ZIMBABWE Sekta Isiyo Rasmi Yavutia Wahitimu wa Chuo Kikuu Ignatius Banda
BULAWAYO, Machi 1 (IPS) - Kutoka kusafiri na mabasi ya kizamani ambayo yalifanya safari ndefu za kuvuka mipaka katika ukiritimba unaochanganya mpakani, kuvumilia unyanyasaji wa kingono unaofanywa na wafanyakazi wa basi na maafisa wa forodha na kupoteza bidhaa zenye thamani ya maelfu ya dola, Irene Moyo mwenye umri wa miaka 28 ameshashuhudia kila kitu.
"Hii haitokani na kuwa na moyo uliozimia," anasema juu ya kazi yake na njia hatari nyingi ambazo ilibidi kupitia kama mfanyabiashara mdogo mwanamke mjini Bulawayo.
"Nimejitolea maisha yangu kutumika usiku mzima katikati ya mahali ambapo sipajui baada ya basi kuharibika, na unaweza kutarajia kitu chochote kile katika mazingira kama hayo. Mara nyingine nafikiri ni afadhali kwa wanaume kwani wenyewe hawaathiriki sana ikilinganishwa na sisi," aliimbia IPS. Ngono mara zote inakuwa ajenda yenye kipaumbele miongoni mwa wafanyakazi wa basi ambao wanaitarajia kama wanavyotarajia kupata fedha kutokana na maarifa yao ya kujificha wakati wa kuvusha bidhaa mpakani bila kulipa ushuru mkubwa.
"Katikati mwa eneo ambalo hata hulijui na usiku mnene, inabidi uwe tayari kuombwa ngono na wafanyakazi wa basi. Baadhi yao wanadhani kuwa ni suala la kawaida tu kufanya hivyo," anasema Moyo ambaye amekuwa akifanya safari za mara kwa mara kuvuka mpaka kwenda Botswana na Afrika Kusini kwa miaka mitano sasa.
Akiwa mfanyabiashara anayevuka mpaka mara kwa mara akisafirisha kiasi kikubwa cha bidhaa, Moyo anasema wafanyakazi wa basi ni miongoni mwa wafanyakazi wake anaopaswa kuwalipa.
Anawalipa dola zipatazo 130 kwa safari ili bidhaa zake ziweze kuvuka bila ya kuwa na usumbufu wa kulipa ushuru mkubwa.
Analipia kwasababu ana uwezo wa kufanya hivyo, anasema, lakini siyo wafanyabiashara wote wanawake wanaweza kutumia njia hiyo. Jambo la kuchagua ni kukubali kufanya ngono, kama ukikataa kuacha bidhaa zako mpakani au kujadili ushuru wa kulipa, ambao sehemu yake wafanyakazi wa basi hutumia kuwapa rushwa maafisa wa forodha.
Kinachofanya suala la Moyo kutokuwa la kawaida ni kwamba ni mhitimu wa chuo kikuu. Kama ilivyo kwa maelfu ya wahitimu wengine, Moyo hajawahi kufanya kazi katika ajira rasmi tangu alipomaliza chuo kikuu na kuhitimu shahada ya uandishi wa habari miaka kadhaa iliyopita. Anatoka katika kizazi cha Wazimbabwe ambao walikwenda chuo kikuu wakati nchi ikitumbukia katika mgogoro wa kiuchumi na kuwa na mfumuko wa bei ulioweka rekodi duniani, wakati makampuni aidha yakipunguza wafanyakazi au yakifunga biashara.
Hata hivyo, anasema hasikitikii sana biashara yake kwani imemfanya kununua nyumba na gari – mali ambazo wasomi wenzake wa fani ya uandishi hawawezi kuzipata.
Mfanyabiashara mwenzake Sarudzai Washaya, pia mhitimu wa chuo kikuu, anaendesha duka dogo la nguo za wanawake na urembo katika eneo la biashara mjini Bulawayo na ananunua bidhaa zake kutoka Afrika Kusini na Botswana.
"Kuna wakati najisikia nimechoka mno na kutaka kuacha, lakini fedha ninazopata siwezi kuzipata katika ajira rasmi na hivyo navumilia," aliiambia IPS.
Wanawake hawa mashujaa wamekuwa "tabaka la kati jipya" katika nchi ambapo ajira rasmi inazidi kukimbiwa kutokana na mishahara duni.
Mapema Februari mwaka huu, maelfu ya wafanyakazi wa serikali waliandamana wakipinga mishahara duni. Wafanyakazi wa serikali wanaripotiwa kuingiza kati ya dola 120 – 200 kwa mwezi, na wamekuwa wakishinikiza serikali kuongeza mishahara mara tano na kufikia wastani wa dola 630 kwa mwezi.
Moyo anapongeza elimu yake ya chuo kikuu kwani imemfanya kuwa ushawishi katika biashara ya kuvuka mpaka na kumfanya kuwa salama.
"Bado kuna unyanyasaji wa kimfumo dume hapa ambao umefanya maisha kuwa magumu kwa wanawake wanaofanya biashara kuvuka mpaka. Lakini elimu ya chuo kikuu ni jambo ambalo bado linatishia baadhi ya wanaume," anasema.
Likini kuwa na elimu ya chuo kikuu hakufanyi kuwa rahisi kuwezesha kuwa na mahusiano mazuri ya kifamilia wakati unapokuwa barabarani mara zote. Kwa wanawake walioolewa ambao wanafanya safari kadhaa kuvuka mpaka kununua bidhaa, Moyo anasema wengi wameachana na biashara, kwani waume zao wanahoji wake zao wanatumia usiku wao wapi.
Ukweli huu umesababisha wasiwasi miongoni mwa baadhi ya NGOs, kama vile shirika la "International Organisation for Immigration's Partnership on HIV and Mobility in Southern Africa (PHAMSA)", ambalo linasema kuwa wafanyabiashara wanawake wanaweza kuambukizwa VVU kwa urahisi wakati wakizungumza na wasafirishaji, maafisa wa forodha na wana hatari ya kubakwa na aina nyingine ya unyanyasaji wa kijinsia katika mazingira yasiyojulikana na hatari.
Pamoja na changamoto hizi na nyinginezo, Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Wanawake (UNIFEM) linasema kuwa wafanyabiashara wasiokuwa rasmi wa kuvuka mpaka wanachangia wastani wa dola bilioni 18 kila mwaka katika biashara kwenye Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika.
Wengi wao ni wanawake ambao Moyo ana imani kuwa biashara za mpakani zimefanya wanawake kunyanyaswa katika jumuiya zao ambapo ajira pekee ‘bora’ wanawake wanatarajiwa kuwa nayo ni "ile inayoonekana" ambapo kila mmoja anajua anakofanya kazi.
"Kama uko mbali katika kitanda cha ndoa kwa usiku mmoja tu, majirani wanaanza kuongea na hii inaongeza shinikizo kwa mume wako," Moyo anasema.
"Hakuna mtu atakayekuelewa unaposema basi liliharibika. Inaonekana kama maelezo ya kujitetea tu. Hivyo kwangu mimi, kutokana na kutokuolewa ina maana naweza kuweka nguvu zangu katika biashara bila kujieleza kwa mtu yoyote yule Lakini nitakuwa wa kwanza kukubali ni maisha ya upweke," anasema Washaya.
Wakati baadhi ya wafanyabiashara wanawake wanaofanya vizuri kama Washaya na Moyo wana uwezo wa kuwa na magari yao wenyewe, kuvuja jasho, kwa uhakika, kama ambavyo Moyo anaelezea, siyo kwa ajili ya wenye moyo uliozimia, hasa kutokana na msaada mdogo rasmi kutoka serikalini, na washika dau wengine.
"Msaada wa kifedha umekuwa sehemu ngumu zaidi. Hatuwezi kupata mikopo ya benki kwani mabenki yanasema biashara zetu zina hatari kubwa ya kupoteza fedha huku mengine yakisema hayatoi mikopo katika uchumi kama wetu," anasema Washaya.
Wakati Wizara ya Biashara Ndogo ndogo na za kati inaendelea kuendesha warsha za mafunzo kwa wafanyabiashara vijana wa kike, Moyo anasema hawapati kitu chochote kutokana na mafunzo hayo katika suala la mikopo ambayo anasema anaihitaji mno kuweza kupanua biashara yake.
"Tuna uwezo wa kuendesha mambo makubwa zaidi na uwezo wangu wa kuendesha soko langu ni ushahidi wa jambo hilo, Moyo aliiambia IPS.
(END/2010)
|
|
|