Inter Press Service News Agency
Tuesday, February 09, 2010   14:52 GMT    
  Subscribe !
 

Enter your email and receive TerraViva Africa, our free weekly journal

   Homepage
   World Service
   East Africa
   Southern Africa
   West Africa
   Central Africa
 
   Environment
   Health-HIV/AIDS
   Education
   Rights
   Politics
   Economics
   and Finance
   Development
   Energy
   Population
   Culture
 
   Radio Service
 
   Français
 
   About IPS
   ENGLISH
   ESPAÑOL
   FRANÇAIS
   SVENSKA
   ITALIANO
   DEUTSCH
   SWAHILI
   NEDERLANDS
   ARABIC
   SUOMI
   PORTUGUÊS
   JAPANESE
PrintSend to a friend
Readers Opinions

AFRIKA:
Kuongezeka kwa Matumizi ya Simu za Mkononi katika Kupanga Uzazi
Susan Anyangu

KAMPALA, Nov 19 (IPS) - Kuongezeka kwa matumizi ya simu za mkononi, hasa katika nchi zinazoendelea, kunawapatia wataalam wa afya aina mpya ya mawasiliano kutoa taarifa za uzazi wa mpango.

"Idadi ya watumiaji wa simu za mkononi inazidi kuongezeka kwa kasi huku idadi ya watumiaji wa simu hizo duniani ikikadiriwa kufikia bilioni 2.6 mwaka 2006 kati ya wakazi bilioni 6.6," anasema David Cantor, meneja ufundi mkuu katika kampuni ya ICF Macro nchini Marekani.

"Takwimu hizi zinatarajiwa kuongezeka hadi bilioni 3.3 au wastani wa nusu ya idadi ya watu wote duniani ifikapo mwaka 2010, huku ongezeko kubwa likiwa barani Asia, Mashariki ya Kati na Afrika."

Cantor, ambaye alikuwa akihudhuria Mkutano wa Kimataifa wa Uzazi wa Mpango mjini Kampala, Uganda Nov. 15-18, anasema kuna ongezeko la nia ya sekta ya afya katika kuwekeza kwenye mawasiliano haya yanayokua kwa kasi.

Kampuni ya One World's Mobile4Good nchini Kenya inatumia teknolojia ya simu za mkononi kuwapa taarifa watumiaji kuhusu fursa za kupima au kupata tiba bure, na pia kutoa huduma ya maswali na majibu ambayo yanaruhusu watu mmoja mmoja kuuliza maswali nyeti ya kiafya.

Nchini Afrika Kusini na Botswana, teknolojia ya simu za mkononi inatumika kukumbusha watu wanaohitaji kupata dawa mara kwa mara.

Jamaica Corker wa shirika la Population Services International (PSI) – programu ya afya ya kimataifa inayolenga katika kupambana na malaria, maisha ya watoto, VVU/UKIMWI na afya ya uzazi – anasema mradi katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo ambako watumiaji wa simu za mkononi wanatumia laini ya bure kupata taarifa zinazohusiana na uzazi wa mpango kumeonyesha nguvu ya teknolojia ya simu za mkononi.

Tangu mwaka 2005, PSI imekuwa ikiendesha laini ya simu za bure ambapo wapigaji wanaweza kuzungumza na waelimishaji na kupata taarifa sahihi kuhusu uzazi wa mpango, au kupelekwa kwenye kliniki au famasi ya karibu, katika eneo ambalo mpiga simu anapatikana.

"Wakati ndiyo inaanza tu, mradi una lengo la kufikia wanawake zaidi, tumeshajifunza kuwa teknolojia ni njia inayofaa kufikia watu kwa ujumbe wa uzazi wa mpango," Corker anasema.

"Kutokana na kwamba wanaume ni idadi kubwa ya watumiaji wa simu za mikononi, wengi wanapiga kwa niaba ya wake zao au marafiki zao wa kike na tunafikisha ujumbe kwao pia."

Matumizi ya laini ya simu za bure ya PSI kwa wanaume wanaotaka taarifa za uzazi wa mpango kunaweza kuonyesha kuongezeka kwa nia ya uzazi wa mpangp miongoni mwa wanaume, pengine kutokana na usiri wa mawasiliano kwa kutumia simu za mkononi.

Kutokana na teknolojia ya simu za mkononi kushuka kwa kasi, Cantor anasema jukwaa limewekwa kwa ajili ya maendeleo ya kasi katika sekta.

Mbali ya kutoa taarifa za uzazi wa mpango, simu za mkononi zinatumiwa kama vyombo vya kufuatilia wagonjwa. Simu za mkononi pia zinatumika kukusanya takwimu za jamii na kliniki, kwa ajili ya kupeleka taarifa kwa wafanyakazi wa afya, watafiti na wagonjwa, na kufuatilia dalili muhimu za mgonjwa. (END/2009)

 

 
 Latest News from Africa
News in RSS
BIODIVERSITY: Companies Push Hard to Halt Tuna Collapse
ETHIOPIA: Dam Critics Won't Go Away
ENVIRONMENT: Keeping Wetlands from Becoming Wastelands
UGANDA: Early Diagnosis of HIV Still Elusive
KENYA: Insuring Pastoralists Against Increasing Risks
EGYPT: Minimum Wage Not Enough
SUDAN: Bashir May Face Genocide Charges
KENYA: Victory for Anti-Abortion Lobby
POLITICS-SUDAN: Security Essential to Ensure Peaceful Elections
NIGERIA: No Oil Company Will Know Peace in the Creeks
More >>
  Dernières Nouvelles
News in RSS
BIODIVERSITY: Companies Push Hard to Halt Tuna Collapse
ETHIOPIA: Dam Critics Won't Go Away
ENVIRONMENT: Keeping Wetlands from Becoming Wastelands
UGANDA: Early Diagnosis of HIV Still Elusive
KENYA: Insuring Pastoralists Against Increasing Risks
A lire également>>
 News in Swahili
News in RSS