Inter Press Service News Agency
Saturday, July 31, 2010   23:09 GMT    
   Homepage
   World Service
   East Africa
   Southern Africa
   West Africa
   Central Africa
 
   Environment
   Health-HIV/AIDS
   Education
   Rights
   Politics
   Economics
   and Finance
   Development
   Energy
   Population
   Culture
 
   Radio Service
 
   Français
 
   About IPS
 
   ENGLISH
   ESPAÑOL
   FRANÇAIS
   ARABIC
   ČESKY
   DEUTSCH
   ITALIANO
   JAPANESE
   NEDERLANDS
   POLSKI
   PORTUGUÊS
   SUOMI
   SVENSKA
   SWAHILI
PrintSend to a friend
Readers Opinions

JUKWAA LA JAMII DUNIANI
Sierra Leone Inaona Fursa Zikipanda
Mohamed Fofanah

FREETOWN, Jan 29 (IPS) - Jukwaa la Kijamii Duniani lililofanyika mjini Nairobi mwaka 2007 liliwafanya wanaharakati wa Sierra Leone kujipanga kudai mambo kama vile nyumba, huduma za afya na uwajibikaji mkubwa kutoka serikalini. Hamasa hiyo haikudumu.

"Baada ya kurejea kutoka Kenya tulikuwa na siku tano kuu za mkutano katika mji wa pili kwa ukubwa nchini Sierra Leone, Bo," anasema Abu Brima, mkurugenzi mtendaji wa shirika lisilokuwa la kiserikali linalojulikana kama "National Movement for Justice and Development".

"Ulihudhuriwa na mashirika mengi ya kiraia na tulijadili mambo kama vile rushwa na jinsi gani ya kuifanya serikali kuwajibika kwa watu wake, jinsi gani ya kuifanya serikali kutoa huduma za nyumba na afya, na jinsi gani ya kuimarisha amani ambayo nchi imekuwa ikifaidi baada ya kuibuka kutoka kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe."

Brima anasema matokeo ya jukwaa hilo ni kuandaa mkakati wa mashirika yote ya kiraia wa kutumia katika kubuni programu zao za maendeleo na mapendekezo ya miradi. Pia ajenda ya vyama vya siasa kujitolea kama ambavyo wameahidi katika kampeni zao za uchaguzi wa rais na wabunge mwaka 2007.

"Uanaharakati huo wa kijamii haukudumishwa," aliongeza.

Lakini uanaharakati wa kijamii umepata mafanikio kadhaa. Mwezi Desemba 2007, watu katika wilaya ya madini ya Kono waliandamana kupinga mikataba iliyotolewa kwa makampuni ya madini, wakati ufuatiliaji wa serikali na udhibiti wa shughuli zao ulikuwa duni au haukuwepo kabisa. Hii ilipelekea kutungwa kwa sheria mpya ya madini ambayo – angalau katika karatasi – inasahihisha madhaifu mengi.

Brima alibainisha kuwa kwa mafanikio vijana walikosoa serikali mwaka 2009 kuanzisha Tume ya Vijana kama ilivyopendekezwa na Ripoti ya Tume ya Ukweli na Maridhiano mwaka 2004.

"Haya ni mafanikio ya msingi ambayo yalipatikana kutokana na harakati hizi, lakini mara tu baada ya mashirika haya ya harakati kusimama kwa miguu yao wenyewe yalianguka tena," alivuta pumzi.

Brima Abdulai Sheriff, mkurugenzi wa shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International nchini Sierra Leone, anapendekeza kuwa sehemu ya tatizo ni kwamba wanaharakati wengi wa mashirika ya kiraia wanaendeshwa na fursa za kifedha badala ya nia ya kweli ya kuleta mabadiliko. Sherrif ana imani kuwa wanaharakati pia mara nyingi hubuni kampeni zao ili kukidhi mahitaji ya wafadhili badala ya mahitaji ya watu. Halafu mara tu fedha zinapokauka kampeni pia hukauka nazo.

Sheriff alisema wanaharakati wengine wanaongoza mashirika ya harakati tu kutumia jukwaa hilo ili kupata nafasi ya kisiasa.

Anasema majukwaa mbalimbali ya kijamii yamekuwa muhimu katika kupanua shabaha yake ya shirika kuhakikisha watu wanaweza kushiriki katika maisha ya kiraia na kisiasa ya kitaifa bila kubaguliwa au kukandamizwa, hivyo haki za kijamii na kiuchumi kama haki ya chakula, nyumba na afya.

Sheriff alisema kuwa shirika la Amnesty leo hii linafanya kampeni dhidi ya vifo vya uzazi nchini Sierra Leone, ambayo ina moja ya hali mbaya zaidi ya afya ya uzazi duniani.

"Hata hivyo, mbali ya mashirika makubwa ya kimataifa kufaidi kutokana na WSF, mashirika ya harakati katika jamii nchini Sierra Leone ni vigumu mno kushiriki katika majukwaa haya." Sheriff alisema.

Jukwaa la Kijamii Duniani mwaka huu linafanya mfululizo wa matukio duniani kote. Tukio la Afrika lililopangwa hadi sasa litaangalia suala la kazi na uhamiaji, usalama wa chakula na umaskini, mtikisiko wa kifedha duniani.

Matukio haya, pamoja na jukwaa la kimataifa lililopangwa kufanyika mjini Dakar, Senegal mwaka 2011, yanatoa fursa kwa mashirika ya harakati za jamii nchini Sierra Leone kufikia mengine yanayokabiliwa na changamoto kama hizo kubadilisha mawazo na uzoefu na mikakati.

Sonnia Kabba, afisa wa haki za binadamu anayefanya kazi katika Tume ya Haki za Binadamu Sierra Leone, anaonyesha maeneo kadhaa kwa ajili ya mazungumzo yenye matunda na kushirikiana, ikiwa ni pamoja na mikataba kamilifu ya mabadiliko ya hali ya hewa na kufutwa kwa madini.

Kabba alishauri: "Sierra Leone inapaswa kuzingatia ukweli ambao unalinganisha na nchi nyingine duniani, tumepigika sana na matatizo yote ya kijamii na kiuchumi ambayo inasukumiza nchi katika kelele za mwisho katika Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu." Alisema ana matumaini kuwa mashirika ya kiraia ya Sierra Leone yatainuka katika hali endelevu na ya kujipanga kama harakati za kijamii mahali pengine duniani zimeweza kufanya katika kupigania haki zao na kwa ajili ya maendeleo.

Brima anakubaliana na maneno haya. "WSF ni mahali pa fursa ambako watu huja kutoka pande zote za dunia na kuwasilisha mawazo mbadala ya kiutawala, mifumo mbadala ya kiuchumi, na pia inaleta hisia za mshikamano. Sote tunaelezea haja ya kubadilisha jamii. Tuna fursa za kushirikiana na wengine na kujifunza maarifa kama vile ya utetezi. Kwa ujumla wake kuna hisia za kuvutia."

(END/2010)

 

 








 Latest News from Africa
News in RSS
BURKINA FASO: Race to Achieve Goals on Sanitation
MALAWI: Innovative Campaigning by Women Candidates
SOUTHERN AFRICA: Realising Trade in Virtual Water
KENYA: Claim Disputed that Trade Measures "Aid" Counterfeiters
POLITICS-GUINEA: Women Amongst Also-Rans in Presidential Elections
ZIMBABWE: Badly Needed Work Begins on Bulawayo Water System
MADAGASCAR: Women Form Own Political Parties for Fair Representation
HEALTH: Uganda Authority Finding Less Counterfeit Drugs
TRADE-NAMIBIA: EU Backs Off on EPA
TRADE: Malawi Stands Firm on Conditions for Signing EPA
More >>
  Dernières Nouvelles
News in RSS
BURKINA FASO: Race to Achieve Goals on Sanitation
MALAWI: Innovative Campaigning by Women Candidates
SOUTHERN AFRICA: Realising Trade in Virtual Water
KENYA: Claim Disputed that Trade Measures "Aid" Counterfeiters
POLITICS-GUINEA: Women Amongst Also-Rans in Presidential Elections
A lire également>>