NIGERIA Hakuna Kampuni ya Mafuta Itatambua Amani Katika Vikundi Sam Olukoya
YENAGOA, Feb 1 (IPS) - Vituo vitatu vya mafuta katika ukanda wenye mafuta mengi wa Niger Delta ilibidi vifungwe baada ya bomba la mafuta kuhujumiwa, kulingana na shirika la mafuta la Kiholanzi la Shell.
Kampuni hiyo ilisema kuvuja kwa mafuta Jan. 30 katika bomba la Trans Ramos kulitokana na hujuma, lakini hakuna kikundi hadi sasa kimedai kuhusika na shambulizi hilo.
Mwakilishi wa Kikundi cha Kukomboa Niger Delta aliliambia gazeti la Nigerian mwishoni mwa Januari kuwa kilikuwa kikimaliza mkataba wa amani uliofikiwa Oktoba 2009.
Msamaha
Msamaha na mpango wa kupokonya silaha ulioanzishwa katika Niger Delta Oktoba ulimaliza zaidi ya miaka mitano ya uasi uliofanywa na vikundi vya wapiganaji. Wanamgambo elfu ishirini kutoka vikundi mbalimbali walisalimu silaha zao kwa ahadi ya kupewa mafao ya kila mwezi ya dola za Kimarekani 430 kwa kila mpiganaji.
Wakati uasi ulimalizika, vikundi vinavyopigania kugawana mapato ya mafuta ya Nigeria vilishambulia mara kwa mara mabomba ya mafuta, viliteka wafanyakazi wa makampuni ya mafuta na kuuza mapipa yapatayo 100,000 kwa siku katika masoko ya uchochoroni. Kabla ya kupokonya silaha, wanamgambo walifanikiwa kupunguza uzalishaji wa mafuta nchini Nigeria kwa zaidi ya nusu.
Malalamiko makubwa katika Niger Delta ni kwamba mapato ya miongo mitano ya uchimbaji wa mafuta hayajaboresha maisha ya wanajamii. Badala yake faida zinagawanywa kati ya serikali ya Nigeria na makampuni ya mafuta yanayofanya kazi katika kanda.
Kuishi maisha ya juu
Kiongozi wa zamani wa wanamgambo Edward Udoiwei alikuwa mmoja wa wengi waliotengeneza fedha za haraka. "Nilipokuwa msituni, nilitengeneza zaidi ya naira milioni tatu (dola 20,000) kwa mwezi. Naweza kuita makampuni ya mafuta, 'Hey! Wavulana wangu wanaumwa njaa, leteni naira milioni mbili.' Na wangeweza kunijibu haraka," aliiambia IPS mwishoni mwa Desemba.
Mafao ya mwezi ya naira 65,000 ni chache sana kwa mbali ikilinganishwa na mamilioni ya naira ambayo viongozi wa wanamgambo walitengenezwa walipokuwa na bunduki katika vikundi.
"Ninacholipwa sasa kwa mwezi ndicho ninachotumia kwa masaa mawili au matatu msituni na wavulana wangu," anasema Udoiwei. "Nikiwa msituni, nina furaha zaidi ya hii. Napata fedha nyingi zaidi ya hii. N65,000 ni ndogo mno kwangu mimi kama kiongozi."
Ahadi zimevunjwa
Wanamgambo pia wana hasira kuwa serikali ya Nigeria bado haijatimiza ahadi yake ya mpango baada ya kupokonya silaha. Hii ni pamoja na kuingiza mpango wa ukarabati kama ambao ni muhimu kwa kujenga uwezo, mafunzo na kupata ujuzi wenye lengo la kubadili maisha yao kuwa mazuri zaidi.
Serikali ya Nigeria inasema programu hiyo haiwezi kuanza kama ilivyopangwa kwasababu hakuna vifaa kwa ajili ya ukarabati na mafunzo. Serikali imeomba wanamgambo ambao walihama kutoka katika makambi yao katika makundi kurejea kwenye miji kwa ajili ya kujengwa upya na kurejeshwa vijijini kwao wakati inajenga miundo mbinu.
Lakini wanamgambo wanasita kurejea nyumbani, wakisema kuwa hawana cha kufanya huko. Zaidi ya wanamgambo 6,000 wa zamani ambao walihamia Yenagoa, mji mkuu wa Jimbo la Bayelsa, wanabakia mjini, wakizurura mitaani bila malengo.
Serikali inasema lengo la msamaha ni kujenga hali inayofaa kuleta maendeleo katika kanda. Dk. Timiebi Koripamo-Agary, mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Rais, anasema mpango huo unatoa matumaini bora zaidi kwa mabadiliko ambayo wanamgambo wanadai.
"Msamaha huu unawapatia fursa za kuwa huru na kuwapatia haki ya kuzungumza kwa niaba yao wenyewe na kwa masuala ambayo wamekuwa wakidai na kupigania," anasema.
Kupooza kisiasa
Lakini – pengine kwa kudhoofishwa na maladhi makubwa ya rais wa Nigeria, Umar Yar'Adua – utekelezaji wa mpango huo umekwenda polepole. Uhujumu dhidi ya bomba hilo unaweza kuonyesha dalili kuwa uvumilivu wa wanamgambo umekwisha.
Mwanamgambo mwingine wa zamani ambaye alitoa jina lake kama Monday anasema itakuwa rahisi kwa serikali kufikia matakwa ya wanamgambo kuliko kumeza mashambulizi zaidi katika miundombinu ya mafuta nchini.
"Wanapaswa kutambua kuwa tutakuja kusababisha shida. Fedha ambazo wangetumia kwenda na kutatua shida hiyo, nadhani wangepaswa kutumia sasa kutatua kila kitu ambacho kinakuja hilo ni wazo langu," anasema.
Kwa upande mwingine, MEND – pamoja na kwamba haiko wazi ni sehemu gani ya uongozi wa kundi ambalo linahusika na taarifa – inapendekeza kuwa mwisho wa mapigano utakuja kwa gharama kubwa katika sekta ya mafuta ya Nigeria.
"Makampuni yote yanayohusiana na sekta ya mafuta katika Niger Delta yanapaswa kujiandaa na kubomolewa kwa miundombinu yake na watu wake. Hakuna kitu ambacho kitaachwa," inasema taarifa ya MEND.
Kama kikundi cha wanamgambo kitafanikiwa katika kitisho chake, sekta ya mafuta ya Nigeria inaweza kupaswa kujiandaa kushuka zaidi, na kuwa na madhara makubwa katika uchumi. Maana yake kwa maskini wa nchi hiyo – hasa kwa watu wa Niger Delta ambao bado ni maskini – hatakuwa nzuri.
(END/2010)
|
|
|