Inter Press Service News Agency
Saturday, July 31, 2010   23:08 GMT    
   Homepage
   World Service
   East Africa
   Southern Africa
   West Africa
   Central Africa
 
   Environment
   Health-HIV/AIDS
   Education
   Rights
   Politics
   Economics
   and Finance
   Development
   Energy
   Population
   Culture
 
   Radio Service
 
   Français
 
   About IPS
 
   ENGLISH
   ESPAÑOL
   FRANÇAIS
   ARABIC
   ČESKY
   DEUTSCH
   ITALIANO
   JAPANESE
   NEDERLANDS
   POLSKI
   PORTUGUÊS
   SUOMI
   SVENSKA
   SWAHILI
PrintSend to a friend
Readers Opinions

HAKI
Samaki Watafanya Nini Katika Sahara Magharibi
David Cronin

BRUSSELS, Feb 27 (IPS) - Ushauri wa kisheria unaosema kuwa vyombo vya Ulaya havina haki ya kuvua samaki katika pwani ya Sahara Magharibi – jimbo linalokaliwa na Morocco – umezua msuguano kati ya taasisi kuu za kisiasa nchini Brussels.

Chini ya vifungu vya mkataba wa uvuvi mwaka 2005 kati ya Umoja wa Ulaya (EU) na Morocco, boti zinaweza kufanya kazi katika Sahara Magharibi, ili mradi tu shughuli zao zinakuwa na faida kwa wazawa wanaojulikana kama Wasahrawi. Lakini waraka mpya wa ushauri wa kisheria ulioandikwa na wanasheria kushauri Bunge la Ulaya umekuta kuwa hakuna ushahidi kama Wasahrawi wanafaidika kutokana na utekelezaji wa mkataba huo, ambao ulianza mwaka 2007.

Waraka huo wa ushauri unatetea kuwa jitihada zinatakiwa kufanywa kupata "ufumbuzi wa maridhiano" ambao Wasahrawi wanaweza kupata faida kutokana na mkataba. Lakini kama hakuna maridhiano, unasema kuwa boti za Ulaya zinapaswa kuzuiliwa kuingia maili 200 za ukanda huru wa Sahara Magharibi.

Pamoja na matokeo haya, chombo cha utendaji cha EU, Tume ya Ulaya, kinakataa kukubali kuwa mkataba huo umekuwa na matatizo. Maafisa wa Uvuvi wa EU walisema Tume "imeshawishika" kuwa mkataba huo "una faida za moja kwa moja na zile zisizokuwa za moja kwa moja katika jimbo la Sahara Magharibi."

"Mkataba unahakikisha kuwa shughuli za vyombo vya EU vinafanya kazi katika mazingira ya uwazi na yanayodhibitiwa na vimewezesha uwekezaji wa EU katika jimbo," afisa huyo, ambaye hakutaka kujulikana, aliiambia IPS. "Meli za EU zinapeleka baadhi ya samaki nchini Morocco, ikiwa ni pamoja na bandari katika Sahara Magharibi, jambo ambalo lina faida katika uchumi wa ndani. FPA (mkataba wa ushirikiano katika uvuvi) una mchango chanya katika uchumi wa Sahara Magharibi na kipato cha wakazi wake."

Morocco, ambayo ilivamia Sahara Magharibi baada ya wakoloni wa zamani wa Hispania kuondoka katika jimbo hilo mwaka 1974, itapokea jumla ya euro milioni 144 (dola milioni 196) kutokana na mkataba wa uvuvi wa miaka minne. Kulingana na waraka wa ushauri wa sheria kwa Bunge, mkataba huo "unakubali kuwa mamlaka ya Morocco yana mamlaka kamili" juu ya jinsi fedha inazopata zinatumika, hata kama mkataba huo una lengo la kukuza uvuvi "wa uwajibikaji na endelevu".

Aicha Dahane, mkimbizi Msahrawi anayeishi nchini Uingereza, alisema kuwa hakuna mtu aliyemfahamu katika Sahara Magharibi amepewa taarifa kwa njia yoyote ile wakati mkataba unajadiliwa. Wala hakumjua Msahrawi yoyote ambaye alipata ajira kutokana a utekelezaji wa mkataba.

Aliishutumu EU, pia, kwa kupindisha vipaumbele kwani ilitoa euro milioni 10 tu kwa mwaka kama msaada wa kibinadamu katika makambi ya wakimbizi Wasahrawi nchini Algeria, ambako watu 100,000 – nusu kutoka Sahara Magharibi – walikimbilia miaka ya 1970. " EU inalipa fedha zaidi kwa Morocco ili kuweza kuvua samaki kuliko inavyofanya kwa wakimbizi nchini Algeria," alipinga.

Mfumo wa EU kwa Sahara Magharibi unalinganishwa na ule uliochukuliwa na Marekani, ambao uliondoa jimbo hilo katika mkataba wa biashara mwaka 2004 kati yake na Morocco. Katika jaribio lake la kutoa sababu ya upanuzi wa mkataba wake wa uvuvi kwa Sahara Magharibi, Tume ya Ulaya ilisema kuwa kufanya hivyo kutazingatia waraka wa maoni ya kisheria wa Umoja wa Mataifa mwaka 2002. Lakini Hans Correll, mwandishi wa maoni hayo, alisema miaka sita baadaye kuwa "alichukizwa kama raia wa Ulaya" kuwa maoni yake yametafsiriwa kwa njia hii. Correll alisisitiza kuwa EU ingevua samaki tu katika pwani ya Sahara Magharibi kama ingepewa kibali na watu wa jimbo hilo.

Sara Eyckmans, mwanaharakati katika shirika la "Western Sahara Resource Watch", alisema Tume ya Ulaya hadi sasa "haijatoa hata punje ya ushahidi" kuunga mkono madai yake kuwa Wasahrawi walisaidiwa na mkataba. "Hii inakatisha tamaa na kutushtua," aliongeza.

Alisema kuwa mkataba ulikiuka sheria za kimataifa za bahari, ambazo zinasema kuwa uvuvi hauwezi kufanyika katika maji ambayo taifa husika halijaomba. Wakati Morocco imetuma maombi kwa jimbo la Sahara Magharibi, haijaelezea mipaka ya mamlaka yake katika maji hayo.

Wanasheria wa Bunge wanasema kuwa Sahara Magharibi inapaswa kuzingatiwa kuwa "ni jimbo lisilojitawala". Sheria za kimataifa zinataka kwamba matakwa ya wakazi katika jimbo hilo kuheshimiwa wakati rasilimali zao zinapotumiwa kwa ajili ya mafanikio ya kiuchumi, wanasema wanasheria hao.

Kukalia kwa Morocco Sahara Magharibi hamekuwa kukipingwa na maazimio mbalimbali ya Umoja wa Mataifa. Uamuzi wa mwaka 1975 wa Mahakama ya Haki ya Kimataifa pia ulikuta kwamba Morocco haikuwa na uhalali wowote kisheria kulikalia jimbo hilo.

Mchakato wa kisiasa una lengo la kujua mustakabali wa Sahara Magharibi umeleta mvutano kwa miaka mingi. Mwaka 1991, Umoja wa Mataifa uliendesha makubaliano ya kusitisha mgogoro wa kutumia silaha kati ya Morocco na chama cha Polisario Front, ambacho kiliwakilisha Wasahrawi, ambao ulianza mwaka 1976.

Wakati kura ya maoni juu ya msimamo wa kikatiba kuhusu Sahara Magharibi uliahidiwa kufanyika miaka ya 1990, lakini tangu wakati huo Morocco imekuwa ikizuia kura hiyo kufanyika. (END/2010)

 

 








 Latest News from Africa
News in RSS
BURKINA FASO: Race to Achieve Goals on Sanitation
MALAWI: Innovative Campaigning by Women Candidates
SOUTHERN AFRICA: Realising Trade in Virtual Water
KENYA: Claim Disputed that Trade Measures "Aid" Counterfeiters
POLITICS-GUINEA: Women Amongst Also-Rans in Presidential Elections
ZIMBABWE: Badly Needed Work Begins on Bulawayo Water System
MADAGASCAR: Women Form Own Political Parties for Fair Representation
HEALTH: Uganda Authority Finding Less Counterfeit Drugs
TRADE-NAMIBIA: EU Backs Off on EPA
TRADE: Malawi Stands Firm on Conditions for Signing EPA
More >>
  Dernières Nouvelles
News in RSS
BURKINA FASO: Race to Achieve Goals on Sanitation
MALAWI: Innovative Campaigning by Women Candidates
SOUTHERN AFRICA: Realising Trade in Virtual Water
KENYA: Claim Disputed that Trade Measures "Aid" Counterfeiters
POLITICS-GUINEA: Women Amongst Also-Rans in Presidential Elections
A lire également>>