Inter Press Service News Agency
Tuesday, February 09, 2010   13:42 GMT    
  Subscribe !
 

Enter your email and receive TerraViva Africa, our free weekly journal

   Homepage
   World Service
   East Africa
   Southern Africa
   West Africa
   Central Africa
 
   Environment
   Health-HIV/AIDS
   Education
   Rights
   Politics
   Economics
   and Finance
   Development
   Energy
   Population
   Culture
 
   Radio Service
 
   Français
 
   About IPS
   ENGLISH
   ESPAÑOL
   FRANÇAIS
   SVENSKA
   ITALIANO
   DEUTSCH
   SWAHILI
   NEDERLANDS
   ARABIC
   SUOMI
   PORTUGUÊS
   JAPANESE
PrintSend to a friend
Readers Opinions

Tahariri - Mario Lubetkin:
Changamoto za mkutano wa Nairobi


NAIROBI, Januari 23 (IPS) - Tumewasili katika mkutano wa saba wa maswala ya kijamii, kongamano la kwanza kabisa kuandaliwa Barani Afrika. Tumeshuhudia ufanisi wa mikutano mingine minne iliyoandaliwa Porto Alegre, Brazil na huko Mumbai India. Mnamo mwaka wa 2006, tulishiriki katika mkutano wa kwanza ulioandaliwa Bamako, Caracas na Karachi.

WSF imedhihirisha uwezo na nguvu zake miaka iliyopita kwa kuhamasisha mikutano ya maelfu ya watu kimaeneo, kimataifa na kutoka pembe mbali mbali za dunia na kupelekea kuwepo kwa matarajio na matumaini miongoni mwa mamilioni ya watu kote ulimwenguni, kwamba 'ulimwengu mwingine unawezekana''. Mikakati muhimu imeibuka kutoka WSF kama vile kuandaa juhudi za pamoja mwaka wa 2003 kuhusiana na amani, kupinga vita na kampeini iliyofana sana iliyozinduliwa mwaka wa 2005 kupambana na umaskini.(GCAP).

Baada ya miaka 7, maswali mapya yameibuka kuhusiana na hali ya baadaye ya WSF. Je, vuguvugu hili linaelekea wapi?Je, malengo yake ya baadaye ni yapi? Je, vuguvugu hili litakabiliana vipi na mabadiliko makubwa na kuwa na matumaini? Kila mmoja wetu anaweza kuwa na maswali mapya lakini ni muhimu kuangazia matumaini ya baadaye ya WSF.

Ni kwa sababu hiyo ambapo mashirika mengi mojawapo likiwa IPS linalokuletea TerraViva limekubali kujihusisha na shughuli mbali mbali zinazoangazia siku za awali za WSF, Nairobi. Madhumuni yake ni kufahamu yaliyotendeka miaka iliyopita kuhusiana na WSF, wajibu wa wanaharakati wa kijamii na kwa mujibu huu wajibu wa mikutano na pia uhusiano wake na mifumo ya kisiasa kwa kuzingatia serikali nyingi zilizoibuka tangu mwaka wa 2001 chini ya wafuasi wa WSF.

Sio tu kwa kupata majibu mahsusi lakini kwa kubuni taratibu za kujadiliwa baada ya mkutano wa Nairobi. Mawasiliano lazima yachukue nafasi muhimu katika mjadala huu ulio wazi na wa haki. Ni kwa sababu hiyo ndipo tumefanya kazi na mashirika rafiki kuandaa mkutano wa tatu wa kimataifa kuhusu habari na mawasiliano chini ya muktadha wa WSF, kuzidi kuimarisha ufahamu kuhusu mawasiliano na kwa jumla jamii nzima.

Lakini , kwa wakati huo, lazima tuwe na vyombo vya mawasiliano vitakavyotuwezesha kuangazia hatua za kuanzia mjini Nairobi. Kama ilivyokawaida, IPS, itatekeleza wajibu wake. Kwa washiriki wote wa kongamano la IPS mjini Nairobi , endeleeni kusoma jarida la TerraViva! (END/2007)

 

 
 Latest News from Africa
News in RSS
BIODIVERSITY: Companies Push Hard to Halt Tuna Collapse
ETHIOPIA: Dam Critics Won't Go Away
ENVIRONMENT: Keeping Wetlands from Becoming Wastelands
UGANDA: Early Diagnosis of HIV Still Elusive
KENYA: Insuring Pastoralists Against Increasing Risks
EGYPT: Minimum Wage Not Enough
SUDAN: Bashir May Face Genocide Charges
KENYA: Victory for Anti-Abortion Lobby
POLITICS-SUDAN: Security Essential to Ensure Peaceful Elections
NIGERIA: No Oil Company Will Know Peace in the Creeks
More >>
  Dernières Nouvelles
News in RSS
BIODIVERSITY: Companies Push Hard to Halt Tuna Collapse
ETHIOPIA: Dam Critics Won't Go Away
ENVIRONMENT: Keeping Wetlands from Becoming Wastelands
UGANDA: Early Diagnosis of HIV Still Elusive
KENYA: Insuring Pastoralists Against Increasing Risks
A lire également>>
 News in Swahili
News in RSS