Afrika:
Wakulima wa Mjini Nchini Zimbabwe Wahatarisha Kupoteza Mavuno

Reprint | | Print |

HARARE - Wakulima wa mjini katika jiji la pili kwa ukubwa nchini Zimbabwe la Bulawayo, wanaweza wasipate mavuno mazuri waliyolima katika ardhi yao.
 
Hii inatokana na sehemu kubwa ya ardhi kumilikiwa na manisipaa ya jiji hilo na sheria ndogo nchini Zimbabwe zinazuia kilimo katika ardhi hii.

Hata hivyo, kwa mujibu wa Japhet Mlilo, mtafiti wa masuala ya maendeleo katika Chuo Kikuu cha Zimbabwe, kilimo cha mjini kinaweza kusaidia chakula na kupunguza uhaba wa chakula kwa wakazi wa nchini humo ambao tayari wanakabiliwa na mgogoro wa chakula.

Kwa mujibu wa wizara ya kilimo, taifa hilo linahitaji tani milioni 2.2 ili kukidhi mahitaji ya mahindi kwa mwaka.

Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa linakadiria kuwa zaidi ya watu milioni 800 duniani kote wanaendesha kilimo cha mjini na kimewezesha watu hao kukabiliana na kupanda kwa gharama za chakula na kupunguza kukosekana kwa usalama wa chakula. (END//2014)

Back to radio index >>

Republish | | Print |