Afrika:
Bado Athari Zinaendelea Kuwepo kwa Waliopona Ubakaji Wakati wa Mauaji ya Halaiki Rwanda

Reprint | | Print |

KIGALI - Ikiwa Rwanda inatimiza miaka 20 tangu kufanyika kwa mauaji ya halaiki, wanawake ambao walikuwa wahanga wa ubakaji wakati wa mauaji hayo na ambao walipata mimba kutokana na ubakaji ni wanaendelea kuugulia maumivu mioyoni mwao.
 
Claudine, mmoja wa wanawake waliookoka mauaji hayo, bado hajamweleza mtoto wake wa kiume kuwa mimba yake aliipata kupitia kitendo cha ubakaji.

Akiwa emebakwa na wanaume saba, ambapo mmoja wao alimmwekea sime tumboni, na kuambukizwa VVU, Claudine aliokolewa na jirani wake wa Kihutu ambaye alimsaidia kukimbia.

Inakadiriwa kuwa kati ya wanawake laki moja hadi laki mbili na nusu walibakwa wakati wa mauaji ya halaiki nchini Rwanda.

Kwa mujibu wa mkurugenzi mtendaji wa shirika lisilokuwa la kiserikali la Foundation Rwanda, Jules Shell, idadi kubwa ya wanawake waliobakwa wakati huo pia waliambukizwa VVU. (END//2014)

Back to radio index >>

Republish | | Print |