Inter Press Service News Agency
Tuesday, February 09, 2010   14:54 GMT    
  Subscribe !
 

Enter your email and receive TerraViva Africa, our free weekly journal

   Homepage
   World Service
   East Africa
   Southern Africa
   West Africa
   Central Africa
 
   Environment
   Health-HIV/AIDS
   Education
   Rights
   Politics
   Economics
   and Finance
   Development
   Energy
   Population
   Culture
 
   Radio Service
 
   Français
 
   About IPS
   ENGLISH
   ESPAÑOL
   FRANÇAIS
   SVENSKA
   ITALIANO
   DEUTSCH
   SWAHILI
   NEDERLANDS
   ARABIC
   SUOMI
   PORTUGUÊS
   JAPANESE
PrintSend to a friend
Readers Opinions

NGUZU ZA WATU:
Kutoka majengo ya mabanda hadi ulimwengu mwingine
Na Joyce Mulama

NAIROBI, Januari 25 (IPS) - Waliandamana kutoka makao ya mabanda yaliyo makubwa zaidi kanda hii hadi Bustani ya Uhuru kutangaza kwamba ''Ulimwengu mwingine unawezekana'' na wakati huo kuzindua mkutano wa saba kuhusu maswala ya kijamii (WSF) siku ya Jumamosi.

Kongamano hili lililoanza Januari 20 hadi 25 limejumuisha pamoja maelfu ya wajumbe kutoka pembe zote za dunia ili kuweka pamoja ''haki za kijamii, umoja wa kimataifa, usawa wa kijnsia, amani na kuzuia uharibifu wa mazingira'' katika agenda za kimataifa.

Mkutano kuhusu maswala ya kijamii umewadiwa huku wanaharakati wa kijamii wakikabiliana na changamoto zinazoibuka kutokana na ''vita dhidi ya ugaidi'', ukosefu wa usawa kiuchumi unaosababishwa na utandawazi huku wanaharakati hao wakiombwa kudhihirisha uhalalishaji, uwazi na uwajibikaji.

Washiriki wengi walifurika katika Bustani ya Uhuru huku wakiwa wamevalia fulana zilizokuwa na maandishi na kupeperusha bendera na mabango baada ya kufanya maandamano dhidi ya umaskini yaliyoanzia mtaa wa Kibera ulioko karibu kilomita saba Kusini Magharibi mwa Jiji la Nairobi.

Huku ukiwa na idadi ya watu wapatao elfu 700,000, mtaa huu ndio mkubwa zaidi katika eneo la Afrika Mashariki. Katika mtaa huu, wajumbe walikumbana ana kwa a na hali ya kusikitisha ya umaskini, nyumba za matope,harufu mbaya iliyotokana na maji taka, ukosefu wa maji, barabara au huduma zozote. Katika Bustani, kila aliyezungumza alishutumu mataifa tajiri kwa kubuni sera zilizopelekea kuongezeka kwa hali ya umaskini katika mataifa yanayokua.

''Tunafahamu dunia tunayotaka. Dunia isiyotawaliwa na mataifa kutoka magharibi. Dunia yenye heshima na isiyo na madeni yaliyotokana na utawala huu.'' Chico Whitaker ambaye ni mwanachama wa Baraza la WSF akasema.

Swala kuhusu ugonjwa hatari wa HIV/AIDS lilichukua nafasi kubwa huku waliotoa hotuba wakisema janga hili limekuwa changamoto kwa mataifa yanayoendelea. ''Kuzuia ni bora kuliko kutibu.'' Akasema Rais Mstaafu wa Zambia Bw. Kenneth Kaunda. ''Ni lazima tukumbuke vituo vya kupimwa kwa hiari (VCT).

''Kujua hali yako ya afya na kujadili wazi kuhusu swala hili kutapunguza unyanyapaa. Siwambii jambo ambalo sijalifanya.'' Akasema Rais Kaunda ambaye alipimwa kwa hiari baada ya mwanawe wa kiume kuaga dunia kutokana na maradhi ya Ukimwi.

Mkutano wa WSF unaandaliwa chini ya mwito wake ''watu wanajitahidi, njia badala za watu''. Bw. Oduor Ong'wen ambaye ni mwanachama wa kamati andalizi ya mkutano alizungumuza kwa ufupi kuhusu matarajio ya mkutano kwa niaba ya TerraViva.

''Tunatarajia kwamba watu watajadiliana kuhusu dnuia ya sasa, jinsi ilivyo na kutafuta njia badala za kuwa na ulimwengu bora''. (END/2007)

 

 
 Latest News from Africa
News in RSS
BIODIVERSITY: Companies Push Hard to Halt Tuna Collapse
ETHIOPIA: Dam Critics Won't Go Away
ENVIRONMENT: Keeping Wetlands from Becoming Wastelands
UGANDA: Early Diagnosis of HIV Still Elusive
KENYA: Insuring Pastoralists Against Increasing Risks
EGYPT: Minimum Wage Not Enough
SUDAN: Bashir May Face Genocide Charges
KENYA: Victory for Anti-Abortion Lobby
POLITICS-SUDAN: Security Essential to Ensure Peaceful Elections
NIGERIA: No Oil Company Will Know Peace in the Creeks
More >>
  Dernières Nouvelles
News in RSS
BIODIVERSITY: Companies Push Hard to Halt Tuna Collapse
ETHIOPIA: Dam Critics Won't Go Away
ENVIRONMENT: Keeping Wetlands from Becoming Wastelands
UGANDA: Early Diagnosis of HIV Still Elusive
KENYA: Insuring Pastoralists Against Increasing Risks
A lire également>>
 News in Swahili
News in RSS