KONGAMANO LA KIJAMII DUNIANI Historia ya Bajeti Kukandamizwa na Mafuta ya Usiku wa Manane Joyce Mulama
NAIROBI, Januari 16 (IPS) - Huku zikiwa zimesalia siku chache kabla ya kufanyika kwa Kongano la saba la Kijamii Duniani (WSF) mjini Nairobi kila kitu kinafanywa na waandaji, ambao wanajiandaa kukaribisha maelfu ya wajumbe katika mji mkuu wa Kenya kuwa Jukwaa kwa ajili ya mkutano wa Januari 20-25.
Kongamano la kila mwaka litakuwa ni jukwaa kwa mashirika na watu binafsi ambao wanapinga mfumo wa sasa wa utandawazi – lakini pia linakabiliwa na changamoto ya gharama, bila kutaja kwamba mwaka 2007 utakuwa wa kwanza kwa Afrika kuwa muandaaji pekee wa tukio hilo. Kutokana na hili, tuna swali kwa ajili ya Onyango Oloo, mratibu wa kitaifa wa Kongamano la kijamii nchini Kenya, ambalo ni sehemu ya kamati ya maandalizi ya WSF ya mwaka 2007.
IPS: Uko tayari kwa ajili ya WSF?
Onyango Oloo (OO): Siyo tu kwamba tupo tayari kwa ajili ya WSF ya mwaka 2007, tunasubiri kwa hamu tukio hilo kufanyika. Tumechoma mafuta ya usiku wa manane na kufanya kazi ngumu sana, timu yenye kipaji hapa katika sekretarieti ambayo imetokana na mkusanyiko wa watu mbali mbali duniani. Tuna Wakenya, Watanzania, Waganda, watu kutoka Salvador, Hondurus, Canada (na) watu kutoka Senegal, Zimbabwe, Tunisia na wengine wengi kutoka maeneo mbalimbali ya dunia. Tuna watafsiri wa lugha wa kujitolea, wataalam wa IT (teknolojia ya habari), na watu wengine wenye ujuzi ambao wanavuja jasho usiku na mchana kwa ajili ya kufanikisha Kongamano la Kijamii Duniani.
IPS: Kuna watu wangapi wamethibitisha kushiriki katika kongamano?
OO: Tumezidiwa na maombi ya kutaka kujisajili, hususani katika wiki hizi tatu za mwisho. Kutoa mfano
mmoja: (mapema mwezi huu) tulikuwa katika Ukumbi wa Muthuruwa (Muthuruwa ni eneo la makazi ya kipato cha chini kwa ajili ya wafanyakazi wa Shirika la Reli la
Kenya) tukizungumza na watu kuhusu WSF. Walikuwa na njaa kupata fomu za kujisajili. Kila siku tunaona watu wakitembea kuingia ofisini mwetu wakitaka kujua kuhusu wapi wanaweza kujiandikisha, kulipa ada – au kama tumepokea na kushughulikia fomu zao za kujiandikisha kwenye mtandao. Mtandao wa Kutoka (kikundi cha makanisa ya Katoliki katika maeneo duni) inaandaa kundi na watu binafsi kujiandikisha kwa kutumia mtandao wa makanisa na mashariki magharibi mwa makazi duni ya Nairobi.
Ni vigumu kuthibtisha watu waliojisajili, kwasababu siyo fomu…zote zimeshafanyiwa kazi. Mfanyakazi mwenzangu Oduor Ong’wen alisema mapema wiki hii kwamba kwa uchache watu 15,000 wameshaandikishwa, na hao ni Wakenya tu.
IPS: Je kuhusu uwakilishi wa kimataifa?
OO: Tunatarajia watu wengi sana kutoka duniani kote kutua mjini Nairobi. Tayari mamia wameshafanya hivyo.
Kila siku kuna mtu anapiga simu kutoka uwanja wa ndege kutueleza kuwasili kwake …Takwimu moja inajielezea:
kuna kikundi cha wanaharakati 250 kutoka Afrika Kusini, na hicho hakihusiani na idadi ya Waafrika Kusini watakaokuja kwenye mkutano kwa gharama zao wenyewe.
IPS: Ni changamoto gani ambayo umekutana nayo wakati wa kuandaa tukio hili?
OO: Pengine changamoto kubwa ilikuwa kiwango cha
kisaikolojia: kukabiliana na mitizamo, hususani kutoka Afrika, kwamba pengine kazi hii ilikuwa kubwa mno kwa sisi kuifanya barani Afrika. Kama ambavyo mmoja wa wafanyakazi wenzangu anapenda kurudia rudia: ilikuwa – ni – matarajio makubwa ya kushindwa kwa pamoja na matarajio machache sana ya kufanikiwa. Tumethibitisha wakati wote kwamba tunaweza kukabiliana na changamoto.
Chanamoto nyingine muhimu ilikuwa rasilimali. Ni muujiza kwamba tumeweza kufanya kazi na rasilimali tulizonazo, ambazo hadi hivi karibuni zilikuwa chini ya asilimia 50 ya lengo la bajeti yetu.
IPS: Nini kitapatikana kama moja ya zawadi ambayo umekutana nayo wakati wa kuandaa WSF ya mwaka huu?
OO: Jambo linalovutia zaidi ni jinsi watu wa Kenya na maeneo mengine ya Afrika wamekaribisha wazo la WSF katika eneo letu hili la dunia. Moja ya faida za karibuni za jambo hilo ni kumiminika kwa wafanyakazi wa kujitolea wakija kusaidia kufanikisha WSF mjini Nairobi mwaka 2007.
IPS: Je usalama ni suala la kuhofia, hasa ikizingatiwa Kenya imewahi kuwa mwathirika wa mashambulizi ya kigaidi miaka ya nyuma?
OO: Usalama siyo jambo la kuhofiwa sana. Nairobi imewahi kuwa mwenyeji wa mikutano mingi ya kimataifa na kikanda. Nairobi haina matatizo ya kiusalama kama ilivyo, mfano, New York, Montreal, Paris au Liverpool.
Mbali na hilo tumekuwa tukifanya kazi kwa karibu na serikali ya Kenya kuweka mifumo yote ya tahadhari.
IPS: Ni nini ungependa kijitokeze zaidi katika tukio hili?
OO: Watu waelewe nguvu chanya ya Kongamano Jipya la Kijamii Duniani, mawasiliano mapya na mitandao, na kumiliki mchakato mzima kwa kurejea katika jamii zao kufanyia kazi masuala maalum ya kijamii, kitamaduni, kisiasa, kiuchumi na mengineyo – huku wakiwa na mawazo ya kubadili ukweli wao kwa ajili ya mafanikio zaidi.
Ninatarajia, kwa mfano, kuwepo kwa ushirikiano mkubwa kati ya bara la Asia na Afrika – na uhusiano wa karibu na Caribbean, Amerika ya Kusini, na wazawa duniani kote. Ninataka makundi katika jamii yanayonyanyasika zaidi duniani kote, hususani wanawake, vijana, watu wenye ulemavu, watu wachache wanaofuata utamaduni na ukabila kupewa uwezo zaidi kujua asili yao.
(END/2007)
|
|
|