Afrika:
Rais wa Pili Mwanamke Afrika ana Imani ya Kushinda Uchaguzi

Reprint | | Print |

LILONGWE - Wakati Malawi ikielekea uchaguzi wa Mei 20, Rais Joyce Banda ana imani kuwa atashinda uchaguzi na kuitawala nchi hiyo kwa kipindi cha awamu ya pili
 
Katika mahojiano na IPS, Rais Banda alisisitiza mabadiliko chanya ambayo yamepatikana nchini Malawi tangu alipochukua madaraka Aprili 2012 kufuatia kifo cha Rais Bingu wa Mutharika.

Alielezea mabadiliko hayo kama kuleta mageuzi ya kiuchumi, kufanyia mabadiliko sheria za kikandamizaji, kubadili hadhi ya wanawake na kupambana na rushwa.

Lakini wengi wana imani kuwa kuonekana kwa rushwa kubwa katika sekta ya umma kunaweza kumwangusha.

Ripoti ya mkaguzi wa mahesabu ya Februari ilionyesha kashfa kuwa dola milioni 30 ziliibwa katika kipindi cha miezi sita tu mwaka 2013. Pamoja na kufungia zaidi ya akaunti za benki 30 na kesi 18 kuwa mahakamani kwa sasa, Banda amekabiliwa na shinikizo la kutakiwa kujiuzulu. (END//2014)

Back to radio index >>

Republish | | Print |