zao. Na wakati Babamnini, iliyochezwa na Silvanos Mudzova, ikitoka nje ya mkutano wa ndoa bila maamuzi yoyote, na ikawa wazi kwa wasikilizaji ni jinsi gani hakuna umakini kwa mchakato kuhitimishwa haraka kuruhusu watu kuangalia masuala mengine muhimu. (END/2010)

 

 








 Latest News from Africa
News in RSS
BURKINA FASO: Race to Achieve Goals on Sanitation
MALAWI: Innovative Campaigning by Women Candidates
SOUTHERN AFRICA: Realising Trade in Virtual Water
KENYA: Claim Disputed that Trade Measures "Aid" Counterfeiters
POLITICS-GUINEA: Women Amongst Also-Rans in Presidential Elections
ZIMBABWE: Badly Needed Work Begins on Bulawayo Water System
MADAGASCAR: Women Form Own Political Parties for Fair Representation
HEALTH: Uganda Authority Finding Less Counterfeit Drugs
TRADE-NAMIBIA: EU Backs Off on EPA
TRADE: Malawi Stands Firm on Conditions for Signing EPA
More >>
  Dernières Nouvelles
News in RSS
BURKINA FASO: Race to Achieve Goals on Sanitation
MALAWI: Innovative Campaigning by Women Candidates
SOUTHERN AFRICA: Realising Trade in Virtual Water
KENYA: Claim Disputed that Trade Measures "Aid" Counterfeiters
POLITICS-GUINEA: Women Amongst Also-Rans in Presidential Elections
A lire également>>